Madaktari - tutakutana na waziri mkuu jumatatu

Vancomycin

Senior Member
Jan 7, 2011
171
111

TAARIFA MUHIMU: KULINGANA NA MAAZIMIO YA KIKAO CHAJUMUIYA YA MADAKTARI NA WAFANYAKAZI WA AFYA LEO TAREHE 28/01/2012, WANAJUMUIYA WOTE TUNAKUTANA TENA SIKU YA JUMATATU UKUMBI WA STARLIGHT HOTEL SAA TATU ASUBUHI. BARUA YA MAOMBI YA KUTUONA KESHO KUTOKA KWENYE OFISI YA WAZIRI MKUU IMETUFIKIA MIDA YA SAA KUMI NA MOJA JIONI NA IMEISHAJIBIWA RASMI KWA BARUA NA KUFIKISHWA NA KUPOKELEWA NYUMBANI KWAKE IKIELEZEA SABABU ZA KUTOKUWEZA KUONANA NAYE KESHO (SABABU MOJAWAPO KUWA NI WENZETU KUTOKA MIKOANI WAWEZE KUHUDHURIA MKUTANO HUO NA PIA BARUA KUFIKA BAADA YA MKUTANO KUAHIRISHWA MPAKA JUMATATU).
TAFADHALI SANA TUSIPOTOSHE TAARIFA HII. TAARIFA ILIYOTOLEWA TBC NI YA UPOTOSHWAJI.

NARUDIA TENA KUKUTANA NI JUMATATU SAA TATU UKUMBI NI STAR LIGHT NA WATAKUJA WAJUMBE KUTOKA MIKOA MBALIMBALI.
UKIPATA TAARIFA JITOLEE KUWATAARIFU WENGINEa

Source : Ukurasa wa facebook wa daktari mmoja ambaye ni mjumbe kwenye kamati ya kuratibu mgomo
 
Jamani si muitane kwa dharura mkutane naye mmsikilize. Hali ni mbaya wanaokufa ni watu wasio na uwezo wa kwenda Aga Khan na Regency. Madaktari wamegoma Muhimbili ila haohao wanenda Regency kuwatibu wenye vipato ambao ndio watoa maamuzi huku wasiojiweza wakikata roho huko Muhimbili. Jamani waoneeni huruma wananchi. Hivi Chama cha Madaktari ni kwa ajili ya Madaktari wote ama ni kwa ajili madaktari wa serikali tu?
 
nimekupata mkuu pia pande za fc bk. kumbe ni wewe.
big up msimamo mzuri sana. kuna fani zinatakiwa kufanyiwa siasa lakini si utabibu watajibeba mbafu zao!!!
 
wanaouliza ma'dr wanapata wapi hela za ukumbi, naomba niwajibu kwa uhakika kuwa wanachangia wenyewe kila wanapokutana, na kuna maprofesa na madokta wakubwa wanachanga pia...hadi watu wa wizarani wanachangia pia!hawamtaki blandna nyoni........wanataka reform kwenye wizara!

source:mwandishi wa habari anahudhuria vikao vya madokta.
 
Jamani si muitane kwa dharura mkutane naye mmsikilize. Hali ni mbaya wanaokufa ni watu wasio na uwezo wa kwenda Aga Khan na Regency. Madaktari wamegoma Muhimbili ila haohao wanenda Regency kuwatibu wenye vipato ambao ndio watoa maamuzi huku wasiojiweza wakikata roho huko Muhimbili. Jamani waoneeni huruma wananchi. Hivi Chama cha Madaktari ni kwa ajili ya Madaktari wote ama ni kwa ajili madaktari wa serikali tu?

Mkuu ni ngumu kuratibu hii ikitu kwani ki ukweli hatuwezi kugharimikia usafiri wa ndege kipato chetu ni kidogo sana kama unavyojua ndege one way ni zaidi ya laki mbili na nusu ambayo ni nusu ya mshahara wa daktari tutawezaje? hebu tafakari? labda kama waziri mkuu anaona hili ni suala muhimu na akaamua kuwafacilitate hawa wenzetu waweze kufika mapema tutashukuru sana kwa kweli kama vipi hata kesho mchana tukutane tutakuwa watu wa ajabu kama hatutashirikisha wenzetu wa mikoani ambao tumekuwa nao bega kwa bega tangu awali...

the truth is the gov doesnt give a damn how many people die they are there to proteect their politica interest huo ndio ukweli na katiba inasema wazi kuwa serikali ndiyo inayowajibika kutoa huduma ya afya kwa watanzania na sio mtu au taasisi nyingine yeyote

serikali haiwapendi wananchi wake hata kidogo ila inapenda kutupia mzigo kwa wengine

Guys inachosha na inauma sana Natamani mngekuwa kwenye hii sekta ya afya labda mngenielewa
wanasema wenyewe serikali huduma kwa kina mama na watoto ni bure lakini hawaleti vifaaa mahospitalini mgonjwa akikosa huduma anajua wafanyakazi wa afya wanachakachua sikatai ila kua wanaochakachua ila ukweli mara zaidi ya 85 kati ya mia seriikali inatugombanisha na wananchi wenzetu.......
 
Mkuu ni ngumu kuratibu hii ikitu kwani ki ukweli hatuwezi kugharimikia usafiri wa ndege kipato chetu ni kidogo sana kama unavyojua ndege one way ni zaidi ya laki mbili na nusu ambayo ni nusu ya mshahara wa daktari tutawezaje? hebu tafakari? labda kama waziri mkuu anaona hili ni suala muhimu na akaamua kuwafacilitate hawa wenzetu waweze kufika mapema tutashukuru sana kwa kweli kama vipi hata kesho mchana tukutane tutakuwa watu wa ajabu kama hatutashirikisha wenzetu wa mikoani ambao tumekuwa nao bega kwa bega tangu awali...

the truth is the gov doesnt give a damn how many people die they are there to proteect their politica interest huo ndio ukweli na katiba inasema wazi kuwa serikali ndiyo inayowajibika kutoa huduma ya afya kwa watanzania na sio mtu au taasisi nyingine yeyote

serikali haiwapendi wananchi wake hata kidogo ila inapenda kutupia mzigo kwa wengine

Guys inachosha na inauma sana Natamani mngekuwa kwenye hii sekta ya afya labda mngenielewa
wanasema wenyewe serikali huduma kwa kina mama na watoto ni bure lakini hawaleti vifaaa mahospitalini mgonjwa akikosa huduma anajua wafanyakazi wa afya wanachakachua sikatai ila kua wanaochakachua ila ukweli mara zaidi ya 85 kati ya mia seriikali inatugombanisha na wananchi wenzetu.......
Dr. Klinton hebu acheni upuuzi wenu eti wa kusubiria wenzenu wa mikoani and don't dictate terms, kesho nendeni mkamsikilize Pinda Jumatatu ni siku ya kazi, baada ya kesho mtatakiwa kuripoti kazini Jumatatu asubuhi!.

Hakuna ubishi kuhusu umuhimu wenu kama madaktari na hakuna anaepinga madai yenu ni genuine lakini lazima mfike mahali muwe na kiasi with moderations na kuwa more considarate kwa loss of lives zinazotokana na mgomo wenu!.

Msijitengenezee super class baada ya wabunge, walimu nao ni watu, polisi pia ni watu, watumishi wa serikali pia ni watu!. Msitarajie kupata preferential treatment kwa kushika roho za Watanzania as bargaining powers za madai yenu!. Public iko nyuma yenu mkikosekana kikao cha Pinda leo, public haitawaelewa!.
 
Mkuu Dr. Klinton pia tutafurahi kama mkijibu hizi hoja g
Nimejaribu kukaa kimya lakini nafsi yangu inanisuta. Siwezi kuendelea kukaa kimya. My opinion is unpopular, lakini nitasema.

Nitagusa hoja moja baada ya nyingine kama zilivyotolewa na "jumuiya ya madaktari".

Kuongezwa mshahara: Jumuiya imetoa tarakimu zisizo sahihi kuwa mshahara wa daktari ni sh. laki 7. Hii imeandikwa katika ripoti waliyoipeleka kwa waziri mkuu. Hii inadhihirisha kuwa jumuiya hii haiko serious katika hili swala. Lakini tuangalie uhalisia - jumuiya inataka mshahara uongezwe toka hiyo laki 7 (ambayo si sahihi) mpaka miil. 3.5 with immediate effect. Hivi kweli is it reasonable kudai ongezeko la asilimia 500 la mshahara na uongezwe mara moja la sivyo unagoma? Katika historia, swala hili madaktari hawajafanya jitihada za kujadiliana na serikali kidiplomasia. Ulipotokea mgogoro wa interns wa muhimbili kuhamishwa vituo, basi madaktari wakaibuka na kutaka mshahara wa 3.5 mil na kugoma. Mambo hayafanyiki hivi! Tukiwaambia madaktari waonyeshe barua waliyokwishawahi kuiandikia serikalli kuomba mshahara huo, hakuna atakayetoa barua au ushahidi wowote kwa sababu madaktari wameanza na mgomo moja kwa moja. Siungi mkono mgomo wa namna hii.

Madaktari kupewa nyumba: Mara nyingi adui wa daktari huwa daktari mwenzake. Hili swala la nyumba lilishajadiliwa huko nyuma. Nini kilitokea? Baada ya madaktari wa muhimbili kuthibitishiwwa kuwa wao watalipwa sh laki 4 kila mwezi basi chama cha madaktari ambacho viongozi wake wengi ni madaktari wa muhimbili wakapoteza interest ya kubargain na serikali ili posho hiyo wapate madaktari wa nchi nzima. Chama hicho kilikataa kabisa mara kadhaa kuitisha vikao vya kujadili posho za nyumba huku wakitoa sababu za kuepusha migomo. Sasa hivi inakuja "jumuiya ya madaktari" na kuilazimisha serikali kutoa posho hizo with immediate effect. Siku zote madaktari walikuwa wapi? Je walikuwa wanangoja interns wafukuzwe muhimbili ndio wakumbuke kuwa wanahitaji nyumba? Standing orders za mwaka 1994 zinaeleza kinaga ubaga kuwa daktari anastahili kupewa nyumba, standing orders za mwaka 2009 hazimtaji daktari katika watumishi wanaostahili kupewa nyumba. Maafisa utumishi wote wanatafsiri kuwa standing orders za mwaka 2009 zimemtoa daktari kwenye kundi la watakaopewa nyumba. Ni lini madaktari walienda kujadili hili na wizara ya utumishi? je ni sahihi kuanza na mgomo? Ili madaktari warudishiwe stahili hiyo ni LAZIMA kifungu kwenye standing orders za mwaka 2009 kifanyiwe marekebisho. Je, hilo linaweza kufanyika with immediate effect? Madaktari wamekuwa wavivu kufuatilia mambo yanayowahusu na siwezi kuunga mkono mgomo wa kundi la wavivu wa kubargain na kulobby.

Call allowance: "Jumuiya ya madaktari" inataka call allowance ilipwe kwa half per diem. This is very simple! Kwa nini mnagoma kwenda kazini during working hours? Ni kweli kuwa daktari anastahili kulipwa angalau sh. elfu 40 kwa call lakini solution yake ni rahisi kuliko zote. Madaktari waingie kazini, muda wa kazi ukiisha madaktari warudi nyumbani kama watumishi wengine. Wasikae call mpaka watakapokubaliwa kulipwa kiasi hicho. Kugoma kwenda kazini asubuhi kwa sababu ya malipo madogo ya zamu ya usiku doesn't make sense. lakini again, jitihada gani zimefanyika awali kuhakikisha call inaongezwa? Can doctors provide evidence of their effeorts? HAKUNA.

Mazingira duni ya kazi: Swala la mazingira duni ya kazi ikiwemo wagonjwa kulala chini sio la kulalamikiwa na madaktari. Hili swala waachieni wananchi wenyewe. Daktari unachotakiwa kujua ni capacity ya hospitali yako, beyond that usipokee mgonjwa. Ukishampokea basi unalea ubovu. MV Bukoba, MV spice zilizama kwa sababu ya kubebeshwa mzigo mkubwa kuliko uwezo wake. MV Muhimbili nayo inaingia kwenye hili kundi. Nani alaumiwe? Nahodha lazima awe miongoni mwa watu wa kulaumiwa. Kama madaktarri wataendelea kupekea wagonjwa wengi kuliko idadi ya vitanda it is obvious kuwa wengine watalala chini. hata Ulaya wangekubali kupokea wagonjwa wengi kulikoi uwezo kungekuwa na wagonjwa wanaolala chini. Ila Ulaya swala hilo halipo. Nafasi zikijaa zimejaa, mgonjwa apelekwe wapi, sio swala la daktari. Hata hiyo hospitali unayofanya kazi hujaijenga wewe daktari, ilijengwa kwa sababu mahitaji yalikuwepo. Ukiendelea kupokea wagonjwa wengi kuliko uwezo unaonyesha kuwa mahitaji sio urgent. Wagonjwa wakikosa pa kulazwa ndipo wananchi watashinikiza viongozi wao wawahakikshie facilities za kutosha.

Interns kuhamishiwa hospitali nyingine: Sababu iliyotolewa kuwa hospitali nyingine hazina vifaa inakosa uzito kwa sababu kuna madaktari ambao wapo huko kwenye hizo hospitali nyingine wanafanya intern. Hata hivyo hili swala ni so benign, haliwezi kusababisha mgomo nchi nzima.

Huduma huuzwa na kununuliwa. Bei ya huduma uamuliwa na nguvu za mahitaji na upatikanaji wa huduma. Hakuna daktari aliyelazimishwa kufanya kazi serikali. Kwanini madaktari wanakimbilia kufanya kazi serikalini? Madaktari wawe wakweli na watuambie faida zilizopo serikalini. kwanini madaktari wasitoe notice ya kuacha kazi serikali na kwenda kufanya kazi sehemu bora zaidi. Tanzania kuna soko huria. Kama watu walitumia mamilioni kwenda Loliondo basi hata daktari wanayeamini huduma zake watamfuata popote alipo. Madaktari mnangoja nini kutambua hili?

Mwisho: Mgomo ni risasi ya mwisho. Si sahihi kwa wasomi kutatua changamoto wanazokutana nazo kwa kuanzia na mgomo. Tanzania ni nchi masikini, ili umasikini huo uondoke ni LAZIMA tushirikiane WOTE kuutoa. Ewe daktari, jiulize ni mara ngapi umeingia kazini kwa muda unaostahili na ukafanya kazi mpaka muda wa kazi kuisha? Je, tabia yako ya kila siku kazini inachangia kuondoa umasikini wa nchi yetu? Kila mtu aweke jibu lake moyoni na kujiuliza tena, je mgomo unaoendelea hivi sasa unapaswa kuungwa mkono? Je, kwa siku hizi mlizogoma mshahara mnauchukua wote bila aibu?

Also: Am just curious, nani analipia gharama za kukodi ukumbi wa mikutano wa Starlight Hotel ambao madaktari wamekuwa wakikutania kwa siku kadhaa?!

Mungu Ibariki Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
inabidi tuwaambie hawa wana siasa nikipiga filimbi pale manzese naweza kupata mawaziri 100, lakini nitafuta ma dr kwa njia hiyo hiyo sehemu hiyo hiyo siwezi kupata dr 10

...labda utapata madoctor wa mitishamba :):) alias kikombe cha babu :)

 
Ni madaktari ndio wenye uamuzi wa jinsi ya kumaliza mgomo. Serikali ingekuwa na uwezo wa kumaliza mgomo isingeanzisha. I support the doctors.
Mkuu Mwanakijiji, hapa inatumika formular ya " anza wewe, mimi namaliza" na sio ile anayeanza ndiye lazima amelize!.

Madaktari wameanza mgomo na wana madai yao genuine kwa serikali, leo serikali itawapatia walichotaka na haitawaachia madaktari ndio waseme sasa wanarudi kazini, no!, itawaamuru wale wote wanaotaka ajira ya serikali, warudi na kazini by Jumatatu saa 2:00 asubuhi na wasiotaka wende kokote wanakotaka. Muda wa kumbelezana nao nwisho ni leo. Jana wamewahishiwa barua ya kikao cha leo pale Starlight, viongozi wao wakaigomea kuwatangazia wenzao!. Badala ya kuitika mwito sasa wao ndio wana dictate terms waitwe lini na wapi!.
Lets keep our fingers crossed ile hii deadlock imalizike leo, ikiachiwa mpaka Jumatatu it will be blown beyond proportion na posibbly to get off hand!.
 
Mkuu Dr. Klinton pia tutafurahi kama mkijibu hizi hoja g

ngoja nikujibu baadhi ya hoja. Suala la huduma mbovu: hivi ni mara ngapi umesikia vifaa hospitali havifanyi kazi? Ni mara ngapi hospitali hakuna dawa? Kama mpaka national hospital rbg machine zote mbovu kama zipo hazina strips tutafika? Mara ngapi wananchi wameandamana kudai haki hizo? Au unadhani daktari anapenda kuona mtu anamfia kwa kukosa vifaa? Haya yote viongozi wanajua ila bajeti nyingi zinaishia kwenye kununua magari ya starehe zao. Kuna mashine zingine wananunua kwa hela nyingi kumbe ni mbovu inatumika siku mbili imeharibika,tutaendelea kuvumilia huu uovu mpaka lini? Suala la wagonjwa kulala chini: kazi ya daktari ni kumuhudumia mgonjwa siyo kupanga idadi ya wagonjwa. Huwezi kugomea mtu ametoka kigoma yuko mbele yako usimuone. Hilo ni suala la watawala ambao wengi wao wamekuwa wanasiasa. Utoaji wa huduma kwa wagonjwa wanapokuwa congested unapokuwa mgumu ndipo kunapohitajika mabadiliko ya kimfumo na kiutendaji. Toka lini umeanza kusikia wagonjwa wanalala chini? Nini kimefanyika zaidi ya nyie wanchi kuendelea kupewa ahadi hewa? Mmeandamana masa ngapi? Tumechoka kuwabadilishia wagonjwa magonjwa na kupinda migongo yetu kuwahudumia wagonjwa wanaolala chini. Wananchi hawawezi kusema hata wakisema hawasikilizwi hata wakisikika utendaji hakuna,kwa nini tusiwasemee? ninaanza kupata picha kile pinda atakachoongea,hamjajipanga vizuri zaidi ya kuja na siasa. Kejeli za wizara ndizo zilizosababisha mvutano uendelee. Suala la intern: kila intern anaomba sehemu kulingana na matakwa yake na malengo yake ya baadaye siyo mtu kwenda mwananyamala ni sawa na kuwa mnh. Vitu vinavyopatikana mbeya siyo sawa na peramiho ndo maana kila mtu anaomba anakotaka kwenda, kwa nini umhamishe kama madai yake umeyakubali? Nani alianza kuvunja mkataba? Kwanza mambo yasingefika huku kama interns wangerudishwa mnh. Kejeli za wizara na kuonesha ni namna gani hawaijui wizara yao ndo zimesababisha kufika huku.
 
Madaktari imetosha!!!!! Walalahoi wanapopukutika, walengwa wa madai yenu viongozi wanapata athari kiduchu. Shime nendeni leo mkamsikilize Pinda . Madai yenu kuhusu malipo hapa TZ hayatekelezeki
 
Hoja ya zemacorpolo ambayo imeungwa mkono na pasco imeniharibia kabisa siku yangu. Bahati mbaya natumia simu, itanichosha sana kuandika. Nikiamka nitamjibu vizuri sana huyu ambaye dhahiri anaonekana ni miongoni mwa vigogo wanaofaidika na keki ya nchi hii. .
Lakini kuna jambo moja ambalo haliwezi kusubiri nalo ni wagonjwa kulala chini. Eti kwamba si suala la madaktari! Ktk dai ambalo drs wameonesha uzalendo ni hili. Ndo maana tunasema udaktari ni taaluma kama zilivyo taaluma nyingine ambapo hatimaye lazima kuwe na output. Positive output kwa daktari ni mgonjwa kupona. Kumbuka mgonjwa vs daktari ni tofauti na category nyingine mfano mwanafunzi vs mwalimu, mhalifu vs polisi, n.k. Anyway ngoja niache tu, kama haya majibu mliomwandalia PM, nendeni mkaya edit
 
zemarcopolo inaonekana nyie ndio mnaowapotosha viongozi wa nchi hii kwa manufaa yenu binafsi. Ndo maana hata washauri wa jk wanamshauri asafiri kila siku wao wapate mapato huku wakijua nchi imefilisika. Mbona mnabase kwenye marurupu ya daktari mnaacha kuzungumzia hali ya huduma ilivyo mbovu? Kwa nn siku zingine mgomo haukutokea? Hayo mambo ya maslahi ni vitu vilivyokuwa kwenye mazungumzo ila imefikia hatua utoaji wa huduma umekuwa mgumu ndo maana yameunganishwa yote. Imefikia hatua huduma haziendi mbele,madaktari wanalaumiwa na wagonjwa kwa ukiritimba wa wachache waliogeuza nchi hi shamba la bibi. Unataka yaanze na mazungumzo ya namna ya kuleta dawa hospitali? Unajua kwamba mnh vipimo vyote wagonjwa wanaenda kufanya hospitali za private? Na wale wanaohitaji serial investigations wataishi vipi?Ni wananchi gani mnaowaonea huruma kwa kuwaua taratibu na kuwaongezea stress watumishi wa afya kwa kuona wagonjwa wengi wakifa kwa uzembe wa watu wachache? Ni bora watu wachache wakafa kwa muda mfupi kuliko watu wengi kufa kwa muda mrefu. Eti daktari agome kuitwa call,hujui kwamba ile ni zamu ya kazi? Nikigoma mgonjwa akafa mtasema kama mnavyosema sasa? Sh 60000 kwa masaa 24? Mbona wabunge wanaenda kupeana mipasho masaa 7 tu, 200000? Tuendelee kubembeleza matatizo mengi kwa muda mrefu? kwa nn hawa shetani wengi wakazikwa kwa wakati mmoja ili wananchi wapate huduma nzuri? Hata hivyo wananchi waliowahi kutibiwa hospitali za umma wanajua tunachopigania na wanakubaliana nasi. Tunaomba msamaha kwa wale wachache walioathirika kwa ajili ya manufaa ya wengi. Mungu ibariki tz na uwalaani viongozi wanaokula mali za umma na vizazi vyao.
 
Back
Top Bottom