Madaktari tumieni busara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madaktari tumieni busara

Discussion in 'JF Doctor' started by Mwanajamii, Jan 22, 2012.

 1. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #1
  Jan 22, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Leo katika gazeti la Mwananchi , kuna taarifa ya Makamu wa Rais wa Chama cha madaktari Tanzania (MAT), Primus Saidia kwamba Majibu toka kwa mwakilishi wa ofisi ya Waziri Mkuu yamewakatisha tamaa. Aidha kuna taarifa kwamba huduma katika hospitali ya muhimbili imedorora na kwamba kuna dalili kwamba kuna uwezekano wa kuwepo mgomo siku ya Jumatatu yaani kesho.


  Pamoja na taarifa hiyo ya Dk Saidia , sikuona aya iliyotamka majibu walioyapata toka kwa Waziri Mkuu. Je majibu hayo ni siri?

  Najiuliza swali hilo kwa vile ninakuwa na wasiwasi sana kwamba, isije ikawa Madaktari nao wanalihusisha tatizo hilo na mambo ya siasa na kujisahau kwamba wao ni wataalamu. Watuambie ni majibu gani wamepewa toka ofisi ya waziri Mkuu ili watanzania tujue ukweli. Mimi naamini Serikali inatambua umuhimu watumishi wake wote na siyo Madaktari pekee. Busara zaidi zinahitajika toka kwa wataalam wetu hawa. Wapime, wakumbuke pia kuwa Serikali haijishughulishi na Madaktari tu. Ni wazi kabisa kwamba madai yao ni halali, lakini kutokana na ukweli kwamba siyo wao peke yao wanaohitaji kuhudumiwa na Serikali , wanaowajibu wa kuangalia ukweli wa viwango wanavyovidai kwa kutambua kwamba ni watumishi wa umma kama watumishi wengine kama mwalimu, mhandisi, askari na wengine wengi. Zaidi wajiulize na kutafakari juu ya nafasi zao na jinsi ambavyo sasa wagonjwa wanapata shida pale. Muhimbili.
   
 2. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #2
  Jan 22, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,019
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  kwani wamesema wanataka kuongezewa mshahara
   
 3. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #3
  Jan 22, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  inasemekana hiki ndicho kilichojibiwa kwa wawakilishi wa madaktari walivyoenda ofisi ya waziri mkuu.sasa kama ni kweli hapa ndipo utaona aina ya viongozi tulionao nchini.je ni yupi aliyepungukiwa busara?
   
 4. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #4
  Jan 22, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Nini tafsiri ya maneno yale ya aya ya mwisho kwenye gazeti la Mwananchi la leo. "kuna taarifa kwamba baadhi ya wakuu wa idara katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na hospitali nyingine nchini, wapo nyuma ya mgomo huo".
  Hizi sasa siasa. Hivi kweli yale madai yalioorodheshwa inawezekana Serikali ikayapuuza? Madai ya madawa, vitendea kazi, na kuangalia sheria ya uhamisho wa Madaktari bingwa ni miongoni mwa madai ya Chama cha madaktari Tanzania (MAT). Ukiangalia madai mengine yanahitaji marekebisho ya sheria, mengine yanahitaji fedha n.k. Mmi naamini kuna majibu ambayo Serikali imeyatoa ila kwa vile tu tayari tatizo limekaa kwa namna ambayo inaonekana kama kupata msukumo toka nje basi inabidi wataalamu wetu wasahau miiko ya kazi yao.
  Ndugu yangu mimi naungana na wewe kwamba busara zinahitajika katika suala hili.
   
 5. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #5
  Jan 22, 2012
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Busara waliyotumia kuua Azimio la Arusha? Busara za kuingiza Ufisadi na kudumaza uchumi wa inchi?

   
 6. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #6
  Jan 22, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  nimesoma madai yao, nawaunga mkono 100% na zaidi hili la kuboresha mazingira yao ya kazi, hawa watu wanafanya kazi ktk mazingira magumu sana na yote haya wameyavumilia kwa miaka 50, ward yenye uwezo wa kuchukua watu 30 inahifadhi wagonjwa 120, kuhudumia wagonjwa kwa kuchuchumaa kisa vitanda vimejaa hata gloves hakuna. Mazingira yakiboreshwa na sisi tutahudumiwa vizuri, tutalala mahali pazuri tukilazwa.
  madaktari watangaze mgomo na maandamano, mimi nitahudhuria.
   
 7. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #7
  Jan 22, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Madai yao ni ya msingi sana.Inashangaza watumishi wengine wakineemeka wakati kuna makundi kama ya hawa madaktari na walimu wakiendelea kuteseka.Watu wanaenda pale mahakama kuu kuhalalisha malipo ya kifisadi ya Dowans wanalipwa mamilioni kwa muda mfupi.Kwa nini madakitari!

  Naunga mkono hoja za madaktari ,Busara ni kuwaachia mafisadi waliochota fedha za walipa kodi mabilioni kwa mabilioni,tena wakipita mitaani kifua mbele kama mashujaa.Wanyonge wanapodai haki zao watulie wasubiri kwani subira yavuta heri.
  Wakidai haki zao Sio busara.

  Huu wimbo wa busara inavyoonekana ni kwa wanyonge pekee,wao ndio wanahamasishwa waimbe.

  Think about that!
   
 8. only83

  only83 JF-Expert Member

  #8
  Jan 22, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Inategemeana wewe una-define busara namna gani,kwangu mimi mgomo ni busara pia,inategemeana wamefanya jitihada gani kufikia suluhu ya matatizo yao.Busara ni kufanya mambo kwa kufuata kanuni na taratibu,kama taratibu jamaa wamefuata sana tena sana...nawapongeza kwa busara waliochukua badala ya kufikiria labda kuchoma wagonjwa kichwani au kuwapa dawa hovyo wameamua wakajikalie nyumbani mpaka serikali itakapoona umuhimu wao..kimsingi watumishi wa umma wamepigika wakuu.
   
 9. S

  SirBonge JF-Expert Member

  #9
  Jan 22, 2012
  Joined: Jul 18, 2010
  Messages: 349
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 60
   
 10. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #10
  Jan 22, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  kama hakuna hata vitendea kazi tuwatibu wagonjwa kwa makalio yetu? Wametugeuza ndio watu wa kutoa maelekezo ya pharmacy za kununua dawa badala ya kuagiza manesi wawapatie wagonjwa dawa. Wananchi naomba mjue mnh hakuna hata prescription form! Aafu njelekela yupo usa kula raha..
   
 11. DAWA YA SIKIO

  DAWA YA SIKIO JF-Expert Member

  #11
  Jan 22, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 985
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Umetumwa?!
  Anza na mbunge wako ambae pamoja na malupulupu kibao anayopata bado misuli ya shingo imemsimama anapigania posho ya kusinzia Bungeni.
  Ndo tutajua busara yako inafananaje!
   
 12. doctorz

  doctorz JF-Expert Member

  #12
  Jan 22, 2012
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 907
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Madaktari wamekuwa na busara kwa muda mrefu sasa. Kitaifa Afya ni sekta muhimu sana lakini serkali imewasahau madakatari sababu eti wanabusara. Kudai haki ni muhimu. Mimi niko pamoja na madaktari.
   
 13. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #13
  Jan 23, 2012
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,067
  Likes Received: 1,805
  Trophy Points: 280
  Hivi aliongea hayo maneno.. duh
   
 14. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #14
  Jan 23, 2012
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Mungu tubariki tunapokwenda kufanya maamuzi magumu leo hapo Don Bosco...tutumie busara, pasi na jazba...ila busara yangu, inaweza ikawa upuuzi kwako. Kwetu sisi madaktari..kwa sasa hali ilipofikia, na matusi ambayo tumeshatukanwa..MGOMO ni busara kwetu. Natanguliza samahani kwa waTanzania wote watakaoathirika na uamuzi wetu. Lakini gharama inabidi ilipwe, na tunatamani kama gharama hiyo ingelipwa na serikali...na si mwananchi mlalahoi mwenzetu! Lakini huyu mlalahoi naye ana jukumu kwa madaktari, kama kweli anathamini mchango wetu kwa jamii...na jukumu lake ni kuwa mkweli na kutusupport!

  Kama wanajamii ya Tanzania nao hawathamini mchango wetu katika kusimamia afya zao...basi sisi wa nini tena?! Hatuhitajiki, hata tukigoma hakuna athari! Lakini kama kutakuwa na athari, basi tunahitajika..na hivyo tuthaminiwe! We are going to DEMONSTRATE...demonstrate kuwa tunahitajika maana kuna malimbukeni serikalini na kwa baadhi ya wananchi hawajui hilo!

  Mungu uwe nasi....mungu uwe na waTanzania. Nikiwa mwanachama mwaminifu wa MAT tunasema...tunawapenda sana waTanzania, na tutaendelea kuwapenda!

  NB: Naelekea Don Bosco.
   
 15. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #15
  Jan 23, 2012
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160

  Matatizo mengi ya nchi hii yanatokana na ubovu wa viongozi ambao wamewekwa na Kiongozi mkuu ambaye pia ni mbovu.
   
 16. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #16
  Jan 23, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Ukiacha majibu ya kwa Waziri Mkuu ambayo me na wewe hatuyajui,lakin majibu ya Nyoni yanatoa majibu,usiseme jambo la kisiasa wakat madai yao yana hoja,we ndo unaleta SIASA
   
 17. Higash

  Higash JF-Expert Member

  #17
  Jan 23, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 844
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  wewe ndo huna busara kwa kuleta huu upuuz wako, tunagoma.
   
 18. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #18
  Jan 23, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Kama hela ya kuongeza posho za wabunge ipo, ya kuimarisha hali bora ya madaktari inakosekanaje? Kazi ya utabibu ni ngumu jamani, tena ikiisha kasheshe ya madaktari manesi nao wafuatie!!!
  Hao walala hoi wanaoteseka siku wakimjua mbaya wao watapata ahueni!
   
 19. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #19
  Jan 23, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  huyo atakuwa mmoja wa wale mwenye shibe hamkumbuki mwenye njaa..

  RIP TZ
   
 20. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #20
  Jan 23, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
   
Loading...