Madaktari Shinyanga watimua mbio baada ya mgonjwa kuonyesha dalili za ugonjwa wa Ebola

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
images

Kufuatia kuzuka kwa ugonjwa hatari wa Ebola katika nchi jirani ya Rwanda mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt,Ntuli Kapologwe amewatoa hofu wananchi wa mkoa wa Shinyanga juu ya uvumi wa kuingia kwa ugonjwa hatari wa Ebola mkoani Shinyanga.

Mganga huyo wa mkoa amewatoa hofu wananchi kufuatia kuenea uvumi kuwa kuna mgonjwa wa Ebola aliyefikishwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga kutoka moja ya mitaa katika Manispaa ya Shinyanga.

Kwa mujibu wa Mganga Mkuu huyo mgonjwa huyo ambaye alikuwa akitokwa damu mdomoni na puani alifika hospitalini hapo Agosti 12 mwaka huu na mara baada ya kufika wauguzi na madakitari walitaharuki.

Mgonjwa alilazimika kupelekwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) huku baadhi ya wauguzi na madaktari wakimkimbia hali iliyotia hofu kwa baadhi ya wahudumu na hata wagonjwa hospitalini hapo.

Hata hivyo Mganga Mkuu huyo alisema hakuna mgonjwa wa Ebola na kuwataka wananchi waamini hivyo na kuwa uongozi wa mkoa umejipanga kukabiliana na ugonjwa.

Alisema mgonjwa aliyepokelewa ana matatizo ya kutokwa damu mara kwa mara na kuwa baada ya uchunguzi wa awali imebainika siyo Ebola.

Hata hivyo katika kukabaliana na ugonjwa huyo waganga wakuu katika halmashauri zote 6 za wilaya za mkoa wamekubaliana pindi atakapogundulika mtu mwenye dalili za ugonjwa huo taarifa itolewe mara moja katika ngazi ya mkoa na kuna timu maalum ya kushughulika na ugonjwa huo hatari.

Alisema mara baada ya taarifa kutolewa timu hiyo ndiyo itakayo thibitisha kama kweli mgojwa huyo ana dalili zote za ebola na taarifa kutolewa.

Mganga huyo pia alisema hospitali zote katika halmashauri za mkoa wa Shinyanga zimepewa maelekezo juu ya kukabiliana na ugonjwa huo. mia
 
hawa ma daktari huwa wanasema hivihiv tu ila maji yakianza kuzidi unga wao ndo wa kwanza
kuhama mazingira hayo.. haya, sasa kwann wakimbie?
 
Wamekula kiapo cha kufanya kazi kaatika mazingira yoyote....sasa kwa nini watimue mbio
 
Ebola ni noma ee Mungu tuepushie gonjwa hili hatali

If your not right...go left,,
 
Wamekula kiapo cha kufanya kazi kaatika mazingira yoyote....sasa kwa nini watimue mbio

hicho kiapo labda cha kwakp hila nilichoapa miye hamna kitu kama hicho.. je wamepelekewa vifaa maalum vya kukabiliana na ugonjwa huo?otherwise hata mi nakimbia.early 2010 alipatikana mgonjwa wa rift valley fever ugonjwa ambao una dalili kama za ebola na nililazimishwa na mkuu wangu wa kazi kumhudumia bila protective gear yaani niliapa sitafanya tena uzembe kama huo
 
[haya kweli ni majanga siku za mwisho hizi tuombeni sana jamani kwa Muuma atuepushe:llama:]
images

Kufuatia kuzuka kwa ugonjwa hatari wa Ebola katika nchi jirani ya Rwanda mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt,Ntuli Kapologwe amewatoa hofu wananchi wa mkoa wa Shinyanga juu ya uvumi wa kuingia kwa ugonjwa hatari wa Ebola mkoani Shinyanga.

Mganga huyo wa mkoa amewatoa hofu wananchi kufuatia kuenea uvumi kuwa kuna mgonjwa wa Ebola aliyefikishwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga kutoka moja ya mitaa katika Manispaa ya Shinyanga.

Kwa mujibu wa Mganga Mkuu huyo mgonjwa huyo ambaye alikuwa akitokwa damu mdomoni na puani alifika hospitalini hapo Agosti 12 mwaka huu na mara baada ya kufika wauguzi na madakitari walitaharuki.

Mgonjwa alilazimika kupelekwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) huku baadhi ya wauguzi na madaktari wakimkimbia hali iliyotia hofu kwa baadhi ya wahudumu na hata wagonjwa hospitalini hapo.

Hata hivyo Mganga Mkuu huyo alisema hakuna mgonjwa wa Ebola na kuwataka wananchi waamini hivyo na kuwa uongozi wa mkoa umejipanga kukabiliana na ugonjwa.

Alisema mgonjwa aliyepokelewa ana matatizo ya kutokwa damu mara kwa mara na kuwa baada ya uchunguzi wa awali imebainika siyo Ebola.

Hata hivyo katika kukabaliana na ugonjwa huyo waganga wakuu katika halmashauri zote 6 za wilaya za mkoa wamekubaliana pindi atakapogundulika mtu mwenye dalili za ugonjwa huo taarifa itolewe mara moja katika ngazi ya mkoa na kuna timu maalum ya kushughulika na ugonjwa huo hatari.

Alisema mara baada ya taarifa kutolewa timu hiyo ndiyo itakayo thibitisha kama kweli mgojwa huyo ana dalili zote za ebola na taarifa kutolewa.

Mganga huyo pia alisema hospitali zote katika halmashauri za mkoa wa Shinyanga zimepewa maelekezo juu ya kukabiliana na ugonjwa huo. mia[/QUOTE]
 
Back
Top Bottom