Mparee2
JF-Expert Member
- Sep 2, 2012
- 2,586
- 4,273
Nimekuwa nafuatilia wasomi wazuri hasa wa Saiyansi kufikia hatua ya PhD na kuona kuwa kuwastaafisha eti kwa kuwa umri umefika kwamtazamo wangu sio sawa.
Kusoma na kufikia kiwango hicho cha Elimu wengi hufikia kwenye miaka 40 na 50. Naona ni hasara kumuachia mtaalam wa aina hiyo astaaf baada ya kutumikia kisomo chake cha PhD pengine kwa miaka 10 hivi na kustaafu
Kumbuka kuna reseach nyingi zinazotumia muda mrefu sana kuzipatia majibu mfano: Utafiti wa mbegu za Korosho hutumia takribani miaka 25 kupata mbegu/majibu halisi ya utafiti nk
Kitendo cha kuwaachia wataalam wetu wastaffu na kuanza kuwalipa part time (baadhi yao) nafikiri sio sawa; kwa nini wasiendelee hadi watakapo poteza uwezo wa kufanya kazi husika au pengine tuweke miaka 75 hivi?
Nakumbuka mtafiti wetu mmoja mbobezi (nafikiri ndiye alifanikisha utafiti wa Mbegu bora za Mihogo na Korosho ambazo zote ni hot cake hapa Africa na Asia) alistaafu miaka 4au tano hivi iliyopita kwa mujibu wa sheria; Miezi michache baadae Kachukuliwa Nchini Zambia kama mshauri mkuu wa Wizara ya Kilimo; binafsi niliona ni hasara kubwa kwa Taifa letu
Nijuavyo huko Ulaya mtu akishasoma kufikia Level hiyo hakuna kustaaf hadi apoteze uwezo wa kufanya kazi husika
Angazo: Mimi sio msomi wa daraja hilo.