Madaktari oneni hili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madaktari oneni hili

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, Jun 29, 2012.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hivi hao madaktari wameshaomba au wameweka awepo wakili aandike vithibitisho kutoka kwa dr na hata kurekodi kauli zake.
  Nawapa hongera madaktari waliojumuika na kuonyesha fani zao katika kuokoa maisha ya mwenzao ,juhudi mnazozionyesha na mafanikio mtakayoyapata inaonyesha wazi ni jinsi gani mlivyo na uwezo.

  uwezo na ujuzi mnaotumia usibakie hapo tu ,nikimaanisha muutumie kwa raia wengine ambao hawana uwezo wa kifedha wala uwezo wa kuwapa chochote ikiwamo rushwa ili mgonjwa wao apate tiba stahiki au angalau aweze kufaidi uwezo na juhudi zenu.

  Ondoeni ile senenesenene ya wananchi kulalamika ikiwa huna hela hupati matibabu hapo muhimbili au kwengineko ,ile tabia ya kumuona daktari pembeni ili mgonjwa wako atibiwe na kupata tiba ya uhakika muiondoe na kuifuta kabisa.

  Oneni jamii inavyoungana nanyi katika hili.Kuwalipa fadhila ni kuhakikisha huko twendako mnawapa huduma nzuri at first place bila ya kujali ni tajiri au masikini mnyonge ,waliomuokota Ulimboka ni hao hao wanyonge ,wanaokuja hapo mahospitalini na kuhitaji msaada wenu ni vizuri muwahudumie bila ya kuwadai au kutaka rushwa pembeni.
   
 2. Losomich

  Losomich JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 373
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Like down loading..............
   
 3. Nakapanya

  Nakapanya JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2012
  Joined: May 22, 2012
  Messages: 1,929
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 160
  excellent
   
Loading...