Jamani msikurupuke. Hiizo flats ni za NHC. Zimepangishwa kwa Muhimbili National Hospital ambayo nayo imepangisha madaktari wanaosomea degree ya pili ya udaktari bingwa. Miaka nenda rudi, wamiliki (NHC), MNH, pamoja na wahusika wa maji taka (DAWASCO) wameshindwa kutatua shida ya mfumo wa maji safi na taka. Sasa nyie mnataka hao madaktari wazibue na kujenga mfumo wa taka kwa mikono yao? Kumbuka, wanaoishi kwenye hizo flats hupangishwa kwa muda usiozidi miaka mitatu tu na kupangishwa watu wengine tena.