Camp Gilgal
JF-Expert Member
- Dec 13, 2014
- 4,453
- 4,595
Sasa wakiandika dawa moja tu kwa kila mgonjwa/mteja MAPATO ya kuendesha hospitali yatatoka wapi? Unajua, dawa ni moja ya chanzo kikubwa cha mapato ya hospitali, teh!Mkome kutupa dawa tano au sita sita mtatuua nyie,msikilizeni naibu wenuView attachment 873620
Anyways hoja yake ni ya msingi, "POLYPHARMACY" au "SHORTGUN THERAPY" sio nzuri otherwise mgonjwa awe na magonjwa zaidi ya moja na yasiyoingiliana mifumo au pale itakapoonekana itaongeza UFANISI na kuleta manufaa;
Katika magonjwa yanayoingiliana mifumo kwa mfano yale ya Presha, moyo nk, kuna dawa ambazo ziko katika muunganiko wa "Active ingredients" zaidi ya moja (FDC); Ni vizuri akapewa hizo ili kumpunguzia lundo la madawa na kumuongezea ufuasi mzuri.
Mara nyingi watu wanashindwa kuwa wafuasi wa dawa sababu ya kulundikiwa madawa kibao na mwisho wa siku tutatengeneza usugu kwenye jamii (hasa Antibiotics) na kutowasaidia ipasavyo.