Madaktari kushitaki serikali (MCT)

KML

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
861
133
Viongoziwa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Jumuiya ya Madaktari na Madaktari waliofukuzwa kazi na wengine kusitishiwa usajili wa leseni zao za muda walikutana jijini Dar es Salaam jana na kupitisha azimio la kuishtaki Serikali na Baraza la Madaktari mahakamani.

Umuzi huo ni matokeo ya ushauri uliotolewa na wanasheria kwa madaktari hao waliopendekeza hatua mojawapo ya kuchukua kuwa ni kulifikisha suala hilo mahakamani.

Mwakilishi wa Madaktari hao, Dk Frank Kagoro, alilimbia gazeti hili kuwa wamefikia hatua ya kwenda mahakamani kudai haki baada ya kugundua kuwa hatua waliyochukuliwa haikuwatendea haki.

"Tumekubaliana kutekeleza usahuri wa wanasheria wetu, tunafikiria kufungua kesi mahakamani kupinga kitendo kilichofanywa na Serikali cha kufukuza baadhi ya madaktari kutokana na mgomo na (MCT) kusitisha leseni za muda kwa baadhi yetu", alisema Dk Kagoro.
 
Mahakama ipi ?? Au hii hii ambayo inaelekezwa kitu cha kufanya na Mhimili mwingine !!!!
 
Mahakama hii ambayo ni mhimili wa dola uliowekwa mfukoni mwa kikwete,ccm na mafisadi?.....siamini km watasimamia haki zaidi ya kusimamia na kuilinda serikali yao dhaifu
 
yaani hapo ni sawa na mkulima anakwenda shambani anakuta Ngedere] amekula mahindi, naye mkulima anakwenda kumshitaki Ngedere kwa Nyani


Hapo hakuna kesi, wataambiwa "jambo hilo lipo mahakamani"


MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
ni utamaduni uliozoeleka kwa wale ambao hawawezi kudai haki zao hukimbilia nje, madaktari wana uwezo huo ila wanataka kuidai haki hiyo...Pambaneni kwa mnacho kiamini
 
Waachane na kesi, wakaombe kazi nje ya nchi ambapo JK na wenzake wanaendaga kutibiwa
 
Back
Top Bottom