Haya ndo matokeo ya kiburi na dharau ya hawa wanaojiita vigogo wa serikali. Hawako tayari kumsikiliza wala kufanya suluhu na mtumishi aliye chini yao. Kwa akili yao wanajua hawezi kuacha kazi kwa sababu atakufa njaa na familia yake. Hawajui kwamba hawa watumishi wanapothaminiwa tu kwa kusikilizwa kero zao na shida zao mbalimbali hata kama huwalipwi mishahara mikubwa, wako tayari kufanya kazi kwa imani kubwa kuliko kuwaona kama wenye njaa tu ambao hawana alternative.