Madaktari 38 waondoka nchini

Kiukweli katika hili, serikali haiwezi kukwepa lawama. Nafikiria ikiwa raia mmoja au wawili wa kizungu wanapokuwa hijacked, let's say, na pirates. Serikali zao hutumia resources nyingi sana ktk kuhakikisha kuwa mtu/watu wao wanakombolewa wakiwa salama. Sasa nimejaribu kufikiria watu ambao wamepoteza maisha tangu mgomo ulipoanza, hatimaye nimeridhika kuwa hakuna haki chini ya jua.
 

Kazi nyingine zote ni wito isipokuwa uongozi hapa tz hasa hasa ubunge hapo wito hakuna kabisaaaaa
 
Doctor migration to developed nations costs sub-Saharan Africa billions of dollars


Source
 
[h=1]Brain drain of African doctors costs sub-Saharan Africa billions, saved U.S. nearly $900 million[/h]
 
Hapo umenena "udaktari wa binadamu" si wito ni profession.Na kama ulikuwa ni wito tungewaweka kwenye ma-convent kama walivyo wamisionari, au wangekuwa monks waishi kwenye temples na iwe kazi yao ni kutibu kwa sadaka na sio kwa mshahara.
 
hii vita haina mshindi wanaoumia ni watu wengine kabisa kwani ma doctor watatibu watoto wao na viongozi watapeleka watoto INDIA
 
Mhe Pinda tukikimbiwa na madatari wetu hawa kwa madai ya nyongeza-kitumbua ndipo sasa mtakapoanza kuhha kutupeleka sote hadi WaTanzania akina kabwela sisi huku kwenda hospitali ya Appolo India kwenda kutibiwa kwa mamilioni?

Ama kweli mtu hujui thamani ya kitu mpaka siku unapoikosa katika maisha yako ya kila siku. Madaktari wanagombaniwa kila mahali duniani huku wakidai hela kiduchu tu ili kuendeleza uzalendo wa utumishi hapa nchini kwetu tu lakini sisi bado tunawarembulia????????

Hakika siamini kama mwajiri wa madaktari hapo wizarani huwa anachukua japo ka dakika moja tu kuoangania soko la madaktari ilivyochafuka ile mbaya kote duniani.

Laiti wakubw wangeju kwamba trend ya dunia haitupendelei hata kidogo hivi sasa kwa kuwa huko magonjwa yakiongezeka kwa kasi lakini idadi ya uzalishaji wa madaktari na manesi ikienda ikipiga tu dana dana tena ya kukatisha tamaa.

Mpaka hapa halafu eti ndio hata nchi yetu masikini bado inajidengulisha kwa madaktari kwa sababu tu viongozi wetu na familia zao madaktari wao wako nchini India na Afrika Kusini!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 

Tutegemee wengi zaidi watafuata wenzao kwenda kwenye nchi ambazo serikali zinawajari wataalamu wake. Serikli yetu imeridhika kwamba haihitaji kuona mazingira na vitendea kazi vya madaktari wetu vinarekebishwa kwa kuzingatia maombi ya Madaktari. Na kwa vile wafanya maamuzi wakiugua wanamahali pa kwenda kutibiwa hivyo serikali haioni umhimu wa hao madaktari kuwepo. Siamini na huenda sitakuja kuamini kwamba serikali yetu ipo kwa ajili wa kuwatumikia wananchi waliyoiweka ila ipo kwa sababu ipo. Kubwa linaloonekana na wengi wanalisema ni kwamba serikali yetu ni yakishikaji na hivyo na maamuzi yake ni ya kiushikaji.
 
Mtoto wangu alitaka PCB nikamwamuru PCM......Thanks God I did that

Mkuu ulifanya uchambuzi yakinifu kwanini mwanao alitaka kusoma PCB? Na wewe ulimpa sababu zipi za Kusoma PCM? Maoni yangu kwako mwache mtoto afanye kile kizuri kinachotoka moyoni mwake na atafanya kwa mafanikio ya juu zaidi!
 
Blandina Nyoni, ukatibu Mkuu si nafasi tu ya kujitutumua mbele ya jamii bali ni maamuzi maridhawa ya kuzingatia maslahi ya umma.

Hebu kajifikirie ki-undani zaidi kama bado huduma zako zitakua zinahitajika kwa WaTanzania kwa nafasi hii endapo tutaendelea kukimbiwa na madaktari zaidi kutokana na ubinafsi wenu wa kutojali maslahi ya wale wanaosota chini yenu.

Bure kabisa na wala hamna kitu pale wizarani - waziri wake ndio kabis yuko likizo katika kipindi hiki kigumu kwetu wenye hatari ya kukosa huduma za afya na tusiokua na uwezo kwenda nje ya nchi.
 

Wenyewe wanasema wataleta madokta kutoka JWTZ tena mabingwa kuliko waliogoma.
 
Ilani ya CCM imasemaje juu ya utoaji wa huduma za afya?
Na kuhusu masilahi ya watumishi wa Umma je?
 

Kuna siku hawa wanasiasa wataenda India na kukuta surgeons kule ni wabongo... sijui watarudi nyumbani?? au watatulia kama hawajui
 

Wenyewe wanasema wataleta madokta kutoka JWTZ tena mabingwa kuliko waliogoma.

Mkuu unajua mpuuzi akiongea, dawa yake ni kumpuuza tu.... ina maana hao madokta hawana kazi huko jeshini?? au watafunga hospitali za jeshi ili huduma zitolewe uraiani?
 
Mkuu unajua mpuuzi akiongea, dawa yake ni kumpuuza tu.... ina maana hao madokta hawana kazi huko jeshini?? au watafunga hospitali za jeshi ili huduma zitolewe uraiani?

Wao hawajali, wanafikiri wanawakomoa madokta waliogoma kuwa mmegoma lakini huduma bado zinaendelea na mishahara haiongezeki. Hawajali kuwa sisi walalahoi ndio tunaoumia kuliko wao Mafisadi, hospital zao zipo India
 
Tusifanye mzaha hapa; THIS IS A NATIONAL CRISIS POINT - swala la kukimbiwa na madaktari bingwa hata zaidi ya kumi tu ni ISSUE kubwa mno na nyeti ajabu kwa watu wanaoona mbali.

Tupo katika Tropical Country ambapo magonjwa ni kila kona, kipato hafifu halafu tena lije hili la kukimbiwa na madaktari kwa uzembe wa serikali yetu???????????????????


A MOST URGENT national debate is needed now and today, in the streets if our Parliament remains adamant, on this most delicate issue that touches on the life of our nation.
 
Kama madai yao yakiridhiwa, Dr atapata 7m kwa mwezi ikiwa ni mshahara na allowance na hii itafanya 2/3 ya pesa yote kwa ajiri ya mishahara ya watumishi wa umma iende kwa madaktari. Hii kitu haiwezekani. NUKUU YA WAZIRI PINDA.
 
utashangaa serikali hii ya jakaya kwao ni bora kuajiri kwa mkataba madakari wa nje
kwa malipo makubwa kuliko kuwalipa stahiki zao madaktari wetu na kuwatimizia mahitaji yao
serikalii hii kwao kuingia garama kubwa kwa jambo ambalo lingeepukika.
madaktari wana hali ngumu iweje mtu wa TRA apokee milion sita wkt daktari anaetibu na kutumia mda mwingi alipwe kiduchu
huwezi amini TRA wengi na rushwa zao kwa mwezi wao take home ni milion kumi.wizi mtupu
 
hili jambo la mgomo limekuwa la muda mrefu sasa limeshatuchosha ondokeni ili tujue tunajipangaje maana halipati ufumbuzi acha tufe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…