mgomo bora?....kwa hiyo wanastahili sifa kwa kusababisha vifo.!!!
Ukweli ma-dr wameitia doa taaluma/weledi wao. Ma-dr wa tz wamegeuka kichekesho cha dunia.
Wamekosa busara na hekima za kawaida kabisa ambazo hata konda na wasukuma mikokoteni wanazo.
Wamekalia tamaa na ulafi wa pesa, hata kama watz wenzao watakufa.
Wanatukuza taaluma yao kana kwamba wao ni miungu watu. Hawajui kuwa mkulima asipolima na kuwauzia chakula hawataishi.
Mtumishi wa DAWASCO akigoma kuwapa maji wanajua hali itakavyokuwa. Fundi wa TANESCO akigoma kumpa umeme anajua matokeo yake. Hata mzoa taka pale hosp akigoma dr hawezi kufanya kazi.
Wamekosa uelewa mdogo ....kwamba tunategemeana sana kila mtu kwa fani yake. Kwa kifupi uwezo wao wa kufikiri ni kichekesho na wamegeuka vilaza wanaokimbizana na pesa.
MS JUDITH, unazijua symptoms of profound mental retardation?
Basi kama ni kuboresha maslahi na kama madaktari wanatujali sana wananchi basi wasubiri kwanzA na polisi na walimu mshahara ufike 900,000 halafu na wao ndio tuwapeleke kwenye hayo mabilioni wanayotaka.
Wakati mwingine ukimya ni kauli tosha: hivyo ukimya wa madaktari uchukuliwe kama kauli inayojitosheleza ambayo yahitaji kusikilizwa kwa umakini mkubwa kupata ujumbe wake.
wapendwa,
hawa madaktari ni watu wa ajabu sana na tena ni wenye dharau kupita kiasi, wauaji wakubwa! hivi wasingebahatika kusoma kabisa wangekuwa na uelewa wa kiwango gani?
sasa mbwembwe zole zooote hadi kuuua ndugu na wapendwa wetu bila hatia yoyote, dawa yao ilikuwa ni juice ya ikulu? kwani hawakujua kabisa kuwa hawana uwezo wala uhalali wa kupanga baraza la mawaziri? pinda laishawaambia ukweli, wakamdharau! hivi kama kitu kile kile pinda alichosema kikashindwa kuwaridhisha, kiliporudiwa na jk kimewaridhisha, sasa tuwaeleweje? mbona akili kidogo tu hata inayotosha kwenye kijiko cha chai ingetosha kujua kuwa kwa unyeti wa sekta ya afya, hawapaswi kugoma? hawa wenzetu wana akili yenye ukubwa gani?
mtu akisikia mgomo anadhani ni jambo la kihunihuni, kumbe mgomo ni suala la kisheria na limeainishwa kisheria sababu pamoja na taratibu zake. sasa watwambie mponda na nkya hawang'oki na hawapewa hata senti moja hadi hivi sasa, hicho walichoahidiwa na jk ndicho alichwaahidi pinda, kwa nini walimpuuza pinda na kuua watu wasio na hatia?
hebu angalieni, daktari anaanza na mshahara wa laki 9+, sekta nyingine mtu mwenye shahada anaanza na laki 4+! hivi hata hapo hawaoni kuwa serikali inawachukulia kwa uzito mkubwa zaidi ya kada nyingine? hayo majivuno yao na kujiona kada yao iko juu ya kada nyingine ndiyo ya kukemewa kwa nguvu zote. kila mtu anajua nchi ilipo kiuchumi, hiyo neema wanayolilia kila siku, wanategemea itatoka nchi gani? au kila mtanzania ageuzwe ng'ombe akamuliwe maziwa (kodi) na maziwa yote wanyweshwe madaktari pekee?
napenda serikali ichukue hatua kuimarisha sekta ya afya pamoja na sekta nyingine, lakini nimehuzunishwa sana na uelewa wa mambo wa madaktari wetu pamoja na viwango vya upendo na maadili ya kazi zao walionao.
kumradhi wote niliowaudhu kwa maoni haya,
mbarikiwe sana
Glory to God!
mgomo wa madaktari utabakia kuwa mgomo bora kuwahi kutokea tanzania.busara waliyoonyesha madaktari ni kubwa kama ilivyotegemewa kutoka kwao.
Bint yangu ms judith naona wewe ni mchochezi usiyeamini kwenye maridhiano.
KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
Ms Judith, salaam sana,karibu tena jamvini ulipotea muda hivi.
Huo mshahara wa laki 9(900,000) kwa mwezi (siku 30) ni sawa na posho iliopendekezwa ya mbunge akikaa katika kiti chake kwa siku 4.5.( jumatatu-alhamisi na ijumaa hadi saa 6 mchana) Ni posho nasisitiza. Sijui hawa ni muhimu sana kuliko kada zingine!!
Spika Makinda alisema wabunge wa Kenya wanawacheka wa Tanzania, na nina hakika madaktari wa Kenya wanawacheka wa Tanzania. Sasa hapo kuna ubaya gani wakiomba waongezewe kama wabunge walivyoomba?
Kada nyingine kama walimu nao wanadai, umesahau Tucta ya mgaya ilikuwa inalalimikia nini. Kama Polisi na mabwana shamba kwa mfano, wameridhika na wanachopata kwanini wawazuie wengine wasidai haki zao?
Kuhusu Nkya na Mponda wao wamesema waendelee kuwepo kama ni busara lakini hawatawapa ushirikiano. Mdau wa sekta ya afya ni nani zaidi ya wataalamu waliomo. Mponda ni mpita njia tu kesho anaweza kuwa ujenzi n.k. Kama uwepo wake utakwaza watu kwanini wasifikirie wao kwanza halafu rais naye apime. Neno kutotoa ushirikiano ni pana na linagusa sehemu kubwa sana.
Ahsante
kama madaktari ni wauwaji ukiugua baki hapo nyumbani kwako. tuone kama wakati unakata roho hutaita daktari kwa sauti kuu.
na kwa kauli yako hii wewe ukiugua ni kifo tu, kisaikologia huwezi kupona kamahuna imani na daktari anaye kutibu. pole you are a deadly walking body.
aaah..madaktari wetu wa internet.,walosahau kuwa wamesomeshwa na kodi za hao hao waliowanyima haki ya kuishi..time will tell..guilty conscience will take its part..:crazy:
unajua mtu anakaa kuropoka tu aafu anataka aonekane naye amechangia. We unalinganisha daktari na mtu wa sociology kuna usawa gani? Daktari anasoma five years ukiongeza na internship inajuwa sita just for first degree we si unakuwa umemaliza mpaka phd? muwe mnafuatilia na nchi zingine wanalipwa kiasi gani,siyo just kukurupuka na inferiority complex na kusema tuko sawa kama kauli mbiu za vikao vya wanawake. Daktari hana weekend wala sikukuu na anafanya kazi 24 hours, wao wanafanya kazi masaa mangapi? Watu wawe wanajiuliza,ulishawahi kwenda hospitali ukaambiwa huu siyo muda wa kazi? Ulishawahi fika hospitali baada ya muda kuisha ukaambiwa njoo kesho. Kuna appointment ambazo doctor anakubaliana na mgonjwa wake kulingana na hali ya mgonjwa na uwezo wa hospitali. Tunatambua uwepo wa wengine na waliotuwezesha kufika hapa lakini we are not equal in importance, hata kichwa maji wa nchi hii aliwaambia!
unataka nani adai haki yako? Ndo maana mnanyanyaswa na mnakaa kimya. Mnatukanwa na ps wa mabosi wenu mnasubiri Mungu ndo aje awaokoe. Lazima ujifunze kupigania heshima yako na haki yako ndo utaipata..
Lazima weye ni mmoja wa waliopata kikombe cha uzima cha babu! Na kama ulikipata na ukakiamini kwa nini una wasi wasi na madaktari wakigoma au la? Kama wanakiburi na ni wauaji kwa nini rerikali iwaruhusu wananchi wake waende kwa wauaji? Je tushtaki serikali kwa kuwapeleka kwa wauaji?
Hivi huo mshahara wa laki tisa, ni take home au ni baada ya kukatwa kodi? Hivi wakina Ngeleja tulisikia walilipwa posho ya miliono nne kwa siku, hivi hawa hawawaonei huruma watanzania walala hoi? Hivi hawa hawajasomewhwa na kodi za watanzania??
Hivi BoT, TRA, bandarini, TANAPA sio za watanzania hizi? Mishahara yao mbona ipo tofauti? Kwani wao wana haki gani kulipwa zaidi ya mwalimu au polisi? Je mhudumu tu anaanza na mshahara wa tsh ngapi?
Acheni propaganda kwenye masuala ya muhimu... Kwa hiyo mnavyoona madaktari wamekaa kimya nyie mnashangilia kuwa mmeshinda?? ( sidhani kama ni wajinga kiasi hicho, kama hatujifunzi kwa walimu na ubora wa elimu, ngojea tuone kwa ukimya wa madaktari kwa wagonjwa, labda itatushtua maana inahusisha uhai!
Najisikitikia kuwa Mtanzania mnyonge maana sina mtetezi.
Ukweli ma-dr wameitia doa taaluma/weledi wao. Ma-dr wa tz wamegeuka kichekesho cha dunia.
Wamekosa busara na hekima za kawaida kabisa ambazo hata konda na wasukuma mikokoteni wanazo.
Wamekalia tamaa na ulafi wa pesa, hata kama watz wenzao watakufa.
Wanatukuza taaluma yao kana kwamba wao ni miungu watu. Hawajui kuwa mkulima asipolima na kuwauzia chakula hawataishi.
Mtumishi wa DAWASCO akigoma kuwapa maji wanajua hali itakavyokuwa. Fundi wa TANESCO akigoma kumpa umeme anajua matokeo yake. Hata mzoa taka pale hosp akigoma dr hawezi kufanya kazi.
Wamekosa uelewa mdogo ....kwamba tunategemeana sana kila mtu kwa fani yake. Kwa kifupi uwezo wao wa kufikiri ni kichekesho na wamegeuka vilaza wanaokimbizana na pesa.
SB na Ms Judith;
Unayoongea yana ukweli, lakini siyo practical. Hao wote wanafanya hayo si kwa faida ya madaktari, kila mtu ni kwa faida yake, we unadhani huyo mkulima asipouza mazao yeye atapata wapi mahitaji mengine? na atalimaje kama anaugua bila kupata matibabu? Unaleta mambo ya kufikirika ambayo hayawezekani. Unayajua kwa kina madai yote ya madaktari au unalijua hilo tu la kusimamishwa kazi mawaziri?
Inakuwaje wanakosa cha kusema na walishajiwekea masharti ya kuacha mgomo? Tatizo haliko kwa waziri wala naibu wake....it is the system in the ministry...kuwatoa na kuweka wengine will not solve the problem but can make it more worse than before....THINK BEFORE U ACT DO N'T BE LIKE NARROW MINDED GUYS.....this is just a comment and challenge 2 people...
Tumeona uwezo wako wa kufikiriwapendwa,
hawa madaktari ni watu wa ajabu sana na tena ni wenye dharau kupita kiasi, wauaji wakubwa! hivi wasingebahatika kusoma kabisa wangekuwa na uelewa wa kiwango gani?
sasa mbwembwe zole zooote hadi kuuua ndugu na wapendwa wetu bila hatia yoyote, dawa yao ilikuwa ni juice ya ikulu? kwani hawakujua kabisa kuwa hawana uwezo wala uhalali wa kupanga baraza la mawaziri? pinda laishawaambia ukweli, wakamdharau! hivi kama kitu kile kile pinda alichosema kikashindwa kuwaridhisha, kiliporudiwa na jk kimewaridhisha, sasa tuwaeleweje? mbona akili kidogo tu hata inayotosha kwenye kijiko cha chai ingetosha kujua kuwa kwa unyeti wa sekta ya afya, hawapaswi kugoma? hawa wenzetu wana akili yenye ukubwa gani?
mtu akisikia mgomo anadhani ni jambo la kihunihuni, kumbe mgomo ni suala la kisheria na limeainishwa kisheria sababu pamoja na taratibu zake. sasa watwambie mponda na nkya hawang'oki na hawapewa hata senti moja hadi hivi sasa, hicho walichoahidiwa na jk ndicho alichwaahidi pinda, kwa nini walimpuuza pinda na kuua watu wasio na hatia?
hebu angalieni, daktari anaanza na mshahara wa laki 9+, sekta nyingine mtu mwenye shahada anaanza na laki 4+! hivi hata hapo hawaoni kuwa serikali inawachukulia kwa uzito mkubwa zaidi ya kada nyingine? hayo majivuno yao na kujiona kada yao iko juu ya kada nyingine ndiyo ya kukemewa kwa nguvu zote. kila mtu anajua nchi ilipo kiuchumi, hiyo neema wanayolilia kila siku, wanategemea itatoka nchi gani? au kila mtanzania ageuzwe ng'ombe akamuliwe maziwa (kodi) na maziwa yote wanyweshwe madaktari pekee?
napenda serikali ichukue hatua kuimarisha sekta ya afya pamoja na sekta nyingine, lakini nimehuzunishwa sana na uelewa wa mambo wa madaktari wetu pamoja na viwango vya upendo na maadili ya kazi zao walionao.
kumradhi wote niliowaudhu kwa maoni haya,
mbarikiwe sana
Glory to God!
mis judith, nimekuambia miaka sita ya kumaliza na internship. Degree ya sociology ni three yrs, mph one yr na phd 3 years. Mpaka daktari anahangaikia mambo ya usajili miaka saba imeshakwisha. Ndo maana nikakwambia tafuta na nchi nyingine madaktari wanalipwaje na hao wengine wanalipwaje. Lawyer ni miaka mitano kwa ud na minne kwenye vyuo vingine pamoja na law school ambayo ilikuwa ni internship zamani.Ndo maana hizo profession wanafundishwa in international standards. Madaktari walijua kugoma ni kinyume na sheria ndo maana wakaamua kugoma ili kushinikiza mambo yao yasiyotatuliwa kwa miaka mingi yafanyiwe kazi. Hii ilikuwa ndo option ya mwisho. Unajua kwamba sheria ya kazi ya mwaka 2004 inataka kila mtu anayekuwa kazini kwa muda wa ziada anatakiwa alipwe 50 percent ya mshahara wake? Mbona haifanyiwi kazi na doctors wanalipwa elfu kumi for 24 hours? Hizo ofisi unazosema zinafungwa hospitali ni za wale co-workers wa sekta ya afya kama wahasibu, sekretaries na outpatient departments. Ofisi ya daktari na nesi haifungwi,ndo maana kuna watu wanaitwa on call workers. Hivi hao watu wa maji, umeme unaowazungumzi uliwahi waita kwako usiku kuja kurekebisha kitu wakaja? Ofisi zao umewahi kuhudumiwa usiku? Mpaka transfoma zilipuke ndo wanakata umeme wa eneo hilo ili kesho waje warekebishe.
yaani mis judith nahisi una matatizo au ni bifu la kukosa kusoma udaktari kama la blandina. Unalinganisha daktari na polisi? Wana vyeti gani hao mpaka wasimamie kwamba kulingana na elimu tuliyonayo tulipwe fedha kadhaa? Mimi nitaonaje umuhimu wa polisi wakati naibiwa kila siku, tunakabwa njiani na kubambikiwa kesi? Kazi yao ni ipi kwa profesion ipi waliyosomea? Ndo maana huko huko kuna makundi za wanaolipwa vizuri na kurubuniwa kuwakandamiza wale wasio na professions. Uliona msimamo wa madaktari kuanzia md mpaka professors? Unaweza kupata msimamo huo kwa polisi? We unataka kuniambia konda na daktari kazi yao sawa, kweli umedharau sana! Mtu mwenye gari lake ataonaje umuhimu wa konda? Ni utaratibu tu wa hii nchi kwa sababu ya wizi mlionao, nchi zingine gari hazina konda abiria mnajichangisha na kumkabidhi dereva nauli. Kwa wengine ni kama utaratibu wa kwenye kivuko, unalipa nauli kwanza ndo unaingia kwenye gari na wanaufuata.