Madakatari wakosa kauli juu ya Mponda/Nkya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madakatari wakosa kauli juu ya Mponda/Nkya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by OSOKONI, Mar 14, 2012.

 1. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,797
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  Madaktari wakosa kauli huhusu Dk. Mponda, Nkya  Rais wa MAT, Dk Namala Mkopi
  Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), kimesema hawana la kusema baada ya Rais Jakaya Kikwete kuweka wazi msimamo wake kwamba hata kama akiwafukuza kazi Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hadji Mponda na Naibu wake, Dk. Lucy Nkya hakuwezi kumaliza matatizo yao.

  Rais Kikwete aliweka wazi msimamo wake juzi alipolihutubia Taifa kupitia kwa wazee wa mkoa wa Dar es Salaam na kuongeza kuwa matatizo ya madaktari hayawezi kulizwa kwa viongozi hao kufutwa kazi, badala yake kinachotakiwa ni kuweka mfumo mzuri ndani ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ili kina mtu atakayekuwa anaiongoza aweze kuufuata.

  Rais wa MAT, Dk Namala Mkopi, alisema hawana cha kusema kufuatia kauli ya Rais na kuongeza kuwa madai yao yanashughulikiwa na Rais Kikwete kama wallivyokubaliana wiki iliyopita.

  “Kwa hilo sina comment (maoni) ila msimamo wetu ni ule ule kwa kuwa tayari tulishazungumza na Rais na tukatoa tamko katika mkutano wetu hivyo kwa sasa siwezi kutengeneza opinion (maoni) kwani tulishaafikiana,” alisema.

  Dk. Mkopi alisema wao tayari walishaongea na Rais Kikwete, hivyo kwa sasa hawana maoni kwa kuwa juzi Rais alikuwa anazungumza na wazee na sio madaktari. Alisema pia kuwa hawakumsikia Rais Kikwete akizungumzia chochote kwamba Dk. Mponda na Nkya hawataondolewa.

  Wakati huo huo, wanaharakati wamesema kuwa harakati walizokuwa wakizifanya zilikuwa zinalenga kuishinikiza serikali kutatua mgomo wa madaktari ili wananchi wasiendelee kufa na sio vinginevyo na si kuchochea mgomo.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Hellen Kijo Bisimba, alisema kauli zilikuwa hazilengi kushinikiza kuwepo kwa mgomo wa madaktari na kwamba nia yao ilikuwa ni kumaliza mgogoro ili wananchi wasikose huduma pindi wanapofikishwa hospitalini.

  Kuhusu kauli ya Rais Kikwete ya kuwashangaa kwa kushindwa kukemea mgomo huo, Dk. Bisimba alisema walichukua hatua zikiwemo za kukutana na madaktari kwa ajili ya kusikiliza madai yao ya msingi kwa serikali.

  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #2
  Mar 14, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  wapendwa,

  hawa madaktari ni watu wa ajabu sana na tena ni wenye dharau kupita kiasi, wauaji wakubwa! hivi wasingebahatika kusoma kabisa wangekuwa na uelewa wa kiwango gani?

  sasa mbwembwe zole zooote hadi kuuua ndugu na wapendwa wetu bila hatia yoyote, dawa yao ilikuwa ni juice ya ikulu? kwani hawakujua kabisa kuwa hawana uwezo wala uhalali wa kupanga baraza la mawaziri? pinda laishawaambia ukweli, wakamdharau! hivi kama kitu kile kile pinda alichosema kikashindwa kuwaridhisha, kiliporudiwa na jk kimewaridhisha, sasa tuwaeleweje? mbona akili kidogo tu hata inayotosha kwenye kijiko cha chai ingetosha kujua kuwa kwa unyeti wa sekta ya afya, hawapaswi kugoma? hawa wenzetu wana akili yenye ukubwa gani?

  mtu akisikia mgomo anadhani ni jambo la kihunihuni, kumbe mgomo ni suala la kisheria na limeainishwa kisheria sababu pamoja na taratibu zake. sasa watwambie mponda na nkya hawang'oki na hawapewa hata senti moja hadi hivi sasa, hicho walichoahidiwa na jk ndicho alichwaahidi pinda, kwa nini walimpuuza pinda na kuua watu wasio na hatia?

  hebu angalieni, daktari anaanza na mshahara wa laki 9+, sekta nyingine mtu mwenye shahada anaanza na laki 4+! hivi hata hapo hawaoni kuwa serikali inawachukulia kwa uzito mkubwa zaidi ya kada nyingine? hayo majivuno yao na kujiona kada yao iko juu ya kada nyingine ndiyo ya kukemewa kwa nguvu zote. kila mtu anajua nchi ilipo kiuchumi, hiyo neema wanayolilia kila siku, wanategemea itatoka nchi gani? au kila mtanzania ageuzwe ng'ombe akamuliwe maziwa (kodi) na maziwa yote wanyweshwe madaktari pekee?

  napenda serikali ichukue hatua kuimarisha sekta ya afya pamoja na sekta nyingine, lakini nimehuzunishwa sana na uelewa wa mambo wa madaktari wetu pamoja na viwango vya upendo na maadili ya kazi zao walionao.

  kumradhi wote niliowaudhu kwa maoni haya,

  mbarikiwe sana

  Glory to God!
   
 3. kakakuona40

  kakakuona40 JF-Expert Member

  #3
  Mar 14, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 300
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Watanzania wanapeenda mifarakano
   
 4. MANI

  MANI Platinum Member

  #4
  Mar 14, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  Ms Judith tulipuuza malalamiko ya walimu matokeo yake ni kuwa wanaopasi sasa hivi 10% ya watihaniwa. Sasa kama na madaktari nao tutawapuuza sijui maisha yetu tutayaweka wapi penye usalama. Maana ni heri mgomo baridi wa walimu kuliko wa madaktari maana hatari kutibiwa na mtu asiye na mood au kujituma kwa dhati.
   
 5. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #5
  Mar 14, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Tumekusamehe!
   
 6. S

  Silent Burner Member

  #6
  Mar 14, 2012
  Joined: Feb 25, 2012
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukweli ma-dr wameitia doa taaluma/weledi wao. Ma-dr wa tz wamegeuka kichekesho cha dunia.

  Wamekosa busara na hekima za kawaida kabisa ambazo hata konda na wasukuma mikokoteni wanazo.

  Wamekalia tamaa na ulafi wa pesa, hata kama watz wenzao watakufa.

  Wanatukuza taaluma yao kana kwamba wao ni miungu watu. Hawajui kuwa mkulima asipolima na kuwauzia chakula hawataishi.

  Mtumishi wa DAWASCO akigoma kuwapa maji wanajua hali itakavyokuwa. Fundi wa TANESCO akigoma kumpa umeme anajua matokeo yake. Hata mzoa taka pale hosp akigoma dr hawezi kufanya kazi.

  Wamekosa uelewa mdogo ....kwamba tunategemeana sana kila mtu kwa fani yake. Kwa kifupi uwezo wao wa kufikiri ni kichekesho na wamegeuka vilaza wanaokimbizana na pesa.
   
 7. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #7
  Mar 14, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  MS JUDITH, unazijua symptoms of profound mental retardation?
   
 8. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #8
  Mar 14, 2012
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Kwani lazima ukatibiwe na madaktari hawa, si nenda hata loliondo kama waona hawa ni wauaji?
   
 9. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #9
  Mar 14, 2012
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Hata mwili si viungo vyote vinategemeana. Vingine vinaweza kuishi bila kutegemea mwenzake, ila vingine haviwezi kuishi pasipo kutegemea mwenzake; ndio kama madaktari!!!

   
 10. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #10
  Mar 14, 2012
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,499
  Likes Received: 2,743
  Trophy Points: 280
  Wamechemsha hivyo wakubali yaishe.................. Na wajue kuwa hawatapata tena nafasi kama hii ndani ya serikali ya CCM ikiwa wataendelea kuwepo madarakani kwa kutuibia kura kama kawaida yao.
   
 11. J

  Julias Member

  #11
  Mar 14, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Inakuwaje wanakosa cha kusema na walishajiwekea masharti ya kuacha mgomo? Tatizo haliko kwa waziri wala naibu wake....it is the system in the ministry...kuwatoa na kuweka wengine will not solve the problem but can make it more worse than before....THINK BEFORE U ACT DO N'T BE LIKE NARROW MINDED GUYS.....this is just a comment and challenge 2 people...
   
 12. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #12
  Mar 14, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  mpendwa,

  mbona mood yao iko chini toka zamani? hujasikia visa vya kupasua kichwa badala ya miguu? hujasikia wajawazito wakijifungulia reception kwa kukosa "kitu kidogo"? hujakutana na dk akakuandikia dawa wakati bado ukiendelea kumwelezea ugonjwa wako? hujui kuwa usugu wa magonjwa mengi tulionao unatokana na madaktari kutoa tiba isiyo sahihi na huku wakijua kuwa siyo sahihi? kuna erafiki yangu ali vimba goti baada ya kuanguka wakataka kumpasua akakataa, familia yake ilipotoa "kitu kidogo" wakamwambia hana tatizo la kupasuliwa, akande tu goti kwa barafu na akafanya hivyo na kupona baada ya wiki mbili tu!

  mpendwa hawa madaktari ni wauaji wakubwa, wamesababishia wapendwa wetu ulemavu na vifo mara nyingi sana kwa kupenda virushwa vidogovidogo, na nawaambia hata wakipewa mishahara ya milioni 17 wanayolilia wataendelea tu na tabia zao. alaye nyama ya mtu, hali mara moja mpendwa!

  ubarikiwe sana


  mpendwa,

  asante kwa kutoa mifano mizuri na ya moja kwa moja na inayoeleweka vizuri sana. kwa kuongeza tu;

  hivi hata wakipewa hayo mamilioni wakati watanzania wenzao ni mafukara watayafurahia maisha huku vibaka na majambazi wanawachekea kwa kuwa ni madaktari na wanavaa makoti meupe kazini?

  tuwaulize hao madaktari, nyumba zao zikiungua moto na kikosi cha zimamoto kimegoma watafanya nini? wakienda msalani wakakuta mpiga deki wao kagoma watajisaidia kwenye mifuko ya makoti yao meupe? hawa wenzetu itabidi wajihoji kisawasawa na wabadilike, vinginevyo wanyamaze wangoje hukumu ya Mungu!

  kwa kweli hata ungesoma kiasi gani, kama hukuelimika ni BURE!

  mbarikiwe sana wapendwa

  Glory to God!
   
 13. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #13
  Mar 14, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  mpendwa,

  tutakwenda kutibiwa na hao hao hukohuko mahospitalini. kutibu ni kazi yao na ni wajibu wao, na wanapata mishahara. na kama wanapokea mishahara wataifanya, huo ndio ukweli, wasitubabaishe!

  nazungumza habari ya division of labor and specialization hapa!

  ubarikiwe sana

  Glory to God!
   
 14. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #14
  Mar 14, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Kwani JK ana hekima na busara?
   
 15. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #15
  Mar 14, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 19,279
  Likes Received: 10,463
  Trophy Points: 280
  mgomo wa madaktari utabakia kuwa mgomo bora kuwahi kutokea tanzania.busara waliyoonyesha madaktari ni kubwa kama ilivyotegemewa kutoka kwao.

  Bint yangu ms judith naona wewe ni mchochezi usiyeamini kwenye maridhiano.

  KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
   
 16. d

  dav22 JF-Expert Member

  #16
  Mar 14, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 1,902
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  hatuwaelewi madaktari aisee
   
 17. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #17
  Mar 14, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,530
  Likes Received: 10,442
  Trophy Points: 280
  mgomo bora?....kwa hiyo wanastahili sifa kwa kusababisha vifo.!!!
   
 18. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #18
  Mar 14, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Ms Judith, salaam sana,karibu tena jamvini ulipotea muda hivi.

  Huo mshahara wa laki 9(900,000) kwa mwezi (siku 30) ni sawa na posho iliopendekezwa ya mbunge akikaa katika kiti chake kwa siku 4.5.( jumatatu-alhamisi na ijumaa hadi saa 6 mchana) Ni posho nasisitiza. Sijui hawa ni muhimu sana kuliko kada zingine!!

  Spika Makinda alisema wabunge wa Kenya wanawacheka wa Tanzania, na nina hakika madaktari wa Kenya wanawacheka wa Tanzania. Sasa hapo kuna ubaya gani wakiomba waongezewe kama wabunge walivyoomba?

  Kada nyingine kama walimu nao wanadai, umesahau Tucta ya mgaya ilikuwa inalalimikia nini. Kama Polisi na mabwana shamba kwa mfano, wameridhika na wanachopata kwanini wawazuie wengine wasidai haki zao?

  Kuhusu Nkya na Mponda wao wamesema waendelee kuwepo kama ni busara lakini hawatawapa ushirikiano. Mdau wa sekta ya afya ni nani zaidi ya wataalamu waliomo. Mponda ni mpita njia tu kesho anaweza kuwa ujenzi n.k. Kama uwepo wake utakwaza watu kwanini wasifikirie wao kwanza halafu rais naye apime. Neno kutotoa ushirikiano ni pana na linagusa sehemu kubwa sana.

  Ahsante
   
 19. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #19
  Mar 14, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,182
  Trophy Points: 280
  Hapa naona matatu.

  1. Rais ana save face kwa kuogopa ku cave in. Anaona akikubali matakwa ya madaktari ataonekana weak na pengine sekta nyingine zitaiga madaktari.

  2. Kwa kusema kumuondoa Waziri hakutatatua matatizo ya madaktari, rais anajionyesha kwamba approach yake ya uongozi ni ya zimamoto. Yaani yeye anataka kuangalia anachoweza kufanya sasa kutatua mgogoro huu, bila kuangalia kwamba Waziri wake kakosea au hajakosea, ni mzembe au si mzembe, anaweza kusababisha madhara mengine au hawezi. Pia anakataa kumuondoa waziri kwa sababu serikali ya CCM haiendeshwi kwa merit, na hata yeye mwenyewe hakuchaguliwa kuwa rais kwa merit. Kulindana na kujilinda kunaendelea kuchukua umuhimu kuliko maswala ya msingi.

  3. Madaktari wamekamatwa pabaya. Walikuwa na chaguo la kum defy rais na amri ya mahakama na kuweza kukosa public support kwa kuonekana washari au kukubali ushindi wa "Maji Maji". Unshindwa na mkoloni Mjerumani lakini kesho anajiuliza mara mbili kabla ya kukunyanyasa. Wakaamua kuchukua ushindi wa "Maji Maji".
   
 20. m

  mtume pauli Member

  #20
  Mar 14, 2012
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kama madaktari ni wauwaji ukiugua baki hapo nyumbani kwako. tuone kama wakati unakata roho hutaita daktari kwa sauti kuu.

  na kwa kauli yako hii wewe ukiugua ni kifo tu, kisaikologia huwezi kupona kamahuna imani na daktari anaye kutibu. pole you are a deadly walking body.
   
Loading...