Madai ya watumishi serikalini

Lutandagula

JF-Expert Member
Apr 8, 2018
1,762
2,157
Mimi ni mwajiriwa serikalini tokea mwaka 2011, nimepanda madaraja kwa mujibu wa taratibu na kununi za utumishi mara 2, mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2015 na mara ya pili ilikuwa mwaka 2019.

Katika kupanda kwangu kulikuwa na ucheleweshwaji wa ubadilishaji wa mishahara mipya na hivyo serikali kulimbikiza madeni,kwa maana hiyo serikali naidai malimbikizo mawili ya mwaka 2015 na 2019, lakini kwa miaka yote hii mpaka sasa sijalipwa mapunjo yangu ya mshahara,na inawezekana watu wa aina kama yangu tupo wengi.

Je, ni kweli serikali haina pesa ya kulipa mapunjo ya mshahara kwa watumishi wanaodai? Ikizingatiwa imekuwa miaka mingi sana pasipo kulipa haya madeni?

Je, huu ni mwendelezo wa Serikali kudharau madai ya watumishi hasa wa kada za chini?

Je, Serikali ina mpango gani na haya madeni ya watumishi?, Ingekuwa ndo Ummy Mwalimu,madai yake yangechukua muda mrefu kiasi hiki?

Ombi langu kwa Serikali tulipeni malimbikizo yetu ya madeni,msituonee sisi watumishi,tunafanya kazi ngumu sana katika hili Taifa lakini cha ajabu wala hamtujali na madai yetu hamuyachukulii umuhimu wowote.

Nakuomba Ummy Mwalimu huu ujumbe ukufikie,naomba mlipe madeni ya watumishi wa umma,msilete visingizio vya uchuguzi,ni uchuguzi gani usioisha, uchuguzi gani wa miaka yote hiyo?

Naomba kuwasilisha.
 
Haki ya mtumishi ni mshahara tu. Mambo mengine inabaki kuwa utashi wa wanasiasa.
 
Haki ya mtumishi ni mshahara tu. Mambo mengine inabaki kuwa utashi wa wanasiasa.
Kama ndo hivyo watangaze kuwa madeni yote wanayodaiwa wameyafuta,lakini pia hayo madeni yametokana na mishahara kunilipa isiyo sahihi baada ya kupata barua ya promotion!
 
Back
Top Bottom