Madai ya ndevu za uamsho gerezani yapata mshiko


Informer

Informer

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2006
Messages
1,359
Points
2,000
Informer

Informer

JF-Expert Member
Joined Jul 29, 2006
1,359 2,000
Na Mohammed Mhina|Jeshi la Polisi Zanzibar

Tuhuma za uamsho kunyolewa ndevu wakiwa gerezani, mahakama kuuyawashauriwa wafungue kesi madai


ZANZIBAR JUMANNE NOVEMBA 20, 2012. Mahakama Kuu ya Vuga mjini Zanzibar imetoa ushauri kwa Viongozi wa Jumuiya mbili za Kiislam Zanzibar wanaotuhumiwa kwa makosa ya kuhatarisha usalama wa Taifa ya kutotendewa haki wakiwa Gerezani wafungue kesi ya madai.Ushauri huo umetolewa na Mrajisi wa Mahakama Kuu ya Zanzibar Mh. George Kazi mara baada ya kupitia kwa makini maombi ya watuhumiwa hao yaliyofikishwa mbele yake Novemba 8, mwaka huu kupitia kwa mawakili wa watuhumiwa hao.

Kesi hiyo inawakabili watu wanane akiwemo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar Sheikhe Faridi Hadi Ahmedi na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uamsho Sheikhe Mselem Ali Mselem.Wengine katika kesi hiyo ni Mussa Juma Issa, Suleiman Juma Suleiman, Azan Khalid Hamdan, Khamis Ali Suleiman, Hassan Bakar Suleiman na Ghalib Ahmada Omar.Akitoa uwamuzi huo, Mh. Kazi amesema watuhumiwa wana haki ya kufungua kesi mahakama kuu ya kile wanachokilalamikia na kwamba mahakama kuu itakuwa na uwamuzi wa kuyasikiliza madai yao tofauti na kesi ya msingi kwa watuhumiwa.

Kwa kupitia kwa Mawakili wao, watuhumiwa hao walidai kuwa wananyimwa uhuru na haki zao za msiki ikiwa ni pamoja na kupigwa marufuku yfugaji wa ngevu wakiwa rumande chuo cha Mafunzo (magereza).
Watuhumiwa hao wanakabiliwa na makosa mashta manne yakiwemo ya kutoa lugha za uchochezi, kufanya vurugu na kusababisha uharibifu wa miundombinu ya barabara mjini Zanzibar.

Wakizungumzia kesi ya msingi kwa watuhumiwa hao, Waendesha Mashtaka wa Serikali walidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamili na kwamba wanaomba siku nyingine ya kutajwa.Mrajisi huyo wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, ameiahirisha kesi hiyo hadi Alhamisi Novemba 29, mwaka huu itakapotajwa tena.

Kama kawaida, Jeshi la Polisi lilifunga barabara zote za kuingia na kutoka mahakamani na kuimarisha ulinzi ndani na nje ya mahakama hiyo ambapo kila pembe walionekana Makachero wa Polisi na Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia.

Nao baadhi ya wananchi waliofika makahakamani hapo waliwataka waandishi wa habari kuandika ukweli kuhusiana na kesi hiyo ili kuinusuru nchi yetu kukumbwa na machafuko.Watuhumiwa hao wanatetewa na Mawakili wa kujitegemea Bw. Salum Toufik na Bw. Abdallah Juma Kaka huku kwa upande wa Serikali ikiwakilishwa na Bw. Ramadhani Nassibu na wenzake wawili kama Waendesha Mashtaka.
 
Ndahani

Ndahani

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2008
Messages
14,954
Points
2,000
Ndahani

Ndahani

JF-Expert Member
Joined Jun 3, 2008
14,954 2,000
Wafungue kesi ya madai wakitokea mahabusu?
 
Mwana Mtoka Pabaya

Mwana Mtoka Pabaya

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2012
Messages
13,719
Points
2,000
Mwana Mtoka Pabaya

Mwana Mtoka Pabaya

JF-Expert Member
Joined Apr 22, 2012
13,719 2,000
Unajua hawa kina yakhe wanakosea, huyu ilfaa aletwe huku bara akafungwe kwenye magereza ya mikoani akakutane na manunda wamgombee.
 
nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Messages
15,871
Points
1,225
nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined Aug 2, 2010
15,871 1,225

TUHUMA ZA UAMSHO KUNYOLEWA NDEVU WAKIWA GEREZANI, MAHAKAMA KUU YAWASHAURIWA WAFUNGUE KESI MADAINa Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Zanzibar

Mahakama Kuu ya Vuga mjini Zanzibar imetoa ushauri kwa Viongozi wa Jumuiya mbili za Kiislam Zanzibar wanaotuhumiwa kwa makosa ya kuhatarisha usalama wa Taifa ya kutotendewa haki wakiwa Gerezani wafungue kesi ya madai.


Ushauri huo umetolewa na Mrajisi wa Mahakama Kuu ya Zanzibar Mh. George Kazi mara baada ya kupitia kwa makini maombi ya watuhumiwa hao yaliyofikishwa mbele yake Novemba 8, mwaka huu kupitia kwa mawakili wa watuhumiwa hao.


Kesi hiyo inawakabili watu wanane akiwemo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar Sheikhe Faridi Hadi Ahmedi na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uamsho Sheikhe Mselem Ali Mselem.


Wengine katika kesi hiyo ni Mussa Juma Issa, Suleiman Juma Suleiman, Azan Khalid Hamdan, Khamis Ali Suleiman, Hassan Bakar Suleiman na Ghalib Ahmada Omar.


Akitoa uwamuzi huo, Mh. Kazi amesema watuhumiwa wana haki ya kufungua kesi mahakama kuu ya kile wanachokilalamikia na kwamba mahakama kuu itakuwa na uwamuzi wa kuyasikiliza madai yao tofauti na kesi ya msingi kwa watuhumiwa.


Kwa kupitia kwa Mawakili wao, watuhumiwa hao walidai kuwa wananyimwa uhuru na haki zao za msiki ikiwa ni pamoja na kupigwa marufuku yfugaji wa ngevu wakiwa rumande chuo cha Mafunzo (magereza).


Watuhumiwa hao wanakabiliwa na makosa mashta manne yakiwemo ya kutoa lugha za uchochezi, kufanya vurugu na kusababisha uharibifu wa miundombinu ya barabara mjini Zanzibar.


Wakizungumzia kesi ya msingi kwa watuhumiwa hao, Waendesha Mashtaka wa Serikali walidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamili na kwamba wanaomba siku nyingine ya kutajwa.


Mrajisi huyo wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, ameiahirisha kesi hiyo hadi Alhamisi Novemba 29, mwaka huu itakapotajwa tena.


Kama kawaida, Jeshi la Polisi lilifunga barabara zote za kuingia na kutoka mahakamani na kuimarisha ulinzi ndani na nje ya mahakama hiyo ambapo kila pembe walionekana Makachero wa Polisi na Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia.Nao baadhi ya wananchi waliofika makahakamani hapo waliwataka waandishi wa habari kuandika ukweli kuhusiana na kesi hiyo ili kuinusuru nchi yetu kukumbwa na machafuko.


Watuhumiwa hao wanatetewa na Mawakili wa kujitegemea Bw. Salum Toufik na Bw. Abdallah Juma Kaka huku kwa upande wa Serikali ikiwakilishwa na Bw. Ramadhani Nassibu na wenzake wawili kama Waendesha Mashtaka.
 
nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Messages
15,871
Points
1,225
nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined Aug 2, 2010
15,871 1,225
Kisheria inatakiwa lakini ni nani atawahakikishia? Itabidi wailete QRAN - Mahakamani??

Mahakama kuu hii zio MATUMIZI ya PESA BILA SABABU???

SOMA MANENO ya HEKIMA

It is not permissible for the Muslim to remove any hair from the beard except what the Lawgiver has allowed. It is reported from one of the companions who narrated the hadeeth, "Leave the beard and trim the mustaches," 'Abdullaah bin 'Umar, that he used to remove from his beard what was below a fistful.

Apart from that, trimming the beard is against the Sunnah, whether or not the man's beard is pleasing to him, and whether or not it is pleasing to others, for all of Allaah's creation is handsome, as in the saheeh hadeeth, where the Prophet (saw) saw a man with a long waist-shirt and ordered him to have his izaar halfway up his shins; the man gave the excuse that he had a defect in his ankles, so the Prophet (saw) said, "All of Allaah's creation is handsome."

(saheeh-Ahmad and others. This phrase is actually of Qur'anic origin cf. Sajdah 32:7)
 
kelao

kelao

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2012
Messages
5,932
Points
2,000
Age
40
kelao

kelao

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2012
5,932 2,000
Shekhe faridi amesikika leo akiendelea kuwahimiza wafuasi wake kuendelea kuupinga muungano kwa nguvu zote! Najiuliza huyu mtu yupo chini ya mikono ya sheria lkn bado ana kiburi kiasi hiki,nguvu anaipata wapi?
 
LordJustice1

LordJustice1

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2011
Messages
2,264
Points
0
LordJustice1

LordJustice1

JF-Expert Member
Joined Jan 19, 2011
2,264 0
Kwa hiyo wanataka kufungua "kesi ya ndevu?"
 
Mabreka

Mabreka

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2012
Messages
709
Points
0
Mabreka

Mabreka

JF-Expert Member
Joined Aug 29, 2012
709 0
huyo fareed anaonekana gaidi kabisa,
huwezi kuwa chini ya ulinzi alafu anawaambia watu wauvunje muungano
 
L

luhombi

Member
Joined
Oct 17, 2012
Messages
85
Points
0
Age
30
L

luhombi

Member
Joined Oct 17, 2012
85 0
hata mandela aliitwa gaidi wakati ule anapigania haki kule south africa, kumbuka ni juzi juzi tu ndio marekani wamemtoa mzee mandela kwenye list yao ya magaidi. acha wapiganie nchi yao bwana
huyo fareed anaonekana gaidi kabisa,
huwezi kuwa chini ya ulinzi alafu anawaambia watu wauvunje muungano
 
K

Kadogoo

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2007
Messages
2,072
Points
1,195
K

Kadogoo

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2007
2,072 1,195
huyo fareed anaonekana gaidi kabisa,
huwezi kuwa chini ya ulinzi alafu anawaambia watu wauvunje muungano
Nani kakuambia kuvunja muungano ni ugaidi? Soviet union, Ethiopi na Eritrea, Yemeni nk zote zilivunjilia mbali Muungano sasa huo ulikuwa ni ugaidi?

We watoka wapi nchi gani weye?
 
Duduwasha

Duduwasha

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2010
Messages
5,377
Points
2,000
Duduwasha

Duduwasha

JF-Expert Member
Joined Nov 3, 2010
5,377 2,000
Mshasikia Waarabu wameanzisha Umoja wao.... mawechoka na wausi ila cha kushangaza niliwatizama kuna black arab pia lol wasomali naona na wao watajiingiza kwenye huo umoja.... nii hali ya hatari inayotujia mbeleni kwetu Watanzania asili.. hawa wageni wanaweza kuwa kama wafanyavyo kule iran wanachagua wao raisi... ndio muiran kesha sambaza mbegu kuhakikisha Taifa lia tanganyika nalo linakuwa la kiislam kama zenji
 
Mwana Mtoka Pabaya

Mwana Mtoka Pabaya

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2012
Messages
13,719
Points
2,000
Mwana Mtoka Pabaya

Mwana Mtoka Pabaya

JF-Expert Member
Joined Apr 22, 2012
13,719 2,000
Nani kakuambia kuvunja muungano ni ugaidi? Soviet union, Ethiopi na Eritrea, Yemeni nk zote zilivunjilia mbali Muungano sasa huo ulikuwa ni ugaidi?

We watoka wapi nchi gani weye?
Wamevunja wenye nchi zao na sio magaidi toka Oman.
 
Thanda

Thanda

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2012
Messages
1,915
Points
0
Thanda

Thanda

JF-Expert Member
Joined Apr 6, 2012
1,915 0
Hapa hatufuati sheria za kiislamu,,,,tunafuata sheria za JMT...mtu akiona hawezi aondoke arudi kuanzisha serikali yake mwenyewe.
Kisheria inatakiwa lakini ni nani atawahakikishia? Itabidi wailete QRAN - Mahakamani??

Mahakama kuu hii zio MATUMIZI ya PESA BILA SABABU???

SOMA MANENO ya HEKIMA

It is not permissible for the Muslim to remove any hair from the beard except what the Lawgiver has allowed. It is reported from one of the companions who narrated the hadeeth, "Leave the beard and trim the mustaches," 'Abdullaah bin 'Umar, that he used to remove from his beard what was below a fistful.

Apart from that, trimming the beard is against the Sunnah, whether or not the man's beard is pleasing to him, and whether or not it is pleasing to others, for all of Allaah's creation is handsome, as in the saheeh hadeeth, where the Prophet (saw) saw a man with a long waist-shirt and ordered him to have his izaar halfway up his shins; the man gave the excuse that he had a defect in his ankles, so the Prophet (saw) said, "All of Allaah's creation is handsome."

(saheeh-Ahmad and others. This phrase is actually of Qur'anic origin cf. Sajdah 32:7)
 
Power G

Power G

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2011
Messages
3,912
Points
1,225
Power G

Power G

JF-Expert Member
Joined Apr 20, 2011
3,912 1,225
VIONGOZI wa Jumuiya ya Uamsho, Sheikhe Faridi Hadi Ahmed na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Sheikh Mselem Ali Mselem, wamewasilisha maombi Mahakama Kuu ya Vuga Zanzibar, kutaka kufungua kesi kupinga kunyolewa ndevu wakiwa mahabusu.

Kutokana na ombi hilo, Mahakama Kuu ya Vuga mjini hapa, imekubali ombi hilo na kutoa uamuzi wa kuwaruhusu viongozi hao, wafungue kesi ya madai, kupinga kunyolewa ndevu zao na kutotendewa haki wakiwa mahabusu. Sheikh Farid na wenzake, wanashtakiwa kwa makosa ya kuhatarisha usalama wa taifa.

Uamuzi wa kuwaruhusu viongozi hao wafungue kesi ya madai, umetolewa na Mrajisi wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, George Kazi, baada ya kupitia kwa makini maombi ya watuhumiwa hao. Washtakiwa hao waliwasilisha maombi hayo Novemba 8, mwaka huu, kupitia kwa mawakili wao, wakipinga kitendo cha polisi kuwanyoa ndevu na kutowatendea haki wakiwa mahabusu.

Maombi hayo yaliwasilishwa na washtakiwa wanane, akiwemo Sheikh Farid na Mwenyekiti wa Uamsho, Sheikh Mselem. Wengine katika kesi hiyo ni Mussa Juma Issa, Suleiman Juma Suleiman, Azan Khalid Hamdan, Khamis Ali Suleiman, Hassan Bakar Suleiman na Ghalib Ahmada Omar.

Akitoa uamuzi wa kufungua kesi ya kupinga kunyolewa ndevu, Jaji Kazi alisema watuhumiwa wana haki ya kufungua kesi mahakama kuu juu ya kile wanachokilalamikia na kwamba Mahakama kuu itakuwa na uamuzi wa kuyasikiliza madai yao tofauti na kesi ya msingi ya uchochezi na kuhatarisha amani.

Kupitia kwa mawakili wao, watuhumiwa hao walidai kuwa wananyimwa uhuru na haki zao za msingi ikiwa ni pamoja na kupigwa marufuku kufuga ndevu wakiwa rumande ya Chuo cha Mafunzo (Magereza).

Source: Mzalendonet
 
Power G

Power G

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2011
Messages
3,912
Points
1,225
Power G

Power G

JF-Expert Member
Joined Apr 20, 2011
3,912 1,225
Mambo hayo na maajabu ya dunia, wenzetu wanadai ndevu!!
 
Baba V

Baba V

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2010
Messages
19,495
Points
1,250
Baba V

Baba V

JF-Expert Member
Joined Dec 29, 2010
19,495 1,250
Zilikuwa za dhahabu nini!? kweli maajabu hayataisha dunia hii
 
Malaria Sugu

Malaria Sugu

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2009
Messages
2,653
Points
0
Malaria Sugu

Malaria Sugu

JF-Expert Member
Joined Jul 7, 2009
2,653 0
serekali ya CCM bana. yaani hata masheikh wanataka wawe kama mapadri hawana ndevu?
 

Forum statistics

Threads 1,286,232
Members 494,902
Posts 30,887,828
Top