Madai ya mgomo Chuo kikuu Dar hayana upeo mkubwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madai ya mgomo Chuo kikuu Dar hayana upeo mkubwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Feb 5, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Feb 5, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kiwango cha posho ya Tsh 5000 kwa siku kwa mwanachuo kwa mazingira ya sasa kwa Tanzania, ni kiwango kinachoweza msaidia kama anaakili ya kupanga vizuri bajeti yake. Kama wanachuo wanataka kuishi kwenye hoteli za gharama au kifahari ni jukumu lao na wazazi wao kuongeza pesa za kujikimu kifahari. Kiwango cha Sh laki moja na nusu kwa mwezi kama yuko makini na kufikiria zaidi future yake anaweza panga vizuri bajeti na akaishi bila tatizo kubwa. Ila kama anataka awe anakwenda kula Hamburgers McDonalds ni juu yake na familia yako kuongeza matumizi.

  Tumepitia vyuo vya Tanzania na tumepitia vyuo vya mataifa makubwa, kwa ulinganifu katika masuala ya posho naweza sema kumbe Tanzania ni bora mwanafunzi anaweza pata posho hiyo kuliko vyuo vya nchi tajiri. Watu hatukulala usingizi ni darasa na kazi. Uwapo kazini wakati wa mapumziko ndo unafanya homework, hakuna kulaza damu.

  Tusiwe watu wa kulaumu serikali katika kila kitu, tulaumu yale ya msingi lakini katika hili mimi binafsi nasema hapana.

  Watanzania tuko wavivu mno wa kujituma na kufikiri. Mazingira yako huru mno kujishughulisha Tanzania kuliko mataifa yaliyoendelea.

  Utakuta walimu wanakimbilia kufundisha shule za mijini, kumbe shule za vijijini zina nafasi zaidi kwa kujiongezea pato kwa kujishughulisha na kilimo au kufungua biashara ndogo ndogo kusaidia wanavijiji kupata bidhaa ambazo wanapata taabu kuzifuata mbali. Mshahara wake ungezalisha zaidi kuliko mijini anamalizia kwenye starehe na gharama kubwa ya maisha.

  Athari wanazopata wanachuo katika migomo yao ni kubwa kwao wanafunzi kuliko viongozi wanaowanyooshea vidole wakati wanaishi maisha ya starehe, na waendapo vyuoni ni kwenda kuwapiga msasa wa kisiasa tu. Kinachofanyika sasa vyuoni ni kama cheer ambayo ni kufuata mkumbo tu na kulazimisha wasiotaka lazima wafanye vinginevyo watadhurika, huku ni kuwanyima wengine uhuru wao wa kujiamulia wanavyotaka. Haki ya uhuru ni uamuzi wa dhamira safi baada ya upembuzi yakinifu.

  Serikali ina mengi ya kufanya si wanafunzi tu, elimu, mawasiliano, afya, na huduma nyingine za jamii. Hata Chama kingine kikitawala hakitamaliza matatizo hayo kwa siku moja.
   
 2. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #2
  Feb 5, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Siasa za ujamaa zimetuharibu..kila kitu tunasubiri serikali, serikali, serikali.. kwa wanginewe tulioshuhudia nchi zengine mtu anajisomesha yeye mwenyewe..mchana anapiga mzigo, usiku anaenda kupiga kitabu..sisi tunataka kila kitu kiekwe mezani TULE.
   
 3. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #3
  Feb 5, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Inshu siyo kuwekewa mezani kila kitu!! ni mfumo wenyewe ulivyowekwa. vipindi vinapigwa hadi saa 2 usiku utapata muda wa kufanya ndugu yangu? Hata hayo mashule ya kata yangekuwa yanawatumia hawa jamaa yasingekuwa yanapata zero hata moja, lakini kwa vile hakuna " The called Coordination ya Elimu kuanzia chini hadi vyuo vikuu au vya elimu basi ni bora liende". Kila mtu anataka anavyoona, nchi haina mipango ya maana kiutekelezaji katika nyanja yeyote zaidi ya mipango kwenye karatasi.

  My take:
  1) Hawa jamaa wawwape muda wa wao hata kutafuta kazi mitaani japo kufundisha kwa masaa mawili mashule ya kata inapunguza matatizo kibao. Nchi inatatizo na walimu wakati ni kiasi cha kutwist some parameters na kujikuta wanasolve mengi.
  2) Kama ni kumwagilia bustani za barabarani, wanalipwa nako poa ni sera tu. Wanaweza kukataa mara ya kwanza baadae watakubali.
   
 4. Swahilian

  Swahilian JF-Expert Member

  #4
  Feb 5, 2011
  Joined: Apr 28, 2009
  Messages: 585
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Usemayo yanawezekana ikiwa kuna mfumo usiobadilika sana wa bei ktk nchi yetu,

  Kwa kumbukumbu yangu kiwango cha Tsh. 5000 kwa siku ilipanda kwa Mara ya Mwisho mwaka 2006, hapo unaweza kutathmini ni miaka mingapi imepita na kuna mabadiliko yapi.

  Wanayo haki ya kudai hiyo pesa, na labda na ujue kuwa hiyo pesa si kwamba wote hutumia ovyo wapo ambao huagizia kwa familia zao vijijini.

  Huko kijijini unakosema eti wahitimu wakimbilie kuna nini? Iwapo hata hao wanakijiji wanalalamika? Na kwa mitaji ipi wanayotoka nayo vyuo?

  Vijana hawa bado wanayo haki na kwa hakika wanaumia na hasa nkijaribu kuangalia gharama za chakula kwa siku, usafiri kwa wale wakaao off campus, matumizi ya utoaji vivuli makaratasi ya kiada na ziada, kulipia pango na nk.

  Wanayo haki na kweli wanaumizwa na ni lazima serikali iwafikirie maombi yao, kuliko huku kupambana na polisi kuumiza vijana wetu na hata kuleta hofu miongoni.

  Bado na nasema bado wanafunzi wa chuo wanadharauliwa na hii ni kutokana na kipato chao kidogo, wanaishi ktk umasikini mkubwa mchana kutwa wanavuja jasho kwa kutembea toka Mabibo hadi Campus na chupa za maji mikononi kujipooza, wanajipa matumaini kwa kuvaa suruali za vitambaa na tai shingoni, siri ya mifuko yao mungu ndio anajua;

  Nasema na nina uchungu katika hilo kwani nimeyajua mateso kwa miaka mitano sasa.

  Hakika wanayo shida na tusiwadharau au kuwabeza kwani si kweli wote ni wajinga na wana akili moja, yapo magumu yalowasibu na sasa wamechoka.

  Ombi lao wananchi tuwasaidie.
   
 5. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #5
  Feb 5, 2011
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Wengi wanajadili matokeo ya tatizo wanasahau kujadili chanzo cha tatizo. Mpaka tutapofanikiwa kumaliza chanzo cha hili tatizo, migomo yote itakwisha. Ni makosa makubwa sana kulinganisha sera ye elimu ya juu ya nchi za magharibi na Tanzania.

  Kwanza mbadili sera ya nchi yetu ifanane na ya nchi za kimagharibi afu muone kama kutakuwa na migomo na kam-kunji kama hizi!
  My take: Wanafunzi wangeshinikiza zaidi serikali iboreshe mazingira wanayosomea, manake hayaendani na hadhi ya chuo kikuu.

  Kama ukifika UDSM na AU, ni pachafu si darasani, kafeteria, au vyooni. Hata ofisi za walimu wao zinatia aibu sana na nyingine ni kichefuchefu hasa zile zinazokuwa karibu na vyoo. Wanachuo na wanataaluma kwa ujumla wanatakiwa wapewe majibu kwanini ruzuku za matengenezo hazitolewi!
   
 6. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #6
  Feb 5, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Nafikiri unajadili event badala ya concept..

  Concept hapo ni kujitegemea sio mgawanyiko wa masaa ya kusoma mchana na usiku, na jinsi mtu atavojishikiza. Kujitegemea kwamba mtu kuwa proud kugharamia elimu yake. Kama huezi kutafuta walau fedha wakati wa semester au term, basi fanya hivo wakati wa likizo. Kama hiyo nayo huezi basi tafuta pesa kabla hujaanza masomo..hamna kisingizio hapo.
   
 7. Mbaha

  Mbaha JF-Expert Member

  #7
  Feb 5, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 697
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mkubwa hivi unajua mazingira ya shule za vijijini kweli???? Unajua shughuli za kilimo zinavyofanyika vijijini na jinsi zinavyolipa???? Unajua purchasing power ya wanavijiji wa kweli huko vijijini??? Nina mashaka kama unafahamu hayo yote.

  Otherwise usingezunguzia hayo uliyoyazungumzia kirahisi hivyo.....
   
 8. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #8
  Feb 5, 2011
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,858
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  Nyie vibaraka tumewashtukia.
   
 9. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #9
  Feb 5, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,763
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  kunawatu niwageni na mazingira ya vijijini kazi yao ni kulopoka tuuu mkuuu!
  MAZINGIRA YA KIJIJINI YANGEBOLESHWA HAKUNA MTU ANGEPENDA KUKAA MIJINI!
   
 10. E

  Elder Member

  #10
  Feb 5, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hao graduates tu hawana kazi, na kwa bahati mbaya likizo wanayoweza kutafuta hizo pesa unazowaambia watafute ni wiki tatu maana most of them likizo ndefu huwa wanakuwa field...
   
 11. muhogomchungu

  muhogomchungu JF-Expert Member

  #11
  Feb 5, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 375
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Madai ya wanafunzi vyuo vikuu ni utoto, ulimbukeni . ni vigumu eti leo mwanafunzi alipwe elf 10 kwa siku huku mfanyakazi Polisi, Mwalimu na wafanyakazi wengine wakilipwa elf 4 kwa siku.

  Mtoto aliyeamaliza kidato cha 6 juzi na kujiunga chuo eti leo andai mapesa mingi kiasi hicho.anataka alipwe au kwa jina la kisomi mkopo wa elf 10 kwa siku . Lkn bado maraha, amstarehe wanayofanya vyuoni hazitasaidia, hazittaosha na matatizo yatazidi. vimwana na vibaba vitazidim kulala vyumba vya wanafunzi kama mabibo kufanya majabozi , kwani baadhi yao huona wakiwa chuoni ndio mwanzo wa maisha ya juu.

  Simu ya bei kubwa, redio kubwa chumbani, friji, tv na mambo mengine ya anasa huku familia zao zikila muhogo mchugu na dagaa. huku wanafunzi hao wakitoka familia maskini wakitumia fedha hizo kw anasa. Club zote za pombe na vinywaji vichafu wakifurika, disko, muziki na maisha ya ajabu yakiwa ndio maisha yao ya kila siku, wengine wakina mji huku wakiwa n elf 5 kwa siku huona tayari ajira kwao
   
 12. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #12
  Feb 5, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Anasa zipo saana vyuoni, lakini je madai yao yanamsingi kimahitaji wawapo vyuoni?
  Ama ni agenda fulani nyuma ya pazia?

  Naomba kuuliza tu ili nijue.
   
 13. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #13
  Feb 5, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,175
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  hebu changanua hiyo 5000 jinsi wewe ungeitumia kwa siku.

  usiweke unafiki.

  usi-assume kuwa uko mwaka wa pili, tatu au nne (hawa hawana garantii ya kupata vyumba kwenye mabweni ya chuo).

  assume kuwa unaishi main campus au mabibo hostel.
   
 14. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #14
  Feb 5, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,763
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  mkuu we sema lolote ni haki yako but wanahaki ya kudai hiyo pesa maisha yamebadilika sana najua hata wewe unajua hilo!
  KAMA POLISI WANALIDHIKA NA RUSHWA WAIPATAYO!

  NI LAZIMA TUWE WAKWELI! PESA HIYO HAITOSHI!
   
 15. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #15
  Feb 5, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Usisahau na subscription ya DSTV ambayo ni $80 kwa mwezi.
   
 16. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #16
  Feb 5, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Du hapana kabisa kuwalipa 330,000/= kwa mwezi wakati hatuna hakika watafaulu wote na kuanza kazi ni unafiki. Kazi wajitafutie wenyewe km wengine tulivyofanya na vyumba ni jukumu lao km mabibo pamejaa. Hivi hiyo hela itatoka wapi? kila mwaka wanaongezeka na Watanzania ndio wanaowakopesha kwanini JKT isingerudi ? wajifunze Uzalendo kula kulala kusoma wangevijua iko siku tutashindwa wadhibiti hawa vijana
   
 17. PatPending

  PatPending JF-Expert Member

  #17
  Feb 5, 2011
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 490
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Je hivi wanafunzi wa UDSM waliwasilisha hoja na maombi yao ya kuomba kuongezewa posho kwa mamlaka husika? Ni vyema tukaona nyaraka hizi ili tufahamu ni muda gani umepita tangu zilipowasilishwa maana hii itatusaidia kujua sababu hasa za maandamano haya.
   
 18. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #18
  Feb 5, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Nimeishi main kampasi na bado pesa haikutosha, nimechemsha maji ili kupunguza garama na ilishndikana, hiyo ni UDSM, SUA ambako mdogo wangu anasoma kuna kozi kama vile tourism desa 1 kupga kopi ni hadi elf 70, sasa hyo pesa ya stationery itatosha?

  Okay nikipata hilo 'bum' nilitakiwa nilipe ada 40% coz bodi ndio walpanga kwa mujibu wa vigezo vyao, narudi kwenye 'akomodeshen' sasa, kwakuwa UDSM na vyuo vingine, nililazimika kununua ubavu kwa laki na nusu, so ukichanga na mwenzio ina maana sehemu ya kulala m2 mmoja, mwalala wawili huku mkiwa mmetoa jumla ya laki 3.

  Hall two ndipo nilipoishi, je hiyo hela itakaa elfu 5? Huyo anaesema hivo ana maana gani? Mbona polisi au wafanyakazi wengine anaosema wanapewa elfu 4 ni watu wa anasa?

  Hebu aache ushabiki, aangalie uhalisia mi naunga mkono KUNJI
   
 19. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #19
  Feb 5, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  katika nchi zingine, kantini zilizoko vyoni bei za vyakula zimekuwa subsidized na kama mwanafunzi anataka chakula cha bei kubwa basi hulazimika kutoka out. hii inasaidia mikopo midogo kutosha kwa mahitaji ya chakula vyuoni, sasa hapa kwetu hakuna unafuu wowote kula chuoni aou kutoka out na saa nyingine ni nafuu kwa mama lishe nje kuliko ndani ya chuo.

  pia kukaa off campus kumechangia kuongeza tatizo la nauli kila siku amabazo nazo ziko juu na zinapanda kila siku kutokana na kupanda kwa mafuta na sababu nyingine. badala ya kujenga hosteli za kutosha maeneo ya karibu na cho, wamekuwa wakijenga maduka. ni muhimu seriakali ikchukua hatua za muda mrefu kuhakikisha maisha vyuoni yanakuwa nafuu na hivyo kupunguza migogoro kaa hiyo.
   
 20. Shakazulu

  Shakazulu JF-Expert Member

  #20
  Feb 5, 2011
  Joined: Feb 23, 2007
  Messages: 940
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Wewe hujasoma Tanzania. Tanzania hakuna mabox ya kubeba au wazee wa kuwaangalia wakati wa likizo kama mnavyofanya huko "majuu".
   
Loading...