Sijasoma Tz wewe ndie ulienisomesha? watu wengine bana..Wewe hujasoma Tanzania. Tanzania hakuna mabox ya kubeba au wazee wa kuwaangalia wakati wa likizo kama mnavyofanya huko "majuu".
If u r looking for excuses u will always find them..hivi kuingiza hela lazima uajiriwe?hao graduates tu hawana kazi, na kwa bahati mbaya likizo wanayoweza kutafuta hizo pesa unazowaambia watafute ni wiki tatu maana most of them likizo ndefu huwa wanakuwa field...
Kiwango cha posho ya Tsh 5000 kwa siku kwa mwanachuo kwa mazingira ya sasa kwa Tanzania, ni kiwango kinachoweza msaidia kama anaakili ya kupanga vizuri bajeti yake. Kama wanachuo wanataka kuishi kwenye hoteli za gharama au kifahari ni jukumu lao na wazazi wao kuongeza pesa za kujikimu kifahari. Kiwango cha Sh laki moja na nusu kwa mwezi kama yuko makini na kufikiria zaidi future yake anaweza panga vizuri bajeti na akaishi bila tatizo kubwa. Ila kama anataka awe anakwenda kula Hamburgers McDonalds ni juu yake na familia yako kuongeza matumizi.
Tumepitia vyuo vya Tanzania na tumepitia vyuo vya mataifa makubwa, kwa ulinganifu katika masuala ya posho naweza sema kumbe Tanzania ni bora mwanafunzi anaweza pata posho hiyo kuliko vyuo vya nchi tajiri. Watu hatukulala usingizi ni darasa na kazi. Uwapo kazini wakati wa mapumziko ndo unafanya homework, hakuna kulaza damu.
Tusiwe watu wa kulaumu serikali katika kila kitu, tulaumu yale ya msingi lakini katika hili mimi binafsi nasema hapana.
Watanzania tuko wavivu mno wa kujituma na kufikiri. Mazingira yako huru mno kujishughulisha Tanzania kuliko mataifa yaliyoendelea.
Utakuta walimu wanakimbilia kufundisha shule za mijini, kumbe shule za vijijini zina nafasi zaidi kwa kujiongezea pato kwa kujishughulisha na kilimo au kufungua biashara ndogo ndogo kusaidia wanavijiji kupata bidhaa ambazo wanapata taabu kuzifuata mbali. Mshahara wake ungezalisha zaidi kuliko mijini anamalizia kwenye starehe na gharama kubwa ya maisha.
Athari wanazopata wanachuo katika migomo yao ni kubwa kwao wanafunzi kuliko viongozi wanaowanyooshea vidole wakati wanaishi maisha ya starehe, na waendapo vyuoni ni kwenda kuwapiga msasa wa kisiasa tu. Kinachofanyika sasa vyuoni ni kama cheer ambayo ni kufuata mkumbo tu na kulazimisha wasiotaka lazima wafanye vinginevyo watadhurika, huku ni kuwanyima wengine uhuru wao wa kujiamulia wanavyotaka. Haki ya uhuru ni uamuzi wa dhamira safi baada ya upembuzi yakinifu.
Serikali ina mengi ya kufanya si wanafunzi tu, elimu, mawasiliano, afya, na huduma nyingine za jamii. Hata Chama kingine kikitawala hakitamaliza matatizo hayo kwa siku moja.
Anasa zipo saana vyuoni, lakini je madai yao yanamsingi kimahitaji wawapo vyuoni?
Ama ni agenda fulani nyuma ya pazia?
Naomba kuuliza tu ili nijue.
Inshu siyo kuwekewa mezani kila kitu!! ni mfumo wenyewe ulivyowekwa. vipindi vinapigwa hadi saa 2 usiku utapata muda wa kufanya ndugu yangu? Hata hayo mashule ya kata yangekuwa yanawatumia hawa jamaa yasingekuwa yanapata zero hata moja, lakini kwa vile hakuna " The called Coordination ya Elimu kuanzia chini hadi vyuo vikuu au vya elimu basi ni bora liende". Kila mtu anataka anavyoona, nchi haina mipango ya maana kiutekelezaji katika nyanja yeyote zaidi ya mipango kwenye karatasi.
My take:
1) Hawa jamaa wawwape muda wa wao hata kutafuta kazi mitaani japo kufundisha kwa masaa mawili mashule ya kata inapunguza matatizo kibao. Nchi inatatizo na walimu wakati ni kiasi cha kutwist some parameters na kujikuta wanasolve mengi.
2) Kama ni kumwagilia bustani za barabarani, wanalipwa nako poa ni sera tu. Wanaweza kukataa mara ya kwanza baadae watakubali.
jamani kuna mfumuko wa bei,maisha yamepanda sana......huwezi sema wajilipie wenyewe kwakuwa huo mfumo haupo na hawawezi uanzisha wao....mi kweli,sioni kama inatosha.....wengi wanakosa vyumba na jioni badala ya kula vyakula vya bei ya chini vinavyopatikana chuoni wanakula mtaani wanakoishi ambako vyakula ni ghali, walipie kodi na nauli za kurudi mitaani walikopanga, bado dispensary ya chuo ukienda mara dawa hamna,mara wakupe referral uende kwa Kariuki...jamani,lets be realistic......
mtu ana vipindi asubuhi hadi saa moja usiku vinapishana tu masaa mawili au moja,kazi atafanya wapi?? biashara ataanzisha na nini kama hela ya mlo hana???Serikali iwaangalie wanafunzi......:coffee:
shoprite+game ni maeneo ambayo wanafunz wanaweza kufanya kaz kwa shift!so waliosaini mikataba wangeweka kipengele hcho
Umaskini unatuua na mwisho kuuana. Kumnyooshea kidole baba yako kila unachoona hakiendi sawa ni upeo finyu. Kaa na baba yako uone bajeti ilivyo ndo utaelewa vipaumbele alivyoweka baba yako. Kisha utatambua kwamba kumbe natakiwa nini nimshauri baba afanye ili kuoongeza kipato na kupanga vizuri bajeti.
Nilipokuwa shule ya msingi awamu ya kwanza ya utawala wa nchi hii nilikuwa nafanya kazi siku za likizo ili kupata mahitaji ya shule kuwasaidia wazazi wangu. Nilipokuwa sekondari vivyo hivyo. Nilipokuwa chuoni serikali ilikuwa na utaratibu wa wanafunzi wakati wa likizo kwenda kufundisha shule za msingi na kupata posho. Na wengine walikuwa majaribio viwandani na idara za serikali au mashirika binafsi.
Utaratibu huo ingefaa pia ufanyike siku hizi.
Ratiba vyuoni isiwakabe mno wanafunzi, ili wapate muda wa kuhangaikia riziki.
Tatizo la walimu shule za kata lingeweza tatuliwa kwa wanachuo kuwa part time instructors.
Vyuoni ratiba za wanachuo ugawanywe katika vipindi viwili, ili kuwepo na wahudhuriaji wa kipindi cha asubuhi na wahudhuriaji wa kipindi cha alasiri. Muda ambao wanafunzi wako huru ndio wanatakuwa wanafanya kazi kujikimu kama kufundisha mashuleni nk.
Hatima wanachuo waweke kando starehe ili kupunguza gharama za maisha zisozolazima ili kupanga vizuri bajeti ya chuoni
Usemayo yanawezekana ikiwa kuna mfumo usiobadilika sana wa bei ktk nchi yetu,
Kwa kumbukumbu yangu kiwango cha Tsh. 5000 kwa siku ilipanda kwa Mara ya Mwisho mwaka 2006, hapo unaweza kutathmini ni miaka mingapi imepita na kuna mabadiliko yapi.
Wanayo haki ya kudai hiyo pesa, na labda na ujue kuwa hiyo pesa si kwamba wote hutumia ovyo wapo ambao huagizia kwa familia zao vijijini.
Huko kijijini unakosema eti wahitimu wakimbilie kuna nini? Iwapo hata hao wanakijiji wanalalamika? Na kwa mitaji ipi wanayotoka nayo vyuo?
Vijana hawa bado wanayo haki na kwa hakika wanaumia na hasa nkijaribu kuangalia gharama za chakula kwa siku, usafiri kwa wale wakaao off campus, matumizi ya utoaji vivuli makaratasi ya kiada na ziada, kulipia pango na nk.
Wanayo haki na kweli wanaumizwa na ni lazima serikali iwafikirie maombi yao, kuliko huku kupambana na polisi kuumiza vijana wetu na hata kuleta hofu miongoni.
Bado na nasema bado wanafunzi wa chuo wanadharauliwa na hii ni kutokana na kipato chao kidogo, wanaishi ktk umasikini mkubwa mchana kutwa wanavuja jasho kwa kutembea toka Mabibo hadi Campus na chupa za maji mikononi kujipooza, wanajipa matumaini kwa kuvaa suruali za vitambaa na tai shingoni, siri ya mifuko yao mungu ndio anajua;
Nasema na nina uchungu katika hilo kwani nimeyajua mateso kwa miaka mitano sasa.
Hakika wanayo shida na tusiwadharau au kuwabeza kwani si kweli wote ni wajinga na wana akili moja, yapo magumu yalowasibu na sasa wamechoka.
Ombi lao wananchi tuwasaidie.