Madai ya Janeth Shayo, Mkazi wa Uru, Moshi, kutosikilizwa

Sina cha kusema zaidi ya furaha niliyonayo kwa wewe mkuu wa kitengo kujitokeza.
Ama hakika bado tunao viongozi ndani ya nchi yetu...mama hongera na umekuja kuondoa sintofahamu juu ya swala la huyu mlalamikaji.
Sasa ni fursa yake ajitetee na kuwa wazi zaidi ili kama nae anawasingizia walimu achukuliwe hatua hata ya kuomba radhi.

Asante sana mama na ukawe na kazi njema.

Jamiiforums iishi milele kwa mfumo huhuu
 
Mh Waziri naomba umfikishie salama zetu waiziri wa Afya Mh Ummy Mwalimu kuwa na yeye tuna muhitaji hapa tuwe tunajadili nae maswala mbali mbali akipata muda …asiogope sisi ni watu waungwana sana! Hongera
 
Mimi natamani sana Viongozi wote nchini ambao Ofisi/Nyadhifa zao zinahusika na kuhudumia jamii wawe kama MAMA yangu Dorth Gwajima wawemke urahisi wa kuwasiliana na wanachi maana siyo rahisi kwa raia wa kawaida kumfikia
Ubarikiwe sana.!
 
ukisoma comment kwenye mada ya awali iliyoletwa na mtu asiyejulikana, na hii aliyoleta mh waziri , ni wazi maoni ya watu wengi yapo kawaisa sa , yanayobeza, yanayo kejeli , yanayo tukana , na yanayo vunja moyo.
wengi wetu walao tumepata elimu kiasi cha kuitwa wasomi, na tunajua lipi linafa kuchangiwa namna hii ama namna ile, lakini maoni yetu na majibizano yetu mwenye mada husika yamekaa kitoto sana na kijinga sana, na ndio maana watendaji wengi wa serikili hawawezi kujitokeza hadharani kama waziri doroth gwajima kwa sababu ya majibu yetu ya kijinga yaliyo mengi.
 
Imetolewa taarifa hapa Jf hoja mchanganyiko na anayejitambulisha kama unknown kuwa: mtajwa hapo juu sikumsikiliza alipokuja mara ya pili kwamba amekwama kwenye mfumo wa huduma dawati la jinsia.

Kwanza napongeza watoa taarifa za kijamii pale penye changamoto za kijamii ambazo, zimekwama hatua moja au nyingine na jamii inahitaji msaada.

HATA HIVYO, naomba kuweka taarifa ya ufafanuzi kuwa, sijawahi kuongea na mlalamikaji kwa simu na wala huwa situmii huduma ya kuongea kwa simu kwa yeyote yule bali huduma ya kuandika ujumbe Ili nibaki na kumbukumbu na ndiyo nilitangaza hivyo.

Nimemuomba mlalamikaji hizo namba ambazo alizipigia baada ya yeye kukanusha pia kuwa hakuongea na mimi, tangu asubuhi hadi sasa jioni nasubiri. Uzuri Nina Imani mifumo ya simu za kuongea inatunza kumbukumbu, hivyo sitarajii nikanushe halafu kumbukumbu ziseme niliongea naye.

Huenda aliongea na namba za call center au namba za madawati ya Jinsia eneo husika, ambapo, tangu asubuhi nimeomba anitumie kumbukumbu husika, bado hajanipatia.

Aidha, kwa taarifa zaidi kuhusu shauri hili ni namba
MOS/IR/1950/2024 KIFO CHA MASHAKA ambapo, Watuhumiwa 5 wamekamatwa na Polisi kwa mahojiano (taarifa ya Polisi imeambatishwa hapa chini kwa rejea sn 3).

WITO WANGU; Watoa taarifa za jamii pamoja na pongezi kwa kazi kubwa mnayofanya, vema muwe mnachukua taarifa pande zote siyo moja (strike a balance). Vinginevyo tutayumbisha mshikamano wa pamoja katika kupambana na matukio haya.

Ahsanteni sana, mbarikiwe wote, Kila mmoja kwa kadri alivyochangia.View attachment 2935559View attachment 2935560

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
Asante kwa Taarifa Mh Waziri Dr Gwajima
 
Kila la heri, mkiona nimechelewa, ni kutoona mapema tu. Hata hivyo, daima nikiona nitasema lile neno ambalo naamini ndiyo lenyewe. Tunajenga pamoja, ahsanteni sana kwa ushirikiano

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
Hongera sana Dkt. Gwajima D kwa kulitolea ufafanuzi suala hili ingawa taarifa ya polisi imetoka kwa kuchelewa inaweza kutengeneza dhana kuwa ilitolewa baada ya kusomwa hapa JamiiForums.
 
Hivi ndiyo wananchi tunapenda kupata msaada wa haraka, mitandao imekuja na imepunguzwa urasimu usio na tija katika kupata huduma kama hivi sasa, mawaziri wengi na viongozi mbalimbali wangekua wanatatua mambo kama hivi tungekua na jamiii yenye furaha zaidi tungefikia rank namba moja kati ya nchi yenye furaha zaidi

Ni kama mama unajua nini unafanya ndiyo manaa una interact na jamiii kwa urahis hongera sana waziri gwajima endelea kukaza we need viongozi wa sampuli yako ili jamii tupate utatuzi wa haraka


Dkt. Gwajima D

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante Mh, tunakupenda Sana Mama unafanya kazi kubwa Sana ya kuipambania jamii na kuweka usawa.
Napenda kiongozi anayejishusha km huyu, amejibu kwa haraka km mtu wa kawaida tofauti na mawaziri wengine. Hebu jaribu kuandika kuhusu wizara km ya uchukuzi usikilizie km Mbarawa atajibu, yule mpemba ana kiburi sana. Hata Mchengerwa si rahisi kujibu tuhuma za humu mtandaoni. Dr. Mungu akubariki sana.
 
Back
Top Bottom