Madagascar: Watu 6 wafariki huku 47,000 wakiyakimbia makazi yao kutokana na Kimbunga Batsirai

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
1644217644972.png


Watu sita wamefariki nchini Madagascar baada ya Kimbunga Batsirai kupiga kisiwa hicho kilichopo kwenye bahari ya Hindi. Kisiwa cha Mananjary na miji ya karibu ya imekabiliwa na uharibifu mkubwa.

Shirika la kudhibiti majanga nchini humo limeeleza kwamba zaidi ya watu wengine 47,000 wameyakimbia makazi yao kutokana na dhoruba iliyoleta mvua kubwa na upepo mkali usiku wa kuamkia Jumapili.

Mkurugenzi wa kitengo cha udhibiti wa hatari katika shirika hilo la kitaifa linaloshughulikia maafa nchini Madagascar, Paolo Emilio Raholinarivo, ameelezea juu ya maafa hayo kwenye ujumbe mfupi kwa shirika la Habari la AFP.

Baada ya kupata nguvu katika Bahari ya Hindi na vilevile kutokana na upepo mkali uliofikia kasi ya maili 145 kwa saa, kimbunga hicho kilipiga karibu na kisiwa cha Mananjary. Kwa mujibu wa idara ya hali ya hewa kisiwani humo, kwa sasa kasi ya upepo mkali imepungua hadi takriban maili 80 kwa saa.

Wakaazi wa kisiwa cha Mananjary na miji ya karibu ya Manakara na Nosy Varika wameelezea juu ya uharibifu mkubwa uliosababishwa na kimbunga hicho, wamesema mapaa ya nyumba yameezuliwa na miti pamoja na nguzo za umeme zimeangushwa hali inayofanya barabara kutopitika na kuyaacha maeneo mengi yakiwa yamefurika.
 
Back
Top Bottom