Hivi kweli Jamii Forums - The home of great thinkers ndio watu wanaandika kuwa Tanzania tunahitaji exchange of power kwa style ya Madacascar. Hivi kweli tunahitaji mtu asiyeheshimu katiba ya nchi ajinyakulie madaraka? Hivi kweli tunahitaji kiongozi anayeungwa mkono na watu ambao idadi yao rasmi haijulikani, just because they live in the capital?
Hivi iwapo humu Jamii Forums kuna vijana wa shule za msingi na sekondari wanasoma maoni ya namna hiyo, watapata fundisho gani?
Kwa changamoto tu labda pitia hapa BBC Africa have your say
BBC NEWS | Have Your Say | What next for Madagascar? ili upate maoni ya wengine duniani especially kule ambako walishawahi kudanganyika kuwa mtindo uliotumika Madagascar unafaa.
Mtanzania usidanganyike, anayeshindwa kuwaconvince wapiga kura wamchague hapaswi kulazimisha kujiingiza mwenyewe madarakani. Huko ni kuwadharau wananchi na katiba ya nchi.