Mada Zetu Ni Mwanga Wa Ulimwengu.

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
1. Enyi wanajambo, ujumbe upokeeni,
Leo hii tumeona, tuje kuwaelezeni,
Yote totakayonena, myaweke akilini,
Mada zetu ni mwanga wa ulimwengu.

2. Tunawauliza swali, tafadhali sikieni,
Yeyote mwenye akili, asikize kwa makini,
Aliye Mzalendo kweli, ajibu toka moyoni,
Mada zetu ni mwanga wa ulimwengu.
.

3. Gonjwa la Ukimwi lipo, mijini na vijijini,
Na waathirika wapo, wengi wasio kifani,
Je wewe hapo ulipo, umesaidia nini?
Mada zetu ni mwanga wa ulimwengu.

4. Dawa za kulevya nazo, nyingi zauzwa sirini,
Waathirika wa hizo, twawaona mitaani,
Katika hili tatizo, watoa shauri gani?
Mada zetu ni mwanga wa ulimwengu..

5. Wewe mwana Mtandao, umefanya jambo gani?
Kutenda au kunena, kama Mt. Yoseph
Ulipita kila kona, kwa wenzetu mitaani?
Mada zetu ni mwanga wa ulimwengu.

6. Je kueneza Democrasia, kwa ndani na mipakani,
Kuutangaza ukweli, wa habari za undani,
Ulitekeleza hili, au uliingia mitini?
Mada zetu ni mwanga wa ulimwengu.

7. Nataka kuwaeleza, hata muwe na Imani,
Ya mafisadi kufukuza, tena kukesha madani,
Wajibu mkipuuza, hamtafika kileleni,
Mada zetu ni mwanga wa ulimwengu.

8. Hata mkienda misa, asubuhi na jioni,
Wajibu mkautosa, mkauweka pembeni,
Elewa hilo ni kosa, kwa wanaharakati wote,
Mada zetu ni mwanga wa ulimwengu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom