Mada za kulinganisha vyuo ni za kipumbavu kwa sasa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mada za kulinganisha vyuo ni za kipumbavu kwa sasa!

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by micro_almunia, Oct 25, 2011.

 1. m

  micro_almunia Senior Member

  #1
  Oct 25, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Wandugu wa Jukwaa la Elimu, nimeona niwasilishe hili kutokana na mijadala isiyo na tija ambayo tunaianzisha kwenye hili jukwaa.

  Naamini jamii-forum, especially hili jukwaa lilianzishwa kwa ajili ya kujadili 'mambo ya msingi' yanayohusu elimu changa inayotolewa hapa Tanzania (ikiwemo hiyo unayopewa wewe - kwa aliye mwanafunzi).

  Mtu kukaa na kujaribu kukisifia chuo chako huku ukiponda kingine inaonesha immaturity kwenye hiyo elimu uliyopewa na unayojaribu kuitafuta.

  Binafsi nawashauri wana-jukwaa wabadili mwelekeo na kuanza kujadili mambo ya msingi yahusuyo elimu na si kupoteza muda kushindana kwa mambo ya kipuuzi. UDSM, MZUMBE, UDOM, MUHAS, IFM, CBE, SUA n.k. vyote ni vyuo vilivyoanzishwa kwa ajili ya kunyanyua elimu za watu. Vyote vina mahali viko imara, na vina mahali viko dhaifu. Mbaya zaidi, ubora wako mwanafunzi haupandi kwa wewe kudahiliwa katika chuo fulani (specifically siku hizi TCU ndio wadahili). HEBU TUWEKE HOJA ZA MSINGI - KILA MTU AJIPIME UWEZO WAKE WA KUJADILI MAMBO YENYE TIJA KISOMI.

  This is Forum - Home of Great Thinkers, ni tofauti na mitandao mingine kama ulivyo facebook. Hatujaingia humu kwa bahati mbaya, tumeinguia kuleta positive impact kwa wana jamii wetu wa Tanzania.

  Thank you!!!!!!!!!!!!!!!
   
 2. H

  HAMY-D JF-Expert Member

  #2
  Oct 25, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 6,825
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  kaka umeongea mambo ya msingi kabisa na hii thread kama moderator angeweza angeifanya kama welcome note yetu kwenye hili jukwaa.

  Ila kaka katika hiyo orodha ya vyuo ulivyoviandika hapo umebugi(umekosea) kukiweka IFM maana akistahili kuwa orodha moja na udsm,sua,muhas,aru na mzumbe.Ukikitoa utaifanya hii thread kuwa outstanding.
   
 3. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #3
  Oct 25, 2011
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Yale yale aliyoyosema micro-almunia kwanini IFM akistahili kuwa orodha moja na hivyo vingine, kwani chenyewe sio chuo cha elimu ya juu?
   
 4. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #4
  Oct 25, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,953
  Likes Received: 1,509
  Trophy Points: 280
  Uko UDOM au St Joseph nini?
   
 5. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #5
  Oct 25, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,029
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  We utakua wa mzumbe tu.
   
 6. H

  HAMY-D JF-Expert Member

  #6
  Oct 25, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 6,825
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  sisomi chuo cha kata(udom) wala sisomi chuo cha binafsi(sjcet).Swala la kueleza mapungufu ya chuo ni moja ya majukumu yetu kama wadau wa elimu na kwenye hilo hatuta nyamaza,ila tatizo linakuja katika kufikisha hayo matatizo jukwaani,wengi tunatumia njia zisizo sahihi na walengwa nikimaanisha wanafunzi wa hivyo vyuo wanakuja juu ndio hapo penye matatizo.Kama kweli unaamini chuo unachosoma hakina mapungufu yanayo semwa humu jukwaani basi inabidi vitolewe vielelezo kuthibitisha tuhuma sio sahihi kuliko kukibeba beba wakati kibovu tu.Tuepuke kupotosha umma wakiwemo wadogo zetu wanaotarajia kusoma katika hivyo vyuo.
   
 7. m

  micro_almunia Senior Member

  #7
  Oct 25, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hahaha! Inaelekea wewe bado uko chuoni...

  Maliza uingie kwenye soko la ajira. Hakuna mwajiri anayeweka chuo chako kama basis ya kukupa au kutokukupa ajira. Hata ungesoma chuo gani, in the end what matters is YOU. Kama unasoma chuo bado, 'zingatia ubora wako' maana hao unaofikiri kuwa si bora ndio wanaopigana zaidi na hatimaye utawaona wakishinda kila competition utakayokuwa pamoja nao. Kipindi hiko university rankings will have no effect on your future. [This is to help you to get ready]

  The reason why intellectuals wanaaibika wakifika kwenye interviews (pamoja na matokeo yao mazuri), ni kuweka focus kwenye mijadala isiyo na msingi na isiyofanana na usomi wao.

  NASHUKURU KWA ALIYEIELEWA HII POST. HAIJAWEKWA IPATE REPLY NYINGI, IMEWEKWA ILI WADAU TUSOME IBADILISHE MWELEKEO WA MIJADALA TUNAYOTEGEMEA KUANZISHA NDANI YA HILI JUKWAA LETU.

  Mchango wa wanafunzi, wafanyakazi na wadau wote wa elimu unahitajika ili kuinua kiwango cha elimu ya Tanzania ambayo inapelekwa na siasa nyingi kuliko kuzingatia ubora.
   
 8. Apollo

  Apollo JF-Expert Member

  #8
  Oct 25, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 4,889
  Likes Received: 1,377
  Trophy Points: 280
  naona huna thread ya kutoa.

  Hayo mambo yapo, mbona unakuwa kama hujawahi kujichanganya na watu. Hayo mambo ya kawaida. Unataka mtu akiponde chuo chake?

  Mfano mimi, huwa natetea udsm kwa sababu nipo hapa na maisha nayaona, sasa unakuta mtu wa SUA anaongea kitu ambacho hana uhakika, unategemea nitamuunga mkono?

  Hamna haja ya kuongea tu, its human nature..itakubidi uzoee. Mimi sioni kama kuna ubaya. Cha msingi msitukanane au kukashifiana.

  Kila mtu ana haki ya kutetea anachokipenda.
   
 9. m

  micro_almunia Senior Member

  #9
  Oct 26, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  wenye akili za kimaendeleo wameelewa!
   
 10. Apollo

  Apollo JF-Expert Member

  #10
  Oct 26, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 4,889
  Likes Received: 1,377
  Trophy Points: 280
  hakuna maendelea yanayoweza kutokea dunia hii kama hakuna competition...
   
 11. only83

  only83 JF-Expert Member

  #11
  Oct 26, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Mkuu your real a great thinker of our times..well done!!
   
 12. SILENT ACtOR

  SILENT ACtOR JF-Expert Member

  #12
  Oct 26, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Msome vizuri micro.. ana mtazamo wa juu zaidi. Kama wewe unatetea UDSM eti kwa vile tu ume/nasoma pale, je mimi ambaye nimesoma UDSM,na UDOM, kwa akili ya kipumbavu niugawe mwaka nusu mbili? Nusu moja nitetee UDOM na nusu UDSM? Jibu umeshapewa ,kuwa na mtazamo mpana wa kubuni njia za kutatua matatizo ktk vyuo vyetu. Watu wengi wanaoshadidia kusifu vyuo hata darasani mara nyingi huwa "bogus" Imagine wewe ni mzazi una mtoto vyuo viwili au vitatu tofauti, utatetea UDSM ulikosoma? Acheni hizo bana!
   
 13. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #13
  Oct 26, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  umrongea point to some extent but ushindani wa elimu na mazingira ni muhimu sana duniani kote na ndio lengo kubwa la kuwa na shule na gradings tofauti
   
 14. Engager

  Engager JF-Expert Member

  #14
  Oct 26, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 329
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Mmemaliza??
   
 15. Apollo

  Apollo JF-Expert Member

  #15
  Oct 27, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 4,889
  Likes Received: 1,377
  Trophy Points: 280
  swala sio kutetea chuo, swala ni kuelekeza kitu ambacho ni fact na hakuna uongo kwa kuwa mazingira umeyapitia. Sio lazima usome ktk chuo then ukitetee, unaweza ukawa umewahi kuishi maeneo ya chuo hicho na kuna details unazozijua. Sasa unakuta mtu anaongea mada inayohusu udsm, halafu mada yenyewe inapotosha, unakuta mimi ninayesoma hapa ninajua mtoa mada amedanganya. Unategemea nitamuunga mkono? Ukimpinga tu, watu wanadai unatetea chuo chako...sasa mtu ufanyaje?

  Sizungumzii mtu apendelee chuo, no! Aongee kitu ambacho ni fact na awe amekiona kweli.
   
 16. Apollo

  Apollo JF-Expert Member

  #16
  Oct 27, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 4,889
  Likes Received: 1,377
  Trophy Points: 280
  Naona watu wengi wanakaa kukiponda chuo cha udsm hapa JF, Wanajipotezea muda tu. Hapa sio mahala pake, pelekeni malalamiko kwenye tafiti zinazotoa ranks ya vyuo.
   
 17. njoro

  njoro Senior Member

  #17
  Oct 27, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 178
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  We na UDSM yako,mzumbe,UDOM,IFM,IAA,..n.k. Soma kwa bidii afu uingie kwenye soko la ajira ndo utajua
   
Loading...