Mada yenye ukakasi: Majini yanayoishi nasi hapa duniani yenye umbo la kibinadamu (Demons/fallen angels in human form)

Hili la kusema ya kuwa Majini ni Malaika walio tupwa toka mbinguni,linahitaji mjadala pweke ili kujua ukweli ni upi hasa. Kadhalika kuna maswali mengi yasiyo kuwa na majibu.

Kwanza naomba uniambie Malaika ni nani na wana sifa gani ? Kadhalika Majini ni nani na Wanasifa gani ?

Sisi Waislamu tunawazungumzia Majini katika jinsi yao pweke na si Malaika.
Binadamu wa kijini aliemuoa Au alieolewa na binadamu wa kawaida mtoto atakayezaliwa lazima atakua jini.
Hakuna ndoa kati ya jini na mwanadamu,wala hakuna kuingiliana yaani kujamiana kati ya jini na mwanadamu,huu ni uongo wa wazi ambao watu wanaishi nao bila kuufanyia utafiti.

Majini wamepewa uwezo wa kuwa na vitimbi na kutoa taarifa za siri na kuwadhuru watu,pamoja na kujibadilisha katika maumbile tofauti.
 
Hizi ni story na hadithi bunifu za waja kuwasilisha mawazo yao katika uhalisia.

Ila ni ngumu sana kumuona jini katika umbile lake la asili,sababu tu wamepewa uwezo wa kujibadilisha. Kadhalika husemwa ya kuwa Jini hakai zaidi ya masaa matatu katika umbile ambalo si lake,atabadilika tu.

Maumbo ambayo majini hupenda kujibadilisha kwayo ni umbile la nyoka mweusi,au mbwa mweusi.
 
Endelea kujidanganya Mubarridi
 
Hivi majini ndo mashetani?

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
wewe bila shaka utakuwa msabato.
 
Uzi safi
 
Kuna majini mengine yanaunga mkono kwenye Chanjo ya Corona. Wanawashawi binadamu wengine wakachome Na vitishisho juu. Nenda kichwa kichwa wakati wezako wapo kwenye mission
 
Mkuu vp kuhusu Stori za jini mahaba..au story za mtu hawezi kuoa au kutolewa kisa amefunga ndoa ya kiroho na jini
 
Bado huwajui majini kajifunze tena mkuu.
 
Amini unachoamini, ila ukweli ni kuwa majini walio na umbo la kibinadamu hapa duniani wapo, na tunaishi nao Aisha j
Sio kihivyo ulivyoelezea wewe.
Majini wana uwezo wa kujigeuza geuza katika maumbo mbalimbali kama ya binadamu,nyoka,paka.
Lakini hawezi kujiweka kama binadamu kwa miaka yote eti kila siku awe anakuja kusoma shule na wewe miaka na miaka au awe jirani yako wa miaka yote hakuna kitu kama hicho kwani wao wana ulimwengu wao tofauti na sisi tunapoishi.
Anaweza kujitokeza mara moja tu pale anapoamua kujidhihirisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…