Mada maalumu ya mapenzi: Anakupenda kwa dhati au unachunwa tu?

Mada maalumu ya mapenzi: Anakupenda kwa dhati au unachunwa tu?

Holoholo

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2023
Posts
6,729
Reaction score
13,748
Wakuu,
Ushawahi kujiuliza hata siku moja kuwa mpenzi wako(iwe mmeoana,mchepuko au mpango wa kando) anakupenda kweli au anakutumia kwa maslahi binafsi akiyapata anakimbia?

Mfano,kuna wanaume wanakuwa na wapenzi wao kwa ajili tu ya kupata burudani ya mwili na moyo lakini hana malengo na huyo mwanamke,mwingine anampenzi wake wa kike kwa vile huyo mwanamke ana hela,hivyo anataka awe anahongwa

Hali hii kwa wadada ndio imetawala,unakuta dada wa watu yupo kimaslahi,kwa ajili ya pesa,zikiisha anakimbia.

Mfano,kuna jamaa anafanya kazi ktk kampuni binafsi,ana pesa lakini ni mbaya kimwonekano,komwe hilo,kichogo na ni black with matege,amemuoa mwanamke mzuri,huyo mwanamke huwa anatamka live kwetu mume wake akiwa kaenda kazini"mimi huyu jamaa sijampenda nimempendea pesa tu,akipokea mshahara nishamwambia tuwe tunaugawana na hufanya hivyo"

Lakini jamaa hujiona anapendwa kweli yani.

Kwa msingi huu,je huyo mpenzi,mwenza wako unampenda kwa sababu gani?
 
Sijui kwakweli, ngoja waje
FB_IMG_1752904236774.jpg
 
Hii nchi ishakua ngumu sana maana minaona hata mapenzi ni uhaini tu...🤣
 
Wanawake wengi siku hizi wapo kwenye mahusiano kimaslahi zaidi.
Mapenzi ya kweli yamepungua kwa Kasi Sana.
 
kila mtu yuko kwenye mahusiano kwa maslahi yake. Mwanaume anataka afaidi uzuri wa mwanamke wake, wakati huohuo mwanamke anataka kufaidi hela zako. Mapenzi ni biashara ya nipe nikupe. Hayo yanayoitwa mapenzi ya kweli ndio yanakuwaje?
 
Back
Top Bottom