Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Ninaomba ushauri kuhusianana gari aina ya toyota WISH mwenye uzoefu aje anipe experiences
 
Wadau nina vitz clavia, nkiweka mafuta ya 10, 000 yaan lita 5, pale kwenye gauge panaleta bar mbili. Lakini nkitembea mfano kutoka tangi bov mpaka posta then nkirud toka posta nkifika mbuyuni, ile bar ya mwisho ina anza ku blink (kuchezacheza) wadau kwa watumiaji wa vitz, is it normal kwa mafuta ya lita 5 kwa distance hyo gari kuanza kublink ile alama ya E ikiashiria fuel tank imeishiwa mafuta? Au kwa kublink kwa hyo E bado naweza kwenda distance ndefu? Gari yangu ni CC 1290.

Mkuu niuzie hii gari kama bado unayo. Nahitaji sana
 
Wadau nina vitz clavia, nkiweka mafuta ya 10, 000 yaan lita 5, pale kwenye gauge panaleta bar mbili. Lakini nkitembea mfano kutoka tangi bov mpaka posta then nkirud toka posta nkifika mbuyuni, ile bar ya mwisho ina anza ku blink (kuchezacheza) wadau kwa watumiaji wa vitz, is it normal kwa mafuta ya lita 5 kwa distance hyo gari kuanza kublink ile alama ya E ikiashiria fuel tank imeishiwa mafuta? Au kwa kublink kwa hyo E bado naweza kwenda distance ndefu? Gari yangu ni CC 1290.
Ni kawaida Vitz Clavia Full fuel tank 42ltrs ila napenda kuchanganua Reserve Tank 7litrs kwa hyo ukiona bar ina blink ujue unaanza kula Reserve Tank km unataka uamini ikianza kublink kaweke Full tank fuel utaona mafuta utakayopimiwa yatakuwa 37Ltrs kwa hapo utakuwa umenielewa
 
Wakuu poleni na majukumu nina mark x yangu yenye engine ya 4GR kuna wakati inakuwa na mis na wakati mwingine ukiendesha ina shitua kama vile inachanganya then inapunguza kasi lakini pia wakati huo ikiwa inaishiwa nguvu ukikanyaga accelerator mshale wa RPM unafika sehemu hauendelei na unashuka wenyewe huku ukiwa bado umekanyaga.
Naomba msaada nini shida.
 
kiipwi cha ngoghwe sidhani kama zipo Altezza 4S na kama zipo ulaji wake waweza uwe hautofautiani sana na 6S
ANGALIZO:
Unaweza ukawa na gari 6S na ikatumia mafuta vizuri zaidi kuliko mwenye 4S! Hii ni kutokana na uendeshaji, kwa mfano unatoka shekilango kuelekea mjini unajua kabisa ukifika big brother lazima upunguze mwendo lakini mtu anaivuta mpaka spidi 80 halafu akifika big anapunguza mpaka spidi 30 then anavuta tena akifika tiptop anapunguza tena huo ni uharibifu was mafuta, kwa jinsi hiyo utakuwa unapoteza mafuta mengi bila sababu

Vilevile hata safari ndefu ongeza mafuta taratibu na jitahidi kucontrol spidi yani kama una hakika kipande fulani hakina kupunguza mwendo ongeza mwendo taratibu mpaka spidi uitakayo kisha nenda nayo hiyo mpaka utakapotaka kupunguza punguza taratibu pia

Ukiwa mtu wa kupanda na kushuka yani mara umevuta toka spidi 80 mpaka 120 mara ukashuka ghafla mpaka 70 kisha mara ukavuta tena mpaka 120, 30, 40 nk kisha ukashuka ghafla utaisoma

Mwisho uendeshaji wa mjini ni ghali mno kwa mafuta kwakuwa break ni kila dakika
Mimi kwa uzoefu wangu altezza nyingi 4 cylinder zinasumbua sana engine lakini ukipata 6 cylinders iko poa na kuhusu mafuta sio kweli kama inakula sana
 
Wakuu poleni na majukumu nina mark x yangu yenye engine ya 4GR kuna wakati inakuwa na mis na wakati mwingine ukiendesha ina shitua kama vile inachanganya then inapunguza kasi lakini pia wakati huo ikiwa inaishiwa nguvu ukikanyaga accelerator mshale wa RPM unafika sehemu hauendelei na unashuka wenyewe huku ukiwa bado umekanyaga.
Naomba msaada nini shida.
Most likely coil zimeshachoka za kubadili
 
Hello wakuu...nina mambo mawili naomba niulize.
1. Hivi unaponunua shockups za gari...unatakiwa upewe na coil springs au zile zinanunuliwa tofauti?
2. Engine oil best kwa Carina Si ni ipi...huwa natumia SAE 40...je ni sawa???
 
Kubadili springs ni optional... Mara nyingi tunachobadili ni shock ups... Engine oil hiyo ni sahihi Ila pata genuine
 
Nimekupata, aksante sana kaka Mshana Jr...changamoto ipo hapo kwenye kuipata ambayo ni genuine...naijuaje???
Hivi kaka Mshana...bima ya gari ikishaexpire...ukirenew nilazima utumia kampuni hilo la awali au naweza lipa kwa kampuni lingine ninalopenda???
 
Oil kwa Carina yako sio sahihi oil sahihi ni 5w30 au 10w30 hasa kwa hapa nchini unashauriwa utumie mojawapo kati ha hizo
 
Aisee hizo oil huku nilipo hazipatikani kabisa...ipo ile 20w50...wapi naweza pata hapa nchini???
Kwa Tanzania hii nadhani hakuna sehemu ambapo hakuna magari yanayofika kutokea hapa dar es salaam nadhani ukiitaji utapata hata kwa kutumiwa
Kwa ushauri kuhusu oil na vilainishi +255719263074
 
Nimekupata, aksante sana kaka Mshana Jr...changamoto ipo hapo kwenye kuipata ambayo ni genuine...naijuaje???
Hivi kaka Mshana...bima ya gari ikishaexpire...ukirenew nilazima utumia kampuni hilo la awali au naweza lipa kwa kampuni lingine ninalopenda???
Bei ndio inatofautisha.. Bima unaweza kubadili kampuni bila shaka
 
Back
Top Bottom