Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Maelezo yako hayajajitosheleza hapo kuna matatizo sehem mbili inawezekana.

Swali je unaposhuka mteremko usipoweka N gari haizimiki ukiweka D unashuka fresh?? Kama jibu ni ndio basi gari haina shida ya umeme.

Kama ukiweka D bado gari inazimika basi hapo kuna shida katika mfumo wa magufa na kitu kinachosababisha kwenye tank ndani huwa kuna kuwa kama kuna kiconterner au kibox kinachohifadhi mafuta ili yasitawanyike kitakuwa na shida.
Nikiweka D haizimi ila nikiweka N inazma baada ya mda kidogo say 3-5sec..
Ila swal hapa ni kuwa kwann zamn nilikuwa naweka N inakwenda tu na haizimi ila kwa sasa ndio inazima??
 
Jamanii wakubwa naomba nielekezwe bei ya oil ya gear box Nissan tiida CVT fluid NS-2 bei gani inauzwa kuna fundi kaniambia laki na nusu ni kweli?
Inauzwa laki hadi laki na ishirini inategemea na sehemu. Mi pia Nina Tiida huwa nabadilisha.
 
Mwenyewe kuelewa anisaidie, gari yangu niktembea inawasha taa ya injini halafu inakuwa Kama inapungua nguvu na nikizima na kuwasha inatembea kawaida Hadi muda tena inaweza kurudia hivyo hvyo naomba nipate pa kuanzia nifanye nn!! Msaada.
 
Warning light ya timing belt most likely
 
Nina toyota hillux d. Csbin 1995 ina 159,000km, 3Y engine direct injection cc1998 ndo nimeagiza juzi petrol consumption ni kama landcruiser yaani 6 to 7 km per liter.
Tatizo linaweza kuwa nini? Engine inanguruma vizuri na haitoi moshi. Nimefanya service na kubadilisha plugs nimeweka genuine toka BOSCH.
 
Hakuna tatizo, kuna baadhi ya engine za 3Y hiyo ndio consumption yake.... Kama zilivyo baadhi ya engine za Rav 4
 
Almost but not that much durable like IST
Mkuu, nataka niichukue hiyo Spacio (new model), ila inaenda kutumika kule kijijini/milimani Ugweno.(nahisi unapafahamu) kwa ajili ya mizunguko ya hapa na pale.

Unanishaurije? Itafaa kwa mazingira na matumizi hayo kwa kule milimani kwetu?
 
Barabara zimeboreshwa siku hizi hivyo hakuna shida
 
Mkuu mshana msaada kati ya rav 4 1999 na carina kwa matumizi ya kazi na familia fuel consumption zake ziko vip
 
Back
Top Bottom