Mada hii ni maalum kwa wanawake watusaidie kujibu maswali haya

Hivi kwa nini ukipingana na wanaume hata kwa mambo madogo,unaitwa Feminist/activist?hili nalo ni swali eti?hata humu hii topic utaiona..soon itakavyokua,lol ni watu kurushiana makombora,sasa hivi wamelala,ngoja waje...pure entertainment!:D:D:D:D:D:D:D:D:D:D
Acha uongo wewe! Yaani mwanaume ashabikie Yanga wewe ushabikie Simba uitwe feminist??? Sema kwa kuwa mshakuwa na feminisim kichwani mwenu mengine mnabishana na wanaume mnaona kawaida kumbe ni harakati mmeshamezeshwa tayari na ni ngumu nyie kugundua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1.Kulea kumebadilika,more Schooling,more income,more power,more choices,kama you can afford a cook,why bother teaching your daughter how to cook??,sasa na mtoto kamuona mama akitoka kazini,ni kuangalia TV.,au yuko kwenye computer,basi ana imitate that,sababu watoto huangalia wazazi wao kama role models.

Kingine ukiangalia mambo ya revolution;certain traits(sijui neon sahihi) zimekua changed over time because of changes in the environment,Kulea back then ilikua kuosha vyombo,kupika,kufua ndio malezi yenyewe,walifanya hivyo kwa kuwa walikua adapted to their environment,hakukua na revolution of technology. Sasa its our time may be its not necessary kumfundisha mtu kupika,sababu any dish can be studied online through youtube tutorials may be ??:rolleyes::rolleyes::rolleyes::rolleyes::D:D:D:D,The use of advance technology,Education,Money etc has made our life easier and we don't need to kufundisha our kids 'manually' ,and future kids will change even more compared to us.....kwa mfano akitaka kuchukua juice kwenye fridge analituma tu li ROBOT linaenda kumchukulia..hahahahah..kuna point nilitaka kuisema sijui kama nimewakilisha vyema.
Mkuu chagua luga moja bac

Sent using Jamii Forums mobile app
 
2.Nina amini ndio,ipo siku wanawake watakuwa sawa na wanaume ktk nyanja zote yaani kiuchumi,siasa etc.

Kwasasa wanawake tumeamka sana na kufunguka tofauti na hapo awali,karibu kila sector mwanamke yupo.Lakn pia wanaume baadhi yao wamejisahau sana kutimiza majukumu yao ktk ngazi za familia unakuta mama ndio anaibeba familia,hiyo inatupa creadit kuwa ipo siku tutakuwa sawa .
Mabadiliko ya dunia yanakuja polepole na kwa kasi pia kisichowezekana saivi kinawezekana ila miaka 50 ijayo kutakuwa na ndoa za jinsia moja nyingi kuliko izi tulizozoea vilivyokatwaza saivi vinafanyika Mungu atusimamie

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kuanzia nitajibu maswali machache kwa uono wangu;..swali namba moja,.malezi ya wakati huu na wakati wa nyuma kidogo ni tofauti kwasababu,moja utandawazi,pili elimu na tatu ushindani..
UTANDAWAZI;wanawake wengi wa kipindi hiki tuko busy sana na mitandao ya kijamii,teknolojia inatupeleka puta kwelikweli kiasi kwamba muda wa kuangalia familia na kufanya shughuli za familia na kijamii hatuna tuko mitandaoni tunapuyanga,muda wa kupitia madaftari ya watoto wakitoka shule hatuna lakini muda wa Instagram tunao wakutosha,majukumu yetu tumewahamishia wadada wa kazi kwa kusema eti "si nina mlipa pesa" tunasahau kwamba kuna wakati familia zetu jamii zetu hazihitaji pesa,.zinahitaji uangalizi,usimamizi,na ufatiliaji wa karibu wa mzazi/mama...ikumbukwe kuwa sisi ndio walezi wakuu wa familia zetu hilo ni jukumu tangu kuumbwa kwa dunia,ina maana tusipokuwa na muda na watoto wetu,familia zetu maadili lazima yayumbe tuu..

ELIMU;elimu ni nzuri hata biblia imesema "mkamate sana elimu usimuache aende zake" lakini elimu hii kwa baadhi ya wanawake imeleta mambo hasi badala ya chanya katika suala zima la kusimamia malezi ma maadili ya watoto,kwanini?kwasababu wanawake wengi wasomi wana Ile kitu "mimi msomi bwana naanzaje kufua nguo za watoto wakati hause boy/girl yupo" aah atafanya Dada,yeye akiamka asubuhi kama ni mwajiriwa basi ni kazini akirudi usiku sana kachoka ni ale alale,hajui watoto wameshindaje,wamekula nn,hajui hata kama mtoto/watoto wana umwa yeye kila kitu kamuachia dada,.kisa ni msomi ana majukumu mengi ya kazi hana muda wa kutosha kuangalia familia,.kwahiyo impact inakuwa kubwa na inawa cost watoto kiukuaji..na ndio maana ndoa za wasomi wengi ndio zenye matatizo kuliko za wasio soma..

USHINDANI;hapa ni kati ya mwanamke na mwanaume hahahah me niseme tuu jamanii mwanaume atabaki kuwa mwanaume na mwanamke halikadhalika,.haya mambo ya 50/50 yanaleta shida hadi kwa watoto kwasababu mama atataka baba nae anyonyeshe wakati hana maziwa😂😂kusaidiana ni lazima lakini haiwezi kuwa mwanamke akawa sawa na mwanaume kimajukumu NEVER..tusijidanganye muhimu ni kila mtu asimame kwenye zamu yake na majukumu yake baaasi..haya mashindano yanayowatesa ni watoto wetu wanakuwa katika misingi mibovu isiyopendeza..
 
2.Nina amini ndio,ipo siku wanawake watakuwa sawa na wanaume ktk nyanja zote yaani kiuchumi,siasa etc.

Kwasasa wanawake tumeamka sana na kufunguka tofauti na hapo awali,karibu kila sector mwanamke yupo.Lakn pia wanaume baadhi yao wamejisahau sana kutimiza majukumu yao ktk ngazi za familia unakuta mama ndio anaibeba familia,hiyo inatupa creadit kuwa ipo siku tutakuwa sawa .
 
Hivi kwa nini ukipinganana wanaume hata kwa mambo Mie lmadogo,unaitwa Feminist/activist?hili nalo ni swali eti?hata humu hii topic utaiona..soon itakavyokua,lol ni watu kurushiana makombora,sasa hivi wamelala,ngoja waje...pure entertainment!:D:D:D:D:D:D:D:D:D:D[/QUOT

Mie niliandika comment yangu nikaopt kuifuta....huu uzi wale wootw wavivu wa kifikiri watajaa hapa km nzi nakuambia..wenye gubu na stress watajaa hapa..wenye miwivu ya maendeleo watamininika hapa..tena ww ulivyo hvyo hahaaa bora usiendelee kuchangia...bado kipanga m1 hajashuka km mwewe hapa😂😂😋.kifupi wanaume hawapendi sie tupige hatua..wanafurah ubaki hapo hapo!...
 
Mama/Dada tunavyoambiwa usawa tulitegemea mtu asikuike usawa huo kama kupata Haki zote stahiki na misingi bora ya mambo mbalimbali. Ambavyo kuhalisia vipo na wanapata, Ni usawa gani mnataka?!
Lakini Feminism inapitishwa kupitia usawa na matoke yake ni ubaguzi, unyanyasaji, ukandamizaji, upotoshaji, chuki, dhuluma, mateso na mengine mengi.

- Baadhi ya shule Government & Private wanatenga wanafunzi kwa jinsi zao, na hawawi wawazi wanafunzi wanapohoji. Pia utoa sababu za tabia na nidhamu ilhali wakiwa-favour KE.
- Sheria mbalimbali zinawalinda KE hasa mabinti ilhali wapo vijana pia seems vijana hawa exist. Mfano: Sheria ya binti apataye mimba shuleni, inamsukuma 30 years jail sentence kijana na kumuacha binti kwa mantiki gani?! Tutofautishe kubaka na kupewa mimba.
- KE kuonekana anathamani kuliko binadamu yeyote na rika zote kwa ME kwenye jamii, nyakati za majanga na uokoaji KE uanza kwa kisingizio ni dhaifu, wakati wakishupaza midomo husema TUNAWEZA ilhali hao hao ndio wanalilia usawa.
- KE wa leo akisema "nabakwaaaa" huchomoki hata kama haikuwepo intention hiyo lakini ME akisema "nabakwaaaa" aisee.

Ni mengi lakini nashindwa hata kuandika.
Wafuatao ni watu hatari sana kwa ME
• Umi Mwalimu
• Joyce Ndalichako
• NGO's[/QUOT😂😂
😂😂😂
 
Laiti mngeamua kusimama kwenye nafasi yebu ya ubaba dunia ingekuwa sehem nzuri sana..sasa majukumu kwa wanawake yamekuwa double zaid kwetu..
Familia tulishe..kila kitu tuhakikishe kipo sawa....ada tusaudiaep kulipa...tukalime walau shamba kwaajili ya chakula nyumbani..tufue tupike...
Lakin mwisho wa siku maadili yakimomonyoka wa kwanza kulaumiwa ni mama!..Bora Yesu arudi tu kwakweli!

ps:Wanaume punguzeni utegemezi!
 
3) Heshima ya mwanamke au mwanamme Kiislam hazina tofauti. Mbora ni mwenye ku mcha Mwenyezi Mungu. Hatutazami kabisa vigezo ulivyoweka wewe.
Huu ni mtazamo wako binafsi au ni mtazamo wa uislam kwa ujumla wake ?

Je unazungumziaje ile dhana kwamba mwanamke akizini katika uislam na jamii ya kiislam adhabu yake apigwe mawe mpaka kufa ilihali mwanaume huachwa bila adhabu yoyote ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari,
Mada hii ni maalum kwa wanawake na kama wao ndiyo wahusika wakuu naomba watusaidie kuelezea kwa uwazi zaidi haya maswali hapa chini.

1. Kwanini malezi yamekuwa magumu sana kipindi hiki ambacho wanawake wengi ni wasomi walio elimika vizuri, wana vipato vizuri na kushika nyadhifa kubwa ndani ya jamii kuliko kipindi chochote kuwahi tokea duniani ???

2. Kiuhalisi: Je, unaamini kwamba ipo siku ambayo mwanamke na mwanaume watakuja kuwa sawa katika nyanja zote za kijamii, kisiasa na kiuchumi ???

3. Kuhusu dhana ya maendeleo ya mwanamke: Je, unaamini kwamba mwanamke ataonekana wa maana na kuheshimika ndani ya jamii pale ambapo atakuwa na kitu cha kushindana na mwanaume au kumfanya mwanaume aogope mfano Elimu, Pesa au Cheo ??? (Kama jibu ni Ndiyo: Je, unaamini kwamba mwanamke anaweza kuishi kwa furaha na kupata amani huku akiwa amaezungukwa na wanaume wanaomwogopa)

4. Kuhusiana na falsafa ya Feminism: Je, unaamini kwamba mwanamke ambaye ni mfuasi wa hii falsafa anaweza kuwa mama mzuri katika malezi ya watoto wa kiume ??

5. Kwanini wanawake wa kiafrika wa miaka 30 iliyopita ambao walikuwa hawajasoma sana wanasifika kwa malezi mazuri kuliko wanasifika kwa malezi mazuri kuliko wanawake waliosoma wa kizazi hiki ?? Ushahidi wa hili ni mmomonyoko wa maadili ambao umelikumba taifa kipindi hiki.

6. Hypothetical Question: Je, siku ambayo mwanamke na mwanamume watakuwa sawa katika kila nyanja, unadhani dunia itakuwa ni mahali salama zaidi ??

7. Dini ni moja ya chanzo cha wanawake kufanyiwa ubaguzi na kukandamizwa na mwanaume. Vitabu vitakatifu kama Biblia na hata sheria za dini ya kiislamu ya baadhi ya nchi kuna sehemu hazimzungumzii vyema mwanamke au hazimuweki mwanamke katika nafasi nzuri: Je, ni kwanini wanawake wengi sana wanaendelea kushikilia hizo dini ilhali wanataka usawa na mabadiliko ndani ya jamii ??

8. Unaielewaje dhana ya "Strong Woman" or "Iron Lady" : Kati ya Oprah Winfrey, Margreth Thatcher, Cookie wa Empire, Michelle Obama, Mange Kimambi, Melinda Gates,Janet Kagame na Bikira Maria Mam wa Yesu nani ni Strong Woman or Iron Lady ?

9. Je, ni sahihi kupima nguvu za mwanamke kwa kuangalia uwezo wake wa kufanya mambo ambayo mwanaume anayafanya ??

10. Je, wewe uliyeelimika unahisi unaishi vizuri na kwa amani na mumeo, kuliko ambavyo mama yako ambaye hakuelimika sana aliishi na baba yako ?? Na je, unahisi wew uliyeelimika umefanikiwa sana katika malezi kuliko ambavyo mama yako ambaye hakusoma sana alikulea wewe ???

NB: Siyo lazima ujibu maswali yote, unaweza ukajibu hata moja tu.

Wasalaam and Happy Valentine..
🌷🌷🌷🌷🌹🌹🌹🌹🌷🌷🌷🌷

Mushobozi Lumumba, Jr.

CC: Heaven Sent , Nalendwa, Valentina, Prishaz
Mh! lumumba umefikiria nini mpaka ukaja na haya? duh! ngoja tuone yajayo kama yatafurahisha au kufundisha kwa wachangiaji.
 
Kwa kuanzia nitajibu maswali machache kwa uono wangu;..swali namba moja,.malezi ya wakati huu na wakati wa nyuma kidogo ni tofauti kwasababu,moja utandawazi,pili elimu na tatu ushindani..
UTANDAWAZI;wanawake wengi wa kipindi hiki tuko busy sana na mitandao ya kijamii,teknolojia inatupeleka puta kwelikweli kiasi kwamba muda wa kuangalia familia na kufanya shughuli za familia na kijamii hatuna tuko mitandaoni tunapuyanga,muda wa kupitia madaftari ya watoto wakitoka shule hatuna lakini muda wa Instagram tunao wakutosha,majukumu yetu tumewahamishia wadada wa kazi kwa kusema eti "si nina mlipa pesa" tunasahau kwamba kuna wakati familia zetu jamii zetu hazihitaji pesa,.zinahitaji uangalizi,usimamizi,na ufatiliaji wa karibu wa mzazi/mama...ikumbukwe kuwa sisi ndio walezi wakuu wa familia zetu hilo ni jukumu tangu kuumbwa kwa dunia,ina maana tusipokuwa na muda na watoto wetu,familia zetu maadili lazima yayumbe tuu..

ELIMU;elimu ni nzuri hata biblia imesema "mkamate sana elimu usimuache aende zake" lakini elimu hii kwa baadhi ya wanawake imeleta mambo hasi badala ya chanya katika suala zima la kusimamia malezi ma maadili ya watoto,kwanini?kwasababu wanawake wengi wasomi wana Ile kitu "mimi msomi bwana naanzaje kufua nguo za watoto wakati hause boy/girl yupo" aah atafanya Dada,yeye akiamka asubuhi kama ni mwajiriwa basi ni kazini akirudi usiku sana kachoka ni ale alale,hajui watoto wameshindaje,wamekula nn,hajui hata kama mtoto/watoto wana umwa yeye kila kitu kamuachia dada,.kisa ni msomi ana majukumu mengi ya kazi hana muda wa kutosha kuangalia familia,.kwahiyo impact inakuwa kubwa na inawa cost watoto kiukuaji..na ndio maana ndoa za wasomi wengi ndio zenye matatizo kuliko za wasio soma..

USHINDANI;hapa ni kati ya mwanamke na mwanaume hahahah me niseme tuu jamanii mwanaume atabaki kuwa mwanaume na mwanamke halikadhalika,.haya mambo ya 50/50 yanaleta shida hadi kwa watoto kwasababu mama atataka baba nae anyonyeshe wakati hana maziwakusaidiana ni lazima lakini haiwezi kuwa mwanamke akawa sawa na mwanaume kimajukumu NEVER..tusijidanganye muhimu ni kila mtu asimame kwenye zamu yake na majukumu yake baaasi..haya mashindano yanayowatesa ni watoto wetu wanakuwa katika misingi mibovu isiyopendeza..
Umegusa mulemule.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu ni mtazamo wako binafsi au ni mtazamo wa uislam kwa ujumla wake ?

Je unazungumziaje ile dhana kwamba mwanamke akizini katika uislam na jamii ya kiislam adhabu yake apigwe mawe mpaka kufa ilihali mwanaume huachwa bila adhabu yoyote ?

Sent using Jamii Forums mobile app
Tazama vigezo alivyoviweka mleta mada, ndivyo nilivyovijibu. Hayo ni mafundisho ya Kiislam yanapatikana ndani ya Qur'an tukufu:

49_13.gif

Qur'an 49:13. Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari. 13
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom