Machungu ya Kuishi mbali na familia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Machungu ya Kuishi mbali na familia

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Saharavoice, Feb 10, 2012.

 1. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #1
  Feb 10, 2012
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Ndugu zangu mlio mbali na familia zenu kwa sababu moja au nyingine tuungane hapa angalau tujiliwaze wakati tunaingia katika week end nyingine huku tukiwa wapweke. Leo nimepata uchungu sana nilipoongea na mwanangu kwa simu halafu akaniuliza “Baba utarudi lini” halafu akaanza kulia Najua wengine watasema, si utafute kamoja for the week end, fine, but, ni nini replacement ya watoto? Ndipo nikakumbuka moja ya wimbo wa Tancut Almasi wa Imma, Nadhani aliimba Kyanga songa na ndugu yake. beti zake hapa chini. (Batalanda utanisahihisha) Ni mbali huko uliko mamaa, nifike tuonane mamaa, tena nijue hali yako, pia nijue hali ya watoto x2 Immaaaaaaa Imma kumbuka miaka tulio ishi na wewe, Imma kumbuka watoto tumezaa na wewe, Siyo rahisi immaaa, nikusahau immaa Imma iyoleelee mamaa, mwenzio usingizi sipati, kwa ajili ya mawazo ohoooo Imma ni kazi inayotutenganisha, Na kazi ndiyo baba wa watoto wetu immaaaa, Sikuzoea Immaa, kuishi peke yangu Immaa, kuishi mbali na wanangu Imma, Imma iyoleelee mamaa, mwenzio usingizi sipati, kwa ajili ya mawazo ohoooo Immaa yolelelee mamaaa, mwenzio ninakonda Immaaaa, mwenzio nateseka Immaaaa, shauri ya kukufikiria mamaaaa Imma iyolele x2 Immaaaaaaaaaa Milima na milima ohooo Immaaa, haikutani ii mamaa, lakini binadamu wanakutana nchi yoyote duniani Immaaaa x2 Imma iyolele x2 Immaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa Week end njema.
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Feb 10, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Inaelekea umeshikilwa.
  Pole, kazi za mbali na home ni disaster.

  Niliwahi resign 24hrs kama mwehu, watoto watamu bwana hasa na wale wakubwa.
   
 3. Zabibu

  Zabibu JF-Expert Member

  #3
  Feb 10, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Aisee inauma sana hasa unapojikuta peke yako na huku umezoea kuwa na familia...hapa nilipo naisubiri likizo kwa hamu zote utafikiri mtoto wa boarding vile.mweeeeeeeeeeeeeh
   
 4. snochet

  snochet JF-Expert Member

  #4
  Feb 10, 2012
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 1,271
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Zabibu,ukianza likizo tu nunua stock ya piriton kwa ajili ya watoto,ujivinjari kwanza.wao watafrahi wakikua
   
Loading...