Macho yangu yamepoteza nguvu ya kuona karibu na mbali

varency

Member
Mar 24, 2022
15
20
Wapendwa kwa moyo mkunjufu naombeni mnisaidie kama kuna mtu ameshawahi kusumbuliwa na tatizo la macho halafu akapona naomba anisaidie jamani macho yangu yamepoteza nguvu ya kuona karibu na mbali hata TV kuangalia hadi nisogelee, simu nayo kuangalia napata tabu naweza kupishana na mtu nnayemjua lakini nisimtambue hadi anisogelee kabisa ndio nita mtambua.

Kiukweli napata tabu sana hali hii inanisumbua kwa mwaka wa 6 sasa nimeshazunguka hospopitali kubwa za macho Dar es Salaam nzima bila mafanikio kama kuna mtu alishawahi kuwa na tatizo kama hili sasa hivi amepona au ana ndugu au jamaa aliyekuwa na tatatizo kama hili lakini sasa hivi amepona tafadhali naomba ANISAIDIE.

20220529_152241.jpg
 
Taco kubwa ni dawa ya macho.
Tiba hiyo inapatikana huko nje eneo ulipo.
 
Dah! Nimekuja mbio mbio kupokea msamaha!

Pole sana kamanda. Soon madaktari bingwa watakuja kukupa mwongozo.
 
Pole kwa tatizo linalokusumbua ila hapo uliposema Dar -es-Salaam nzima je hospital gani ulienda?
 
kama umri umeenda it is normal hata mimi nowadays nakaa karibu na TV hasa ikicheza Yanga! punguza kuangalia kioo cha laptop au simu kwa Masaa mengi kwa siku, kula mchicha sana. Kuna dawa za maji ya kuweka kwenye macho nzuri, una kisukari? kapime kisukari
 
Hizo tiba nyingine utapigwa hela tu ..
Tafuta miwani maisha yaendelee.
 
Wapendwa kwa moyo mkunjufu naombeni mnisaidie kama kuna mtu ameshawai kusumbuliwa na tatizo la macho arafu akapona naomba anisaidie...
Nilijua kuna kitu hakipo sawa ulipoanza kwa kusema "mnisamehe kwa post" weka heading vizuri ili watu waweze kuona na upate msaada
 
Kapime macho mkuu, mimi tatizo ni kuona mbali, nilipima na kupata miwani naona vizuri zaidi ya HD
 
Pole sana. Una umri gani? Umepima macho na kupewa miwani nayo ikashindikana? Pressure ya macho iko sawasawa?
Umri wangu miaka 24 pressure ya macho nimepima nipo sawa kisukari sina wameniambia upungufu wa vitamini tu natumia vidonge vya vitamin mwaka wa 3 sasa lakini hamna maendeleo ndugu
 
Back
Top Bottom