Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Sijui ndio uzee wenyewe au ni mimi tu. Zamani (sasa hapa msianze kuniuliza zamani ya lini) watu walikuwa wanazungumza mambo ya mapenzi kwa staha, heshima, na kujali nani anasikiliza. HIvyo, kuna mambo ambayo dada zetu hasa wasingeweza kuyazungumza mchana kweupe namacho makavu. Walikuwa na haya au soni fulani hivi ambazo kwa kweli zilikuwa zinawafanya waonekane very sexy.
Isipokuwa tu wakishazoeana basi zile soni zinahamia hata chumbani kidogo na kama ni utundu basi ni wa wao wawili huko ndani na hata maneno ya kuchombezana yanafanywa wakiwa wao wenyewe. Lakini siku hizi - sasa msiniulize hizi nazo zimeanza lini - dada zetu ni kama hawana tena soni. Iwe ya hadharani au chumbani. Wanaweza kuzungumza mambo fulani ya kiutuuzima hadi ukashangaa. Tena wengine wanazungumza bila hata kujali kama baba, kaka au mume anaweza kujua anazungumza lugha hiyo. Yaani, kuna lugha fulani ya matusi matusi ambayo siwezi kushangaa inaweza kuwa ni turn off kwa wanaume wengi kwani pamoja na ujanja wote wanaume bado wanapenda msichana au binti mwenye staha kidogo, soni za kuchombezea na aibu fulani fulani za kike.
Kwa mfano, msichana anayepita halafu sketi ikapeperuka kidogo kujiachia akafanya haraka kujifunika au kuvuta kanga anaweza kuwa na mvuto mkubwa kuliko msichana ambaye anaweza kuwa na hilo hilo lakini akajiachia na kujisikia watu wanampigia miluzi. Yule wa pili anaweza akawa ni wa kuchukuliwa kwa kustarehe lakini yule wa kwanza akaonekana anafaa kuwa mke (wife and motherly material).
Sasa najiuliza ni wakati gani dada zetu wawe na zile soni zao za kike na aibu fulani fulani? Ni kweli wanaume hatutaki tena wanawake wenye aibu aibu au tunawaombea watokee tena? Je ni kweli wanawake wanafikiri wanaume wanafurahia msichana ambaye ana macho makavu na hana aibu kabisa? Na hasa hili la siku hizi la baadhi ya dada zetu kwenda "commando" kwa kisingizio cha "joto" kweli siyo la kuonea soni kidogo!?
Au ndio karne ya ishirini na moja yenyewe?
Last edited by a moderator: