Machinga Complex igeuzwe kuwa Business Centre

iMind

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
2,873
4,276
Moja ya sababu ambazo zinakwamisha au zinafanya uanzishaji wa biashara mpya kuwa mgumu ni gharama za juu za kupangisha ofisi. ingawa maghorofa mengi yanajengwa kila kukicha lakini bado gharama ya kupangisha ofisi ziko juu.

Ingawa ni ukweli kwamba kwa tekinolojia ya sasa, unaweza kufanya biashara ukiwa hauna physical office location, let say una watumishi wa 3 na kila mmoja anafanya kazi sehemu yoyote alipo, na mnaweza kukutana asubuhi hotelini kwa morning brainstorming then kila mmoja akafanya kazi kivyake. Hata hivyo wateja wengi hawako tayari kufanya kazi na mtu asiyekuwa na physical office. watu wanakuona kama mwizi, tapeli n.k.

Kwa sababu hiyo basi physical office bado inakua ni mandatory unapoanza biashara. Ofisi rooms nyingi zinachajiwa kwa dola, na unalipa kwa mwaka. Gharama hukokotolewa kulingana na ukubwa wa chumba unachopata. hivyo wajasiriamali wadogo inatuwia ngumu kutoka.

Kwa kua idea ya awali ya machinga Complex inaonekana ku fail, napendekeza yale majengo yageuzwe kuwa business centres. Ambapo zitatengenezwa vyumba vya ofisi vya size ya kati kwa ajili ya kufungua biashara. Wataweka common facilities kama secretarial services, printing, call centre, chumba cha mikutano etc. Lets say kila ofisi 5 zinakua na shared resources zake. Vyumba vitakua furnished na basic furnitures. Strictly hakutakua na maduka ya aina yoyote ile. Ofisi hizi zitakodishwa kwa vijana ambao wamejiari, wajasiliamali ambao watafanya biashara zinazotumia vichwa, kama consulting, computer systems development, legal services etc.

Naamini mpango huu utachochea ukuaji wa uchumi na kuongeza ajira, na itakua ni matumizi sasa ya fedha za wananchi.
Nawasilisha.
 
ukichukulia time value of money pamoja na Return On Investment (ROI), ule mradi ni hasara kwa sasa, either investment appraisal haikufanyika au ilifanyika kwa kuziba mashimo na kufanya kuwa the project is viable, kosa ni hawakusoma tendency ya wanunuzi wa bidhaa za machinga ikoje

labda tujiulize concept nzima ya machinga bussiness ni nini?

naunga mkono hoja machinga complex ibadilishwe matumizi
 
what drove those guys to put up that project was all about 10% (if not 50%) and now they've got it, no one cares!
cha msingi hapa ukiona baadhi ya biashara iliyosimama hapo DSM au kwingineko, yawezekana pesa zilienda huko nasi tukaambiwa inflated costs.
nakubaliana na wasemao kuwa "Tanzania ni zaidi ya uijuavyo" ..."Mitanzania ndivyo tulivyo"
ukichulia time value of money pamoja na Return On Investment (ROI), ule mradi ni hasara kwa sasa, either investment appraisal haikufanyika au ilifanyika kwa kuziba mashimo na kufanya kuwa the project is viable, kosa ni hawakusoma tendency ya wanunuzi wa bidhaa za machinga ikoje

labda tujiulize concept nzima ya machinga bussiness ni nini?

naunga mkono hoja machinga complex ibadilishwe matumizi
 
Halafu wakasahau "Matching Guys" aka Machinga, hufanya biashara kwa kutembeza, na si kukaa sehemu moja ili watu wawafute. Wameibukia tu na kukurupuka kufanya mambo bila kuwa na utafiti wa kutosha wa kiuchumi. Ile ilikuwa ni pressure ya kisiasa, matokeo yake mabanda yamebaki wazi na vijana wanatuletea bidhaa hadi milangoni kama kawa
 
Back
Top Bottom