MACHIMBONI: Sitosahau nilivyonusurika kufa

MACHIMBONI: Sitosahau nilivyonusurika kufa

1700575922288.png
OLI'ILOMOLOMO!
 
Kuna watu wanaitwa ma nyani ukisikia Hilo neno ogopa ni zaid ya Boko haramu. Wacha nikueleze kidogo....

Wale jamaa hawana duara maalumu wao kazi Yao nikuingia kwenye maduara ambayo Tyr yameshafika au Yana Mali Tyr hivo huvamia muda wowote hasa usiku wakiingia kazi Yao kupiga walinzi wa duara maalumu. Wakifika Wana wanakuoa salaam Shari au shwari mkuu ? Ukijibu shwari basi wataingia duarani kiroho safi kabisa wataokota Yale mawe yenye Mali tu wanaweka kwenye bob Marley (beg) ila ukijibu Shari hapo umetangaza vita wafe wao au ufe wewe Kwa kutumia zana za kuchimbia.

Kali ya yote Kuna Wakati duara(mwamba) inalipuliwa jamaa huzama hivohivo Hadi mlipuko unafanyika akiwa sehemu fln humo duarani kajibaza ni very risk but kufa hawawazi kabisa au mlipuko ukifanyika Bado Kuna vumbi wajamaa washazama kitambo.

Nadhani umeelewa ni jina maalufu sana migodini kusikia manyani na hawakoswi Hela.
Nashukuru Kwa kunielewesha ila daaah wanaume tunatafuta Hela Kwa njia nyingi Sana.
 
Sema nao jamaa walikuwa na maksudi tuu ... unamwachaje mgeni apande wakati kiroba hakijafika juu ... alitakiwa akae station..(fonka).

Those days....mwabomba,Nyakasaluma,Mwime,Nyangalata, Bukandwe,Nyakafuru,Nyakahula...
Back days niliwahi pitia mgodi wa mwabomba, shenda na Kuna mwingine lunzewe. Dah maisha ya migodini magumu sana. Tumepakia sana makinikia ya boss seleman wa ushirombo
 
Hivi sa hiv mganyalo wanatoa bei gan si tulikua tunapewa buku tatu kwa siku aisee eti hiyo ndo hela ya kula siku nzima na inaweza isije kwa wakati hapo umepiga kazi vya kutosha njaa yako
 
Mkuu duara Zina tofautiana Moja Hadi nyingine Kuna sehem kabisa ya kama ka chumba fln kadogo ni ngumu kuelewa kama hujaingia duarani hako ndo Huwa Wana kaa Wakati gunia linashuka na Huwa linakuja likigonga side Hadi side Kwa kasi so mara nyingi hukaa hivo. But Kuna wengine wabishi tu anakaa pembeni kidogo na ndicho kilichotokea Kwa jamaa huenda tu ilikuwa hivo Ili nipone ..kumbuka unaposhuka huendi direct unaenda unajipigiza kwenye Kuta za shimo (kugologosha) ni ngumu kuelezea mtu asiyewahi kushuka humu ila Kwa taswira ndo hivo
Duh, aisee pesa inatafutwa hii sio mchezo
 
Back
Top Bottom