Amba Samedi
Senior Member
- Apr 5, 2024
- 193
- 326
Habari wanaJF,
Ni mimi tena, mjoli wenu. Baada ya kuwa off platform siku nyingi, sasa narejea kwa kasi fulani hivi. Jana tu nilisherehekea siku ya kuzaliwa. 38 sio haba, na bado 38 zingine, Inshallah.Kuna swali moja ambalo linajirudia humu karibia kila siku:
"Nataka kununua [bidhaa fulani], ni wapi naweza kupata chimbo?"
Tafuta tu neno "chimbo" utakubaliana na mimi.
Jaribio la Kwanza
Hapo nyuma nilikuwaga na wazo kubwa la kuanzisha mtandao ambapo watu wangeweza kuona orodha ya machimbo ya bidhaa mbalimbali.Uzi huu hapa
Nilinunua vitabu kadhaa vilivyoorodhesha wauzaji, nikaajiri msaidizi, nikafanya research mtandaoni, nikauliza marafiki. Nilipata mawazo mengi humu (nashukuru).
Changamoto kubwa lililonikumba mimi na timu yangu ya utafiti: si rahisi kupata bei halisi kutoka kwa kila duka. Na pia, sio rahisi kudaka bei za chini na kufanya updates kila siku.
Ikabidi idea ikae parking kidogo.
Lakini leo nimerudi tena.
Kwa miezi hiyo yote,, nimekuwa nikijinoa kwenye sekta ya akili mnemba (AI) na matumizi yake katika kutatua matatizo (Agentic AI). Kwa kupitia ujuzi huu, nimetengeneza agents kadhaa (wafanyakazi wa kidigitali kutumia hiyo AI) wanaonisaidia katika mambo yangu ya siku kwa siku.
Mojawapo ya agents nloamua kutengeneza ni AI ya kunisaidia kutafuta wauzaji wa bidhaa upesi. Sifa za mfumo huu ni hizi hapa:
- Nimekusanya orodha ya wauzaji kadhaa ninaowafahamu Dar na Moro ambao wanafanya kwa bei poa.
- Nina wingas walioko Kariakoo na sehemu nyingine, wanaonipa taarifa mpya za machimbo. Kila wakiniletea taarifa bora, nawapa hela yao. Win-win.
- AI yangu ina uwezo wa kupakua habari kutoka mtandaoni (web scraping)—Instagram, Facebook, TikTok, hadi hapa JamiiForums kila siku (bila mimi kubonyeza chochote). Inachambua maoni na majadiliano kuhusu machimbo, halafu napata direction ya watu wanachokitaka na machimbo mapya. Data hii inaingizwa kwenye mfumo na kuboreshwa kila siku.
- Na sasa, nikitaka kitu, sihitaji kuzunguka. Naandika tu: “Natafuta Samsung A03s, bei nafuu iko wapi?”
Napata majibu papo hapo—maduka, bei, na mawasiliano ya simu/whatsapp ya watu 5 hadi 10 ambao wana bidhaa hiyo, kuanzia kwa anayeuza kwa bei ya chini kabisa na kuendelea.
Mfumo huu una msaada mkubwa kwangu, na ina accuracy kubwa kadri nnavozidi kuitumia na kuiboresha kwa ajili ya biashara zangu na kuwasaidia wafanyabiashara wenzangu.
Nakuja Kwenu Sasa
Kwa sasa, ninatumia hii kwa biashara yangu binafsi. Lakini nadhani ni muda wa watu wengi zaidi kufaidika. Mfumo unajitahidi kujibu maswali yafuatayo:- Winga watakulaje? Tumewaweka kuwa sehemu ya mfumo. Wakileta taarifa mpya, wanalipwa.
- Machimbo kupitwa na wakati? Tunafanya scraping kila siku, hivyo chimbo likijadiliwa tu sehemu, taarifa tunayo.
- Mtumiaji hana smartphone (simu janja)? Hakuna matata. Unatuma swali kuhusu chimbo na kupata majibu kwa njia ya SMS pia.
Lakini Naomba Maoni Yako
- Je, hii ni huduma inaweza kufaa kwa sasa? Unaweza kuitumia ama kama mfanya biashara au winga?
- Ni vipengele vipi ambavyo kama mfanyabiashara ungependa viongezwe ili kuwe na ubora zaidi? Vitu muhimu vya kuzingatia ni vipi?
- Ikiwa itakuwa huduma ya kulipiwa (kwa sababu gharama zinatumika tayari km winga analipwa, na msaidizi wangu ni full-time), ni kiasi gani kingekuwa fair kwa matumizi? Na ilipweje?
- Natafuta watu 10 wa kujaribisha baada ya maoni haya...
Na tukumbuke: Kama kuna biashara moja ambayo haikomi, basi ni ile inayosaidia watu kupata bidhaa kwa bei nafuu zaidi.
Nawasikiliza sasa...