Machemli Aibwaga Serikali Kortini

Machemli Aibwaga Serikali Kortini

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,156
Reaction score
13,267
Mbunge wa Jimbo la Ukerewe, mkoani Mwanza (Chadema), Salvatory Machemli, ameibwaga serikali baada ya Mahakama kumwachia huru katika kesi ya uchochezi iliyokuwa ikimkabili.

Machemli aliachiwa huru jana na Mahakama ya Wilaya mjini hapa baada ya upande wa mashitaka kukosa ushahidi wa kutosha wa kuthibitisha shitaka dhidi yake.

Mbunge huyo aliachiwa huru na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Ukerewe iliyokuwa imefurika umati wa watu, Faustine Kishenyi, baada ya kusikiliza ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa Jamhuri na utetezi.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Kishenyi alisema kuwa Mahakama imeridhika kuwa mshtakiwa hana hatia baada ya upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha shitaka dhidi yake.

Hakimu Kishenyi alisema katika uamuzi wake kuwa mbali ya Jeshi la Polisi kushindwa kuwasilisha vielelezo mahakamani kama ilivyo katika hati ya mashitaka, pia ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka haukuwa na hoja wala haujitoshelezi kumtia hatiani mshtakiwa.

Akifafanua, Hakimu Kishenyi alisema kuwa upande wa mashitaka ulishindwa kuwasilisha CD iliyochukuliwa wakati mshtakiwa akitenda kosa huku askari polisi watatu pekee wakijitokeza kutoa ushahidi dhidi ya mshtakiwa Hakimu Kishenyi alisema hakuna mtu aliyekwenda kutoa ushahidi kutoka nje ya Jeshi la Polisi kuthibitisha kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo la uchochezi.

Hakimu huyo alisema kutokana na waliotoa ushahidi kutoka Jeshi la Polisi pekee wakati nalo linahusika katika kesi hiyo, inaonyesha kuwa kulikuwapo na maslahi ya upande mmoja, hivyo ushahidi huo hauwezi kutumika kumtia hatiani mshtakiwa Machemli.

Awali, ilidaiwa na Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Inspekta Samuel Onyango, kuwa Machemli (39), alitenda kosa la uchochezi Oktoba 23, mwaka 2011 wakati anahutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Nyamanga kilichopo katika kisiwani Ukara, mashitaka ambayo hata hivyo, mshtakiwa aliyakanusha.

Katika kesi hiyo, ilidaiwa kuwa mshtakiwa huyo kwa makusudi aliwachochea wananchi wazuie shughuli za Jeshi la Polisi na hata kuwashambulia askari watakapokwenda katika maeneo yao kuwasaka wahalifu.

Hata hivyo, Hakimu Kishenyi alisema kwamba upande wa mashitaka unaweza kukata rufaa ndani ya siku 30 kuanzia jana.

Source: Nipashe 6/6/2014
 
images.jpg
Mbunge Machemuli
 
Ifike mahali twende mbele zaidi, badala ya kushangilia "ushindi" au kumshukuru mungu kwa kutenda "mema", tutumie akili zetu vyema. Baada ya Polisi kushindwa kesi hiyo ya uchochezi ndugu machemli afunge kesi mahakamani ya kudai findia kwa kubambikiwa shitaka lisilokuwepo.

Napendekeza fidia hiyo iwe kama anayodai Manji kwa Mengi. Hii itasaidia kuwadhibiti Polisi ambao hufanya kazi kama Roboti kwa kufahamu kwamba kesho wakifungua kesi za aina hiyo watafikishwa mahakamani kulipa fidia kutokana na madhila ambayo wamekuwa wakiyatekeleza kwa wananchi.

Nategemea Ndugu Machemli, ambaye ni kiongozi kuongoza njia kwa hjili kwa kufungua shauri la kutaka fidia n sio kushangilia "ushindi" kuwa amewabwaga polisi mahakamani, maana yake kesho watamtafuta kwa namna nyingine na kuendeleza mchezo wa paka na panya.
 
Siku moja itafika ambapo haki itatokeza kama nuru,hapo ndipo wale wagizani hatutawaona tena,siyo polisi wala tume ya uchaguzi zote zitashindwa kuwabeba. Mageuzi hayakwepeki.
 
Kuna wakati kulikuwa na zoezi la kuhakiki vyeti vya shule kwa kuanzia na Jeshi la Polisi! Lile zoezi zima lilisitishwa mara moja baada ya kugundua hata hao wanaojiita polisi wenye vyeo vikubwa vyeti vyao ni vya kugushi!!Tusitegemee kuwa na jeshi la polisi linalofanya kazi kwa mujibu wa jeshi lenyewe bali kwa mujibu wa wanasiasa!
 
Machemli ndiyo nani mbona hili jina geni halafu la ajabu sana ndiyo yupi mwigiza au mwimbaji?
 
Ifike mahali twende mbele zaidi, badala ya kushangilia "ushindi" au kumshukuru mungu kwa kutenda "mema", tutumie akili zetu vyema. Baada ya Polisi kushindwa kesi hiyo ya uchochezi ndugu machemli afunge kesi mahakamani ya kudai findia kwa kubambikiwa shitaka lisilokuwepo.
Napendekeza fidia hiyo iwe kama anayodai Manji kwa Mengi. Hii itasaidia kuwadhibiti Polisi ambao hufanya kazi kama Roboti kwa kufahamu kwamba kesho wakifungua kesi za aina hiyo watafikishwa mahakamani kulipa fidia kutokana na madhila ambayo wamekuwa wakiyatekeleza kwa wananchi.

Nategemea Ndugu Machemli, ambaye ni kiongozi kuongoza njia kwa hjili kwa kufungua shauri la kutaka fidia n sio kushangilia "ushindi" kuwa
amewabwaga polisi mahakamani, maana yake kesho watamtafuta kwa namna nyingine na kuendeleza mchezo wa paka na panya.
Nakuunga mkono kabisa. Kesi ngapi za kutunga watu wanashinda na bado polisi wanaendelea kutunga?
Watu wanasoteshwa magereza halafu story inakuwa imekwisha.
Machemuli onyesha njia kwa vitendo. Hata kama utashindwa kesi hiyo lakini watu watakuiga. Kuna watu wamesota magereza kwa sababu tu wanagombea mapenzi na OCD
 
Ingawa ni mimi nitakayeumia kwasababu kodi yangu ndiyo itakayotumika kulipa FIDIA. Lakini namshauri Mhe. Machemli afungue kesi ya KUDAI FIDIA YA MAMILIONI YA SHILINGI ili liwe fundisho kwa POLISI kumbambikia watu kesi. IF YOU WANT TO MAKE AN OMELET YOU SHOULD BREAK SOME EGGS.
 
Machemli ndiyo nani mbona hili jina geni halafu la ajabu sana ndiyo yupi mwigiza au mwimbaji?

Mkuu mbona unafanya uchambuzi kwa hisia sana. Huyu jamaa ni mwananchama wa chadema sasa ni nini kinakufanya ufikirie ni mwigizaji au muimbaji?

Vyama ambavyo kama hauelewi shughuri za wanachama wao utakuwa umefanya uchambuzi wa kisayansi kufikiria ni waimbaji au waigizaji ni vyama viwili,kutokana na sababu zifuatazo.

CCM
-Nadhani unatambua miziki,maigizo na vichekesho ni sehemu ya harakati za kisiasa kwao
-Nadhani unatambua moja ya ahadi iliyotekelezwa kwa asilimia mia moja katika zile zilikuwa kuwa kwenye ilani ya uchaguzi na ahadi za ziada za mgombea uais wao ni studio ya kisasa ya muziki.
-chama hiki ndio pekee chenye bendi ya muziki,maigizo,na. Vichekesho (T0T)
-ni mwenyekiti wake ambaye pia ni rais wa nchi kwa sasa na kama promoter au manager wa mwanamuziki mahili nchini,diamond.

ACT
-Jina tu linabeba maana husika.
-nao pia ni wahusika kuu kwenye leka company,inayojishughurisha na maswala ya ringtones na film production.

Umenielewa. Simiyu yetu?
 
Machemli ndiyo nani mbona hili jina geni halafu la ajabu sana ndiyo yupi mwigiza au mwimbaji?

usijitoe ufahamu. dhamiri inakuchoma mpaka kwenye uvungu wa mifupa na maini yako. umesoma post halafu unauliza Machemli ndio nani? nikisema wewe ni juha nitakuwa nimekuonea? shame upon you bk 7
 
Machemli ndiyo nani mbona hili jina geni halafu la ajabu sana ndiyo yupi mwigiza au mwimbaji?

Mbona babako anaitwa Madako Mulume Wasukuma hatushangai ndo wewe uje uone jina la Mchemli la ajabu?
 
Back
Top Bottom