Machemli Aibwaga Serikali Kortini

Machemli Aibwaga Serikali Kortini

Kuna wakati kulikuwa na zoezi la kuhakiki vyeti vya shule kwa kuanzia na Jeshi la Polisi! Lile zoezi zima lilisitishwa mara moja baada ya kugundua hata hao wanaojiita polisi wenye vyeo vikubwa vyeti vyao ni vya kugushi!!Tusitegemee kuwa na jeshi la polisi linalofanya kazi kwa mujibu wa jeshi lenyewe bali kwa mujibu wa wanasiasa!

Serikalini nusu ya wafanyakazi wamegushi vyeti. Binafsi miaka hio tumemaliza Azania form six kuna jamaa aligushi cheti cha form six akaajiriwa idara ya statistics na nadhani mbulula yule aliunga unga sasa hivi anacheo tu.
Haya utamkagua nani hapo.
Nipo huku nje nchi moja hivi nasoma juzi juzi naongea na teacher mstaafu wa chuo kikuu kimoja kilikuwa cha jeshi sasa ni cha kiraia jina kapuni ananiambia oooh umetoka TZ kumbe, wanakujaga wanajeshi wenu tunawafundisha ila wanafeli mitihani but so long hawafanyi kazi hapa kwetu inabidi kuwapa hivo hivo kulinda heshima zao kwao vile ni watu wakubwa huko kwenu.
Nikamkumbuka Mwema na Kova na kesi za intelligensia ya kujua tu CDM wanamkutano wapi na lini ila ukiwauliza aliempiga Ulimboka na Kibanda ni blackout kabisa. Akiuwa ocd mwanza wauaji siku ya pili wamekamatwa dar. Ila raia uchunguzi unaendelea. For sure ni kukosa weledi na shule. Sasa mtu mwenye cheti magumashi huwa hawajiamini hata siku moja atakuwa na guilt consciousness maisha yote. Na atafanya kazi kwa kujipendekeza na ile tu ya kumfanya aonekane yupo kazini basi.
 
Ifike mahali twende mbele zaidi, badala ya kushangilia "ushindi" au kumshukuru mungu kwa kutenda "mema", tutumie akili zetu vyema. Baada ya Polisi kushindwa kesi hiyo ya uchochezi ndugu machemli afunge kesi mahakamani ya kudai findia kwa kubambikiwa shitaka lisilokuwepo.

Napendekeza fidia hiyo iwe kama anayodai Manji kwa Mengi. Hii itasaidia kuwadhibiti Polisi ambao hufanya kazi kama Roboti kwa kufahamu kwamba kesho wakifungua kesi za aina hiyo watafikishwa mahakamani kulipa fidia kutokana na madhila ambayo wamekuwa wakiyatekeleza kwa wananchi.

Nategemea Ndugu Machemli, ambaye ni kiongozi kuongoza njia kwa hjili kwa kufungua shauri la kutaka fidia n sio kushangilia "ushindi" kuwa amewabwaga polisi mahakamani, maana yake kesho watamtafuta kwa namna nyingine na kuendeleza mchezo wa paka na panya.


Shitaka lilikuwepo ndo maana mahakama ilkalisikiliza, kilichotokea ni kuwa polisi wameshindwa kuthibitisha ingawa tukio lilitokea! Vile vile wamepewa muda wa kukata rufaa mahakama ya juu, hivyo tusishangilie sana mambo yanaweza badilika!
 
Back
Top Bottom