Machawa ni kama wapiga debe stendi au mawinga Kariakoo

Machawa ni kama wapiga debe stendi au mawinga Kariakoo

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
57,243
Reaction score
90,303
Watu wengi huwa wanawalaumu, kuwatukana na hata kuwachukia machawa wakiamini mtu anaweza kuacha uchawa tu akiamua. Ukweli ni kwamba sio rahisi kuondokana na uchawa kama ambavyo sio rahisi kuwandoa wapiga debe wasumbufu stendi au mawinga wa Kariakoo. Uwepo wa hawa watu hautokani na wao moja kwa moja bali wamiliki wa mali(matajiri) ambao wapo tayari kuwalipa kwa aina ya kazi zinazofanya.

Hata kwenye dawa za kulevya tatizo kubwa zaidi sio wauzaji bali watumiaji, ndio maana nchi nyingi mapambano huwa magumu sana kwa sababu huwa zimejikita zaidi kupambana na wasambazaji badala ya kuelekeza mapambano watu wasihitaji kutumia dawa za kulevya.
 
Back
Top Bottom