Machafuko ya Kidini Arusha

Dingswayo

JF-Expert Member
May 26, 2009
4,019
2,923
Jana nilisikia kupitia mtandao wa IPP na hapa JF kwamba kumekuwa na machafuko ya kidini huko Arusha. Nilitegemea kuwa leo ningepata habari zaidi kuhusu jambo hilo na kusikia kuwa viongozi mbali mbali wa kidini na serikali, pamoja na vyobo vya usalama, wamesema kitu gani kuhusu jambo hilo. Nimepitia mitandao mbalimbali ya magazeti, sijasikia tamko lolote.

Jambo hilo linatakiwa kuzungumzwa ili kutafuta chanzo cha machafuko hayo, na namna ya kuzuia na kukabili matatizo hayo ili yasitokee tema. Tukiyanyamazia, yatatufikisha pabaya. Wahenga walisema, 'mficha ugonjwa, kifo kitamuumbua'!
 
Mie sijasikia ebu tujuze ulivyosikia, wamepigana au wamerushiana maneno tu au ilikuwaje hasa. na nani chanzo mpaka ikawa hivyo
 
Na ni eneo gani hasa ilipotokea machafuko ya kidini, nini chanzo mpaka kufikia hapo?
 
mimi nilsikia kwenye habr za magazet tbc1. Wanasema ni mapigano ya wakrstu na waislam huko monduli. Sikumbuk vzr ni gazet gan. Nilsh2ka cz npo a'city!
 
Back
Top Bottom