Elly B
JF-Expert Member
- Jan 11, 2011
- 1,194
- 906
Habari waheshimiwa.
Kwanza kabisa nitangulie kuwataka radhi wale wote ambao kwa namna moja ama nyingine hoja zangu zitawagusa kwa namna ya tofauti.
Siku za hivi karibuni kumeibuka migogoro na machafuko yaliyopelekea watanzania wenzetu kupoteza maisha au kujeruhiwa. Bado ni mapema kusahau tofauti za Waislamu na Wakristo kuhusu uhalali wa kuchinja vitoweo huko kanda ya ziwa, ingawa hilo lilikuwa linagusa hisia za Watanzania wote kwa ujumla wao hasa ukizingatia liligusa imani zao. Bado kuna yaliyojiri Zanzibar ambako viongozi wa Dini za 'Kikristo' wametokea kuwa wahanga na ama kupoteza maisha. Naamini pia hata ile migogoro ya kisiasa iliyopelekea Polisi kuua raia kule Arusha, Morogoro na kwingineko nayo bado haijasahaulika.
Kwa jinsi ilivyo ni dhahiri kuwa Machafuko haya huwa ni matokeo ya fukuto za muda mrefu ambazo zimekuwa zikionyesha dalili na viashiria vya machafuko na migogoro hiyo. Na tatizo kubwa ni kwamba SERIKALI IMEKUWA NA TABIA YA KUFUMBIA MACHO VIASHIRIA VYA UVUNJIFU WA AMANI, ingawa sijui ni kwa madhumuni gani! Nitaelezea.
Tangu kuanza kwa tofauti za waumini wa dini za kikristo na kiislam kuhusu nani achinje au asichinje serikai ilkuwepo. Kuna wawakilishi wa serikali toka Wajumbe wa nyumba kumikumi (ingawa ni wawakilishi wa CCM lakini wanawajibika kwa serikali(ya CCM)). Bado kuna wale wenye dhamana ya usalama hasa polisi na TISS ambao kila kukicha wanatumia kodi za Watanzania kuendesha ofisi zao. Hao wote pamoja na wengine kwa ujumla wao walitosha kujua kuwa linalofuatia siyo salama. Kwani walikuwa wapi?
Serikali imekuwa na tabia ya kunyamazia mambo ya msingi kwa madai ya unyeti (delicate nature) bila kujali kuwa kunyamaza hakutatui tatizo badala yake raia hubaki nayo moyoni yakiendelea kuwakera. Yanapotoa moshi wanakaa kimya, yakiwaka moto wanashangaa na kushtuka! Kwani pamoja na kukubaliana kuwa serikali yetu siyo ya kidini tulisema ni dhambi kujadili mambo yanayohusu dini zetu? Kwani nani alisema Waislam wana haki ya kuchinja ambayo Wakristo hawana? Wala dini hizi hazijawahi kukaa na kukubaliana chochote. Sasa shangaa pale hata baada ya kutokea mgogoro serikali bado inasuasua kutoa kauli thabiti. Kwa nionavyo serikali ingetekeleza wajibu wake kwa wakati isingefikia hali ya kumwaga damu.
Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na chokochoko nyingi za kidini hasa kutoka kwa Waislamu kuusema vibaya Ukristo. hayo yako wazi kwenye Misikiti na mihadhara ya nje. Kwa wanaopita Manzese wanaweza kujua zaidi. Radio kama Imaan zimekuwa zikipanda na kupalilia chuki dhidi ya Ukristo kwa muda mrefu. Sitaki kuamini kuwa hizo redio nazisikia mimi tu. Serikali inategemea nini kutokana na hayo? Kwani tunafikiri nini kingetokea Tanzania kama na Wakristo wangekuwa na tabia ya kutumia redio zao na majukwaa kukashifu uislamu? Kwani kila mtu akinyamaza kwake na dini yake nini kinatokea? Katiba imemruhusu kiongozi wa dini kuzungumzia dini yoyote akiwa ndani ya sehemu yake ya ibada iwe kanisani au msikitini, napo ni kwa malengo ya kufundisha siyo kukashifu. Kama kuna yanayotuwasha kuyasema kwa nini hatuyasemei huko? Watu wanapotoka nje kwenye hadhara na kukashifu imani nyingine na serikali inakaa kimya tutegemee nini? Utashanagaa kuona Serikali inadai kustushwa pale makanisa yanapochomwa Mbagala au Zanzibar! huo ni mshangao wa dhati au unafiki na kujikosha? Bado mpaka sasa hatua za dhati hazichukuliwi bila kujali kuwa hilo linaongeza ufa na linachochea machafuko ya kesho.
Kumekuwa na ongezeko la matukio ya kupigwa kwa polisi siku za hivi karibuni sanjari na kuchomwa kwa vituo au nyumba za polisi. Hali hii ni matokeo ya serikali kupuuza vilio vya wananchi kuhusu ubovu wa vyombo hivyo. Kwa sasa ni kawaida mtu ukishikwa na polisi ukitoka hukuti vitu ulivyoandikisha kaunta! ukipata tatizo linalohitaji msaada wa polisi jikusanye kwani kama huna hela hutapata wa kukusikiliza. Ukitaka kesi iende vizuri jifunze kumhonga mpelelezi wako,ambaye bila shaka atahongwa na mtuhumiwa pia. Halafu utashangaa ukimwona mtuhumiwa yuko mtaani kesho asubuhi. Na utashangaa polisi ikilaani vitendo vya kuchomwa moto wezi na vibaka. Nafikiri niweke vizuri lugha hapa: KAMA RAIA WANAWACHOMA MOTO WAHALIFU NI KWA SABABU HAWANA IMANI NA POLISI. NA KAMA WANAWAUA MPAKA POLISI NI DHAHIRI WANANCHI HAWAONI TOFAUTI YA POLISI NA WAHALIFU! Tuache siasa kwa kudai polisijamii ina ufanisi. Imani ya wananchi itarudishwa kwa vitendo vya dhati na siyo propaganda za owongo na ukweli. Ukweli ukoje? Serikali ipo, yote yako wazi. Kesho utashangaa na serikali itakapotoa mshangao wake pale watakapoona amani inapotea.
Tofauti za kisisasa zimekuwa ni tatizo lingine linalokua kwa kasi ya ajabu. Tumeshashuhudia mara nyingi damu ikimwagika bila sababu za msingi. Ukiangalia kwa makini utakuta machafuko yalitokea kwa sababu tu polisi walitumiwa na chama flani kuharibu mkutano wa chama kingine! Ni vema ikaeleweka kuwa bila kujali kuwa nini tunafanya sasa au tuna uwezo wa kufanya, tusipofanya kwa uadilfu kuna matokeo! FOR EVERY CHOICE THERE IS ALWAYS CONSEQUENCE..ALWAYS. Lawama ya hayo inakwenda moja kwa moja serikalini kwa kuwa ni yenyewe inayoinjinia machafuko hayo ili hali ikijua kuwa wanakiuka haki za raia na wamekuwa wabinafsi kwa kutojali maslahi ya taifa kwanza.
Bado utakuta maswala kama ya MUUNGANO ambayo yanafuka moshi kwa muda mrefu sasa hayapatiwi umakini unaotakiwa. Tatizo hili limeanza siku nyingi zilizopita na limekuwa linapigwa chenga na kutatuliwa kijanjajanja tu. Kwani kuna dhambi gani watu wakikaa chini wakazungumza wanachotaka, wakakubaliana likaisha? Serikali imepiga chenga za kutosha, limeendelea kukua mpaka imefikia sasa Wananchi hawataki tena kujadili, wanataka uvunjike tu. Kwa lugha nyingine srikali imenyamazia hali ya mgonjwa ya kuteguka kidole mpaka hali imekuwa mbaya kiasi cha mgonjwa kuamua kukata mguu kabisa! Sasa na serikali inashangaa! haitaki tena mtu ajadili muungano kama wazo ni la kuvunja! bado serikali imeshindwa kujifunza. Kwa upande wake inadhani kuzuia watu wasiseme ni kusaidia. Ila kwa ninavyojua mimi ni kuongeza tatizo kwani siku watu watakapochoka kufumbwa midomo kitakachotokea si kizuri.
Kuna mifano mingi ya ukiukwaji wa haki za wananchi na watendaji wameachwa bila kushughulikiwa zaidi ya kupandishwa vyeo na kubadilishwa idara na wizara kila kukicha. Jamani hivi ndivyo wananchi tunavyolalamika. Serikali isitegemee waje malaika kutusemea. Kama hatutaki kabisa kusikia tujifunze kwa waliotangulia basi. Twende Burundi na Rwanda tukaulize madhara ya migawanyiko ni yapi! Tukitoka huko tupitie na Misri na Tunisia tukaulizie nini hutokea pale raia wanapopuuzwa. Jamani mifano ni mingi sana!!!!
Kwa kumalizia Napenda kufupisha kwa kuandika yafuatayo:
1.Tabia ya Serikali ya kunyamazia mambo ya msingi yanayowakera wananchi wake inachangia kwa asilimia kubwa kutokea kwa machafuko ambayo yangeepukwa kama serikali ingetekeleza wajibu wake.
2. Kutokana na tabia hiyo kuendelea kuachwa tutegemee machafuko tunayopalilia kutokea ila wakati yanapotokea ni vizuri ikakumbukwa kuwa serikali ndiyo ya kulaumiwa. Kwa haraka nakusudia kusema kuwa KAMA KUNA MACHAFUKO YOYOTE YATAKAYOTOKEA TANZANIA NI KWA KUWA SERIKALI IMEYASABABISHA.
Nimalizie kwa kuishauri serikali kuacha tabia ya kupuuzia mambo badala yake iyashughulikie kwa Muda muafaka na kuyapa uzito unaotakiwa.