Machache usiyoyajua kuhusu Zanzibar.

Machache usiyoyajua kuhusu Zanzibar.

Salaam wakulungwa...
Zanzibar hakuna bunge-kuna baraza la wawakilishi.
Zanzibar hakuna soko-kuna markit.
Zanzibar hakuna shule-kuna skuli.
Zanzibar hakuna kijiji-kuna shamba.
Zanzibar hakuna bomba(lakutoa maji)-kuna mfereji.
Zanzibar hakuna m'bunge-kuna muwakilishi.
Zanzibar hakuna balozi-kuna sheha.
Zanzibar hakuna daftari-kuna buku.
Zanzibar hakuna rula-kuna mstari.
Zanzibar hakuna kalamu-kuna pen/pensel.
Zanzibar hakuna machinga-kuna juakali.
Zanzibar hakuna video ya ngono-kuna kibuluu.
Zanzibar hakuna ice cream-kuna lai.
Kwa kuzingatia hayo machache unaweza kupata urahisi wakuwasiliana na wenyeji wa nchi ya Zanzibar. Karibuni kwa nyongeza.
Vile vile kwenye shule zao kama za huko bala za kata,watoto wote wanalazimishwa kusoma masomo ya dini ya Kiislam hata kama ni wakristo,mambo ya dini na mambo ya Serikali na utawala yanachanganywa,fikiria unaenda kuomba kibali Cha kujenga kanisa kwa sheha ambaye pia Ni kiongozi wa dini.
 
Kibuluu hahahahahahahah
 
Baba mkubwa, kaka yake baba, Shangazi anaitwa chach, nilisahau "Cheichei"ndio shikamoo!!
Hakuna mama fulani kuna mama yake fulani..(hii inatumiwa na watoto kumuita mama yake mtu)

Sasa jichanganye we mtoto uniite mama pretty na sio mama yake pretty kama hujashindikwa gumi la mgongo 😂😂

Kuita mama pretty inatumiwa na watu wazima tu!
 
Daaah, eti kuna Kibuluu.
siku hiyo nilikuwa nje ya banda la video sikua na kiigilio,mara nikasikia shangwe la nguvu, punde kijana mmoja akatoka nje, ndio nikamuuliza kulikoni humo ndani!? Akanisogelea karibu na kunijibu"mkanda wa leo una vipande vya kibuluu" nilipomdadisi zaidi ndio nikajua kumbe kibuluu ni picha la X.
 
Hakuna Big G kuna ubani, hakuna nyama kuku wa kisasa kuna peduu, kwenye daladala hakuna kushusha kuna kuweka, hakuna kukata kona kuna kupinda, hakuna mzunguko kuna duara,
Nina wasiwasi Mwinyi na Samia kama wanajua maneno haya,mbona hawaonekani wakichanganya hata Sikh 1.
 
Ukitaka uinjoi zenji fikia shamba, utafaidi matunda ya kila aina ni bure ghalama yako ni kuomba tu. Mashoki shoki na machenza nimeyabugia sana.

Siku moja nilitaka kununua karanga za kutafuna zilizokaangwa muuzaji akaniambia naunza njugu kwa shingi miatano.. kusikia njugu nikajua ni njugu mawe za huku baadae nilijua njugu ndio karanga kwa kule.
Koleo ni Paulo..
Kukaa wanaita kukaa kitako

Ila Utamu wa zenji upo paje, Makunduchi, Kizimkazi na Jambiani. Ukitaka kucheka sikiliza kiswahili cha Matemwe na Jambiani
vipi Kiwengwa na Nungwi baobab, unakuonaje mkuu!?
 
Nileteeeeni kibuluu nileteeeeni kibuluu nileteeeeni kibuluuu hahahahahaha lol! Hichi cha Zenj si kiswahili safi hata chembe labda tukiite Kizenj lakini hakistahili kuitwa Kiswahili eti bomba wanaita mfereji 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣 sasa sijui mfereji wanaitaje hawa wenzetu.

ndio mkuu, nasikia serikali imefungia tovuti zote za kibuluu!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom