Mac Pro Mpya Yazinduliwa Kwenye WWDC 2013

Mac Pro Mpya Yazinduliwa Kwenye WWDC 2013

ManiTek TV

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2011
Posts
410
Reaction score
159
​
Apple wamerudi na mshindo mkubwa baada ya wengi kudhani kuwa kampuni hiyo sasa imeanza kuanguka, hasa kutokana na presha wanayoipata kutoka kampuni ya Korea ya Kusini Samsung. Mshindo huo imefuatia Apple kutangaza bidhaa na software mbali mbali katika mkutano wa watengenezaji wa Apps WWDC 2013. Apple wametangaza kutoa toleo jipya la kompyuta ambayo si kivutio cha wengi, hasa wale wanaopenda umbile la bidhaa (design) ambao hupendezeshwa zaidi na iMac. Kompyuta hiyo ni Mac Pro ambayo imetolewa na umbile la aina yake ikiwa na muonekano kompyuta ya karne ijayo.


Ikiwa na umbile la mzunguko mithili ya chupa fulani na udogo wa kushangaza, kompyuta na hiyo sio tu imetolewa na umbile jipya bali pia imekuja na kasi na nguvu ya hali ya juu, ambapo katika historia ya Apple hawakuwahi kutoa kompyuta yenye kasi ya namna hii. Kwa upande wa graphics kompyuta hiyo ina GPU mbili (dual GPU), graphics card hiz itakuwa na uwezo wa kutoa mpaka 7 teraflops, ukilinganisha na Mac Pro ya sasa ambayo yenye uwezo wa Teraflps 2.7 tu, hili ni ongezeko kubwa mno. GPU hiyo ni AMD FirePro yenye 6BG VRAM maalum kwa ajili ya graphics tu (dedicated). Kompyuta hii itakuwa na uwezo wa kuhimili 4K video.


​
Tukiingia kwenye masuala ya CPU, MAC Pro mpya itatumia Xeon E5 ambayo ni toleo jipya, itaruhusu kuwa na core hadi 12, Apple wametangaza kuwa CPU hiyo itafikia kasi ya 40GB/s ikitumia PCI Express toleo la 3. Mac Pro hii kwa upande wa prosesa itakuwa na kasi mara mbili ya Mac Pro zilizopo sasa hivi. Kompyuta hiyo pia itakuwa na channel nne za DDR3 kwa upande wa RAM zikiwa na kasi ya 1866MHz, hivyo RAM hizi zitaweza kuchapa kazi nzito bila ya mashaka yoyote ikiwa na bandwith ya 60GB/s, nayo pia itaizidi kasi Mac Pro iliyopo kwa mara mbili zaidi.


Tukiingia kwenye uhifadhi wa mafaili (storage), Mac Pro mpya itatumia drive aina ya PCIe flash yenye kasi ya kusoma 1250 MB/s, tukilinganisha na SATA Flash yenye kasi ya 500 MB/s na SATA Hard Drive yenye kasi ya 110 MB/s bila ya shaka kompyuta hii itakuwa na kasi isiyo na kifani. Kwa kifupi mizunguko ya usomaji itakuwa mara kumi zaidi ya 7200-rpm, yap mara kumi!

​
Kompyuta hii pia ina port za kutosha, awali itakuwa na port mpya kabisa aina ya Thunderbolt 2, USB 3 Gigabit Ethernet na HDMI 1.4. Thuderbolt 2 itakuwa na kasi ya bandwith 20GB/s, port ya thunderbolt 2 peke yake itaruhusu kuunganisha vifaa mpaka 36 kwa mujibu wa taarifa ya Apple iliyotolewa kwenye WWDC 2013. Thunderbolt ni port ambayo inatumika kwenye vifaa vya Apple pekee. Pia uwepo wa HDMI 1.4 kwenye kompyuta hii maana yake itakuwa na uwezo wa kuunganishwa na TV mpya za Ultra HD.


​
Kompyuta hii itakuwa na urefu ya sentimita 25.1 na upana wa sentimita 16.8 na umbile la mzunguko. Hivyo Apple wametumia umbile na udogo wa aina yake kiasi kwamba unaweza hata kuiweka kompyuta hii juu ya meza bila ya kuchukua nafasi kubwa. Mac Pro haitakuwa na DVD au CD drive yoyote, apple wanaamini kuwa DVD na CD katika kompyuta ni aina za media ambazo zimepitwa na wakati.

Kompyuta hii itatengenezwa nchini Marekani kinyume na kawaida ya Apple ambapo bidhaa nyingi kama vile iPhone na iPad hubuniwa Carlifonia na kutengenezwa Shengzu huko China. Huenda huu ndio mwanzo wa Apple kurudisha uzalishaji Marekani kwani kampuni hiyo imepata kashfa na matatizo mbali mbali huko China kufuatia wazalishaji wao kufanya mambo yasiyokubalika kwa viwango vya nchi za Magharibi katika uzalishaji viwandani ikiwa ni pamoja na malipo madogo kwa wafanyakazi, hii imesababisha Apple kuzungumzwa vibaya kwenye vyombo vya habari mara kwa mara.

Je Mac Pro itaweza kuvutia watumiaji wa kompyuta za Apple na hivyo kuiwacha iMac na kuhamia kwenye kompyuta hii? Jibu litapatikana baadae mwaka huu wakati kompyuta hiyo itkapoingizwa mauzoni katika maduka zaidi ya 300 ya Apple, mtandaoni pamoja na wauzaji wengine wa kompyuta.

​
Source: www.gajetek.com
 
Back
Top Bottom