Mabunge yetu

kama ni kubwa kuliko la uingereza na la kenya kulinganisha idadi ya wabunge wanapokuwa bungeni tunakosea. Ni lazima seats zetu nyingi zitaonekana zipo wazi.
eti wamefanya legislative forecast ili nxt time wasije kusumbuka tena kupanua
 
eti wamefanya legislative forecast ili nxt time wasije kusumbuka tena kupanua
ooh! Niliwahi kusikia bunge la uingereza ni dogo kuliko idadi ya wabunge na wamefanya hvyo makusudi kwa sababu wanajua sio wakati wote wa bunge, wabunge wote watakuwa bungeni.
 
. Halafu kutwa Bunge halijajaa hivi wanaenda wapi wakati wanatakiwa kuwa Mjengoni?
inawezekana kuwa ni wakati wa bunge ila mbunge na kazi nyingine muhimu nje ya bunge hvyo anaruhusiwa kutoka mjengoni. Pia anawezekana kuna dharula imetokea jimboni kwake. Ni nadra kukuta wabunge wote mjengoni kipindi cha bunge.
 
Jamani wacha bunge liwe kubwa idadi yaweza kuongezeka si kuna mikoa na wilaya mpya nchi inakuwa hii na maendeleo yanakuja wajameni
 
Nimependa mkao wa bunge la Kenya, ni rahisi sana kumkaba mbunge yeyote anayeongea upuuzi bungeni hata kama ni kwa kumfinya! Bunge letu ni la kifahari sana kiasi kwamba mbunge akiingia pale anasahau shida za wananchi wanaoishi kwa ukwaju na ubuvu nje kidogo tu ya jengo hilo mjini Dodoma na kwingineko.
 
  • Thanks
Reactions: Nzi
Tumeshajichanganya, tumeshajenga, acha wakae cha muhim watimize wajibu siyo kuiomba serikali kwa kitu ambacho ni haki yako. Ndio maana baadhi ya haki za raia viongozi huita msaada. Mfano ".... serikali imewasaidia sana wananchi wa Namanyerere kwa kuwapatia barabara ya kiwango cha lami....." Siyo msaada ni haki yao kwa kodi yao
Sema " tunashukuru kwa kuijenga kwa lami, siyo kw kuwasaidia.!

Mimi naona hata kushukuru hakupaswi...kama ni wajibu wao kutimiza majukumu yao kwa raia, then shukrani haina haja kutolewa....shukrani inapaswa kutolewa pale ambapo mtu/watu wamefanya jukumu ambalo halikupaswa kufanywa na wao!!
Hili jambo pia uwa linanishangaza sana...unamsikia mbunge anaanza kuiomba serikali ipeleke umeme kwenye jimbo lake!! ivi huyu mbunge anakua ana akili kweli!! Kwanini aiombe serikali badala ya kuitaka na kuiagiza?! Afu huyo huyo mbunge baada ya kupata umeme, anaishukuru serikali, ivi hajui kama serikali inatimiza wajibu wake kupitia kodi za wananchi?!
 
Jamani wacha bunge liwe kubwa idadi yaweza kuongezeka si kuna mikoa na wilaya mpya nchi inakuwa hii na maendeleo yanakuja wajameni

Hili ni tatizo. Kwanini kila mara majimbo ya uchaguzi yaongezeke? Hatuwezi kuwa na fixed constituencies? Hatuwezi kuwa na fixed regions na districts? Kuwa na ongezeko la majimbo, wilaya na mikoa kila mara si indicator ya maendeleo!!

Wenzetu Kenya, juzi wameamua kupunguza idadi ya kata kwa kuzinganisha ili pia kupunguza idadi ya madiwani.

​Sisi hapa kila kukicha tunaongeza....!!!!!!!!!
 
Kuna haja ya kuubadilisha ukumbi wa Bunge letu TZ ukae kikazi zaidi. Umekaa kianasa sana ndio maana wanaotafakali kwa kina ni wengi. Halafu kutwa Bunge halijajaa hivi wanaenda wapi wakati wanatakiwa kuwa Mjengoni?

Wana sign kitabu cha mahudhurio haoo 'kupumzikaaaa'
 
Wanasiasa wa Tanzania wanajipenda sana!! Bunge kubwa lote la nini wakati nchi ni masikini,..na kinachojadiliwa ni utumbo especially wabunge wa ccm.
 
3.bp.blogspot.com/-FmVG5vm28NU/TgDhXBloFoI/AAAAAAAAADU/Xud4o_wd10s/s1600/wasira%2Bchapa%2Busingizi.jpg
 
:juggle:kwa stahili hii kwanini wasilale? watajuaje kama wananchi wanashida na wakati wao hiyo shida hawaioni na kila wanachataka kwa maslahi yao binafsi wanapata, ni vigumu Tz kuendelea labda sisiem itoke madarakani.
 
hivi tukiwa na mabunge kama ya wenzetu vipi tutaweza kupumzika baada ya kazi ngumu ya usiku mzima kuwahudumia wahudumu wa bar na sherehe za kupongezana
Lazima tuwe na nafasi ya kutosha nji hii ina nafasi kubwa sana na wananchi ni wachache
 
Si kwamba wamebanana ila pia wamehudhuria kwa wingi ninadhani ni ajabu sana kwa Mbunge kukosa session eti amehudhuria kikao cha Klabu, RAIS anatembelea jimbo, anatakiwa kufungua mkutano wa SACCOS jimboni ana wageni toka jimboni (shit!!!) anahudhuria semina fulani ya posho etc
 
Tukumbuke kwamba Uingereza ina mabunge mawili (House of Commons na House of Lords).. na hii picha inaonyesha mojawapo.
Ila pia uamuzi wa kudumisha historia ya jengo lao ndio unaofanya wabanane humo ndani..Ni uamuzi wa muda mfefu uliofanywa na waziri mkuu Winston Churchill wakati likijengwa upya baada ya kubomolewa na moto vitani.

Sisi hatuna historia yoyote ya kulinda na hivyo sioni tatizo kuwa na jengo la kisasa.
Ila kama hiyo itasababisha watu walale usingizi au kushawishika kuongeza idadi ya wabunge ili kulijaza basi tutakuwa tuna matatizo makubwa.

Je ni kweli hatuna historia ya kulinda? Historia ya kulinda tunaweza kuwa nayo lakini kwa vile watawala wetu wamejaa ufisadi wangeweza kubomoa jengo la historia na kujenga jipya ili mradi wapate 10% yao!! Si uliona jinsi watawala walivyochachamaa kutaka kuvunja jengo la FORODHANI HOTEL ili wampe mwarabu anaemiliki Kilimanjaro hotel ili atengeneze parking lot kwenye hiyo sehemu!!
 
Back
Top Bottom