Mabomu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabomu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jumakidogo, Feb 18, 2011.

 1. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #1
  Feb 18, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  p { margin-bottom: 0.08in; }

  Jengeni makambi ya Jeshi huko porini


  Na Juma Kidogo


  Kwanza kabisa napenda kutoa pole kwa familia na watu wote waliohusika moja kwa moja na kulipukiwa na mabomu yale huko Gongolamboto.
  Pili napenada kutoa pole kwa Watanzania wote kwa ujumra kwani tumepoteza ndugu zetu katika ajali ambayo ingeweza kuepukika iwapo Serikali yertu ingekuwa makini, sikivu, pamoja na kuzingatia maoni ya watu.
  Si jambo jema kabisa kutokwa na uhai katika tukio ambalo lingewezaa kuepukwa iwapo tu serikali yetu ingezingatia umuhimu wa kujenga kambi za jeshi pamoja na maghara ya kuhifadhia silaha hizo hatari mbali na makazi ya watu. Viongozi wetu wa sasa na wabishi, wasio wasikivu na tena si wepesi wa kuzingatia maoni na mawazo ya wale wanaowatawala.
  Inashangaza sana, inashangaza kwani kambi hizo zilijengwa zamani enzi za mwalimu, hapa utaona kuwa mwalimu alikuwa akijali uwepo wa raia wake pmoja na haki zao za msingi za kuishi ndio maana wakati huo makambi hayo ya jeshi yenye maghara ya silaha yalijengwa mbali na makazi ya watu.
  Kulikuwa na kila sababu kwa serikali yetu sasa kuona uwezekano wa kuhamisha makambi hayo mapema kabla madhara makubwa hayajatokea kwa binadamu. Pia uwepo mpango wa makusudi kabisa wa kuharibu silaha zote ambazo zimepitwa na wakati, silaha ambazo zina kila dalili kuwa muda wake wa matumizi sasa umekwisha. Tumeshuhudia mabaki ya mabomu chakavu yenye kutu.
  Mabomu yenye sura mbaya utadhani yalitumika tangia enzi za vita kuu ya kwanza ya dunia. Ni aibu kubwa kwa nchi na jeshi letu kuhifadhi mabaki ya mabomu ambayo yalitumika tangu enzi za vita ya kumtoa Nduli Idd Amini zaidi ya miaka 30 iliyopita.
  Serikali yetu haithamini maisha ya watu, haina habari kabisa na wanachi hawa ambao wanaishi kwa mateso makubwa kutoka na mzigo mkubwa wa gharama za maisha kupanda.
  Hayo kama hayatoshi wananchi tunaaongezewa mzigo mwingine wa kupigwa na mabomu kwa makusudi na kuporwa uhai wa ndugu zetu wasio na hatia.
  Fidia haitoshi, fidia haitoshi hata chembe kwa wale ambao uhai wao umpotea bure. Itashangaza sana iwapo waziri wa ulinzi pamoja na mkuu wa majeshi iwapo wataendelea kubaki madarakani baadala ya kuwapisha watu wenye uwezo pamoja na mipango madhubuti ya kudhibiti majanga haya. Mungu azilaze roho za marehemu waliopigwa na mabomu kwa makusudi mahala pema peponiĀ….. Amina
   
 2. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #2
  Feb 18, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Maporini ndiyo wapi?
   
 3. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #3
  Feb 18, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  mi nilijua yameanza tena!
   
Loading...