Wana JF,
Wajua huwa naijiuliza hivi Jeshi la Police nani huwa anawapa kiburi cha kuamua maamuzi? Kwanini ansema hayo
Majuzi uko Arusha CDM walikataliwa maandamano ya kupinga Mayor wa Arusha na sababu zilizo tolewa na Police ni kuwa CDM hawakupeleka taarifa za Maanadamano ndani ya Masaaa 48, na wakasema kwa ajiri ya usalama ni bora kutoa taarifa mapema.ila waandamanao wapewe ulinzi wa kutosha.
CUF walitoa barua kwa police tarehe 21 Dec 2010 kuwa watakuwa na maandamano ya kutoa mapendekezo yao ya katiba mpya sasa sielewi Police wetu hawa wao wanachopinga nacho ni nini na wanachokitaka ni nini au wao ni kufuata order toka kwa wakubwa hivi Katiba haitawahusu wao au?
Inamaana Police yetu haina watu wa kukaa na kutathimini kuwa ni nini kifanyike sasa na nini kisifanyike au wao ni kukurupuka tuu na kupewa order sishangai Jeshi la police kuwa linadharauliwa kihasi hiki wao wamekuwa wa kuambiwa tuu basi na kutii.
Sasa hapa watuambie walikuwa hwajajiandaa kiusalama napo au? Tanzania hii nani anataka kufanya vurugu kama maandamano yatakubaliwa kwa amani???? Police ndio chambo wa wakubwa na kuchochea vurugu hilo wasijaribu kuliepuka