1.Mtego wa Noti « sasa mbona wanajibishia wenyewe? kwani wao si wako ndani ya serikali? sasa mbona wanatuchanganya?....anyway....ngoja wapigwe virungu...
....na bado.... «
2.Ledman Mtana. « Wanataka serikali ya mseto na bara. wameshaonja utamu huko zenji sio? »
3.Buchanan. « CCM - A inapambana na CCM - B, kaaazi kweli kweli! »
4.Maishapopote. « Hahahahhaha wavunjwe hata miguu »
Great thinkers
Munajidhalilisha kama uwezo wenu wa kufikiri ndio huu !
Yaani mtanzania mwenzako,anapigwa, anajeruhiwa au anauawa katika dai ambali wewe pia ungeandamana kama chama Chengine cha siasa kingeitisha maadamano hayo, sijui niite tabia gani !!
Hayo ya Polisi kupiga CUF inafaa muone kuwa CUF sio chama tawala kama wengi humu munavyotaka tuamini.
Halafu hili la kusema CUF kaolewa au wanalala kitanda kimoja inaonesha wazi vipi mawazo yetu yametawaliwa na fikra ya unyanyasaji wa kijinsia katika mila za hapa Tanzania. Tunaona wanawake ni watu wa « kufanywa tu »,kudharauliwa.
Tumesoma lakini hatujaelimika ! Fikra potofu. Munawatukana, munawadhalilisha mama na dada zenu na hizo dharau munazipeleka katika ulinganisho hata wa kisiasa.
Siku kibao kikiwageukia , nitawakumbushia thread hii.
Badilikeni kama tunataka mabadiliko ya kweli.