BIG X
JF-Expert Member
- Nov 4, 2011
- 777
- 212
Mi nadhani kuna haja kubwa ya kufanyika tafiti za uhakika kuhusu madhara yanayosababishwa au yatakayosababiswa kwa wananchi kutokana na mabomu ya machozi hasa kwenye suala zima la Afya. Askari wetu wamekuwa wakijipigia ovyo haya mabomu. Na wakati mwingine waathirika sio wale ambao wamelengwa moja kwa moja. mfano mbeya mabomu ya machozi yametupwa mpaka ndani ya vituo vya afya (angalia picha) na kusababisha wagonjwa kukimbia wodi, wauguzi kupatwa na presha wakiwa kazini, huu ni unyanyasaji mkubwa. Watu kama hawa serikali inabidi iwafidie kwa madhara ambayo watakuwa wameyapata.
Vitanda vilivyokuwa vikitumiwa na wangonjwa katika Zahanati ya Ipinda, iliyopo Mwanjelwa jijini Mbeya vikiwa wazi baada ya wagonjwa kukimbia mara baada ya bomu la machozi lililopingwa na Jeshi la polisi kutua ndani ya Wadi.
Mgonjwa aliyekuwa akitibiwa Zahanati hapo akiwa amezirai baada ya bomu la machozi lililopingwa na Jeshi la polisi kutua ndani ya Wadi.
Wauguzi waliozirai wakiwa nje ya Zahanati mara baada ya kutibiwa
Mganga Mkuu wa zahanati ya Ipinda jijini Mbeya Dk. Lute Kibopile ambaye pia ni mmiliki wa zahanati hiyo akielezea jinsi bomu la machozi lilivyopingwa.
Muuguzi akionesha eneo ambalo bomu la machozi lilipotua katika Zahanati ya Ipinda, eneo la Mwanjelwa jijini Mbeya.
Mtaalamu wa masuala ya maabara katika Hospitali ya UHAI BAPTIST Dk Ngangele Lisukile akiwa ameshika kigae kilichodondoka mara baada ya bomu la machozi lililopingwa hospitalini hapo majira ya saa 5:30 asubuhi.
Haya ni yale tu yaliyotokea mbeya. Ni uhakika na sehemu zingine yapo zaidi haya. Kwahiyo mi nadhani tafiti ziwe zinafanyika kujua madhara ya haya mabomu ya machozi na watu wawe wanafidiwa.