Mabomu ya DRC yatua Ngara

johnmashilatu

JF-Expert Member
Sep 16, 2010
605
500
Wakazi wa kijiji cha Ruganzo kata ya Kibimba wilayani Ngara mkoani Kagera wamekubwa na hofu baada ya kitu kinachosadikiwa kuwa kipande cha kombora kuanguka kwenye eneo lao


Wakazi hao wamesema kitu hicho chenye umbo la yai, kikiwa na nyuzi nyuzi na ukubwa wa sentimeta 50 kianguka jirani na uwanja wa ndege ulioko kjiji hapo usiku wa kuamkia leo

Wakazi hao wamesema kitu hicho huenda na kipande cha kombora kilichoanguka kwenye eneo lao kutokana na mapigano yanayoendelea katika ejeo la mashariki mwa DRC ambako ni jirani na Ngara

Mkuu wa wilaya ya Ngara Bw Costantine Kanyasu ammbaye amefika kwneye eneo la tukio amesema hakuna mtu ambaye kwa sasa anaweza kutambua kitu hicho, hivyo wamewaomba wataalamu wa mabomu kutoka kambi ya Jehsi la Biharamulo ili kuweza kukitambua na kukishughulikia

"Binafsi sijawahi kuona kitu kama hiki, labda ni kimondo lakini tuwasubiri wataaalmu watatoa taarifa zaidi juu ya kitu hiki"

Katika hatua nyingine wakazi wa kata za Kabanga na Mugoma zilizoko mpakani mwa tanznaia na Burundi wamesema usiku wa kuamkia leo wamesikia milio ya bunduki wakidai inatokea DRC ambako wasi w akundi la M23 wanapambana na majehsi ya serikali

Diwani wa kata ya Kabanga Bw Said Suod amesema usiku wa kuamkia leo wamesikia milioni ya silaha inayosadikiwa kutokea nchini DRC
 

Kitoabu

JF-Expert Member
Jul 7, 2011
5,890
2,000
Kwahiyo mpaka sasa ni juudi gani zinazo endelea? Naomba unijuze mkuu maana ukweni huko dah
 

PMNBuko

JF-Expert Member
Dec 27, 2010
967
0
Duh, fuatilia mkuu maana huko ni nyumbani mwana. Poleni jamani, ngoja nipige simu kuuliza hali ilivyo Kabanga na Ruganzo.
 
Top Bottom