Mabomu Mengine Kulipuka??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabomu Mengine Kulipuka???

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Maishamapya, Feb 21, 2011.

 1. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #1
  Feb 21, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Kutoka majuzi (Ijumaa) niliposikia kauli ya Brigedia Jenerali Paul Meela akizungumza na waandishi wa habari kuwa tukio la kulipuka mabomu la mbagala halijajirudia nimekuwa nikitafakari sana juu ya usalama wetu watanzania. Naomba kwanza ninukuu kauli ya kamanda huyu wa jeshi:

  "ni kweli halijajirudia, kwa maana lile lilitokea Mbagala, hili limetokea Gongolamboto"

  Kauli hii inanifanya nishtuke kwa maana kuwa hii ni taarifa rasmi ya jeshi kwa wananchi kuwa watarajie mabomu mengine kulipuka kutoka kwenye kambi nyingine kama Mabibo, Changanyikeni, Kimara, Kawe, Kigamboni, Boko, Kunduchi na kwingineko. Na kauli watakayopewa na walinzi wao ni kuwa hayajajirudia huko yalikolipuka mwanzo. Nashtuka mno ninapoona kauli hiyo ikitolewa na Brigedia Jenerali wa jeshi letu kupitia vyombo vya habari. Je, tunatangaziwa hali ya hatari au vipi? Hivi wanatuambia nini? kwamba nchi yetu si salama tena?

  Kwa bahati mbaya sana wakuu wetu hawataki kuuzungumzia usalama wa nchi yetu. Spika Mama-wa-makinda hakutaka lizungumziwe huko bungeni. JK na Pinda wakakwepa kulizungumzia. Matokeo yake watanzania wanapewa kauli za kijeuri kama hizo. Tafsiri yangu kwa kauli ya Brigedia Jenerali Meela ni kuwa Watanzania wanaokaa karibu na kambi za jeshi popote pale walipo Tanzania watarajie mabomu kuwalipukia wakati wowote. Hawako salama kabisa kwa vile ndivyo wanavyosema wale waliowapatia dhamana ya kuwalinda. Hii ni hali ya mashaka makubwa sana.

  Kwa kifupi ... TUISHI KWA HOFU!!!

  Brigedia Jenerali Meela anapaswa awaombe radhi watanzania wanaomlipa mshahara kwa kutoa kauli ya mzaha kama hiyo.
  Naomba kuwasilisha.

   
Loading...