Mabomu Dar: Ni Incompetence au CCM in Action? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabomu Dar: Ni Incompetence au CCM in Action?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kamanzi, Feb 18, 2011.

 1. k

  kamanzi Member

  #1
  Feb 18, 2011
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 99
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Kwanza nianze kwa kusema ni aibu isiyo na kifani kwa waziri wa ulinzi kuthubutu kusema milipuko ya mabomu ilikuwa ni ajali. Wakisema wananchi kuwa ni ajali inaleta akili ila kwa wanajeshi waliofunzwa kuruhusu hiyo "ajali" itokee ni incompetence at its very best. Na haswa ukizingatia kuwa miaka miwili iliyopita kulitokea milipuko tena. Kama ni incompetence basi wale waliokuwa wakinibishia nilipowakataa hawa watoto wa viongozi wa kisiasa kama Januari Makamba kurithi uongozi wanitake radhi. Huyu mtoto wa Mwinyi ambaye ndie aliyekuwa waziri wa ulinzi hata wakati wa mabomu ya mbagala anaonyesha hana clue kabisa ni kilitokea na nini kinaendelea katika wizara yake. Ingawa kwa sehemu sishangai maana wakati majeshi mengine yapo serious na ulinzi na uslama wa nchi, JWTZ ipo busy kuhakikisha Dr Dr Dr anainsgia ikulu. Si mnamkumbuka yule jamaa aliyeita press conference kusema vyama vikubali matokeo kabla hata kura kupigwa?

  Najiuliza hivi hizi "taharifa za kiintelijensia" wanazosema kila leo huwa zinapatikana wakati wa kupiga mabomu wanaoipinga CCM tu? KWanini zisipatikane ili kuepusha vifo kama hivi vilivyotokea Gongo La Mboto. Nasema nina wasiwasi kuwa ipo siku kama mambo yataendelea kuwa hivi watalipua nyumba ya Dr Slaa au makao makuu ya CHADEMA na kusema bila aibu kuwa ni "Ajali". Ama kweli Tanznai kichwa cha mwendawazimu, maana kila incompetent Tom and Jerry anaweza kuwa waziri na akiambiwa awajibike anaruka na kusema ni ajali.
   
 2. GATS

  GATS JF-Expert Member

  #2
  Feb 18, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 240
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hawa watu wanamatatizo siwapendi kabisa. Kila ninapowasikia ninapata hasira sana. Wao ndio waliotufanya tuwe hivi tulivyo.
   
Loading...