Nichangie Kidogo Kwa kile ninachojua..
Kwanza unapaswa kujua Lengo (maudhui) lako kubwa la kuanzisha blog ni nin asa
mfano we unataka kwa ajili ya kutangaza biashara yako au kwa ajili ya kutoa Elimu juu ya jambo flan mfano Afya, Tech, au Dini. Au unaweza ukawa unataka kuanzisha kwa ajili ya Habari.
Pili unatakiwa kujua walengwa wa blog yako au wasomaji wako watakuwa watu wa aina gani hii itakusaidi kujua ni wapi paku wapata watembeleaji au wasomaji wa blog yako.
Tatu Jina la Blog yako... hapa ndipo wanapo chemsha.... Unapaswa kuwa na jina linaloendana na blog...
Mfano blog yako inahusiana na makala za michezo inakupasa kuchagua jina ambalo lina maudhui ya kimichezo na si vinginevyo.... Hii itakusaidia hata kupatikana kiurahisi kwenye search engine kubwa kama Google.. Pia unashauriwa kuchagua jina fupi na linalo tamkika kirahisi.... hii itasaidia kukumbukwa kwa urahisi na kuwa na Unique visitors.
La nne ni Template au Design.. Hakikisha blog yako ina mwonekano mzuri, wa kipekee na wa Kuvutia.. Blog kuwa na mwonekano mzuri humfanya mtembeleaji kuipenda na kurudi mara kwa mara kusoma habari zako... Kingine inapaswa kuwa mobile friendly, asilimia kubwa ya watu kwa sasa ni watumiaji wa internet na wengi wakiwa wanatumia simu Janja hivyo hata watembeleaji wengi wa blogs hutumia simu kuperuzi.
Tano ni Uandishi: Wengi wana blog nzuri na zenye sifa karibu zote ila linapokuja swala la uandishi ndipo tunaposhindwa.... Jaribu kuwa wakipekee... Andika habari nzuri na kwa mpangilio mzuri epuka ku copy na Kupest pia andika vitu vitakavyomfanya mtembeleaji kurudi tena kesho.......
Sita na Mwisho kwa leo ni Kuitangaza.
Hii ni muhimu sana kwani blogs kwa sasa zipo nyingi sana kwa hapa tuu tanzania zinaweza zikawa zinafika hata 1000+.... Tumia mitandao ya kijamii kuitangaza kwa kutengeneza funpage kama Facebook, Instagram, Twitter, Whatsapp, Snapchat nk. Hakikisha unapo andika habari mpya una share kwenye hiyo mitandao ya kijamii... Pia unaweza kutumia matangazo ya kulipia kama Facebook +Instagram hapo unaweza tangaza hata kwa $2 pia kuna Google adwords unaweza kutangaza pia kupitia Email marketing mfano mzur MailChimp wanakupa free acount
YOTE HII NI KUIFANYA BLOG YAKO KUJULIKANA NA KUWA NA WASOMAJI WENGI.
Naomba niishie hapo kwa leo japo Yapo mengi ya kuandika kuhusu tasnia hii ya bloger nadhani wengine nao wata changia.