Mabinti zangu, naongea na wewe binti yangu

timetoloveyourself

JF-Expert Member
Mar 24, 2015
206
206
Mabinti zangu

Unasema, "kila mwanaume anayekuja kwangu ananitaka kimapenzi anautaka mwili wangu sipati wanaume serious.

Wanaokubali kuwa na mimi bila kutaka 'asali yangu'...."

Jibu ni rahisi: wewe umeweka mazingira ambayo yanawafanya wakikutazama waone makalio, lips, maziwa, sehemu za mwili wako umeziacha kama nyama ya bucha, unategemea watafanyaje?Kaaah! Watataka tu kujipimia binti yangu.

Ukipigiwa simu na hao wanaume nnaongea vitu vinavyolenga au kugusia mapenzi, ngono, habari za kitandani na kadhalika.Unataka mwisho wa siku wafanyeje?

Kiwango cha heshima uliyonayo, unayojisitiri nayo, ndiyo inayoamua mwanaume ataongea na wewe mpaka wapi!

Ukimpa ruhusa ya kuzungumzia mwili wako au sehemu za mwili wako, baada ya muda atataka kuugusa baada ya kuugusa, atafanya na yale majanga!

Wewe umekaa kingono ngono, unaongea kingonongono, unakutana naye, mazingira yanayohamasisha ngono, halafu unataka akuangalie kama padri?

We endelea kuwa na maisha yako hayo ya kingonongono halafu uone kama wanaume wataaacha kukuchezea na kukuacha!

Naongea na wewe binti yangu vile unavyojiweka mbele ya mwanaume, Itaaamua nini kitafuata ITV!

Hakuna bahati mbaya kwenye dhambi ya uzinzi.

Salamu za kibabu babu.
 
Sasa tutaishije maana wadada poa na wakaka poa ndo hivo tena camanda Siro amekuwa nao mbogo?
 
kiuhalisia wanauwe wanaongoza kwa kuomba papuchi lakini kiukweli wanawake ndio wenye hamu zaidi ya ngono
 
Back
Top Bottom