Mabinti wengine majanga!!!!

chakii

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
21,885
Reaction score
29,675
Habari zenu wanaMMU,.

Hii imetokea juzi wakati narejea kutoka mjini kujipatia matumizi yangu kuelekea mwisho wa wiki,.

Baada ya kujipatia mahitaji yangu nilielekea kituo cha basi na kupata siti ya nyuma kwenye basi ambapo kwenye siti hiyo alikuwa amekaa kijana wa kiume ambaye simfahamu akiwa amekaa na binti ambaye huwa namuonaga mtaani nikimaanisha siyo mgeni machoni pangu na bila shaka mimi siyo mgeni machoni pake maana anauza duka la dawa ( pharmacy) na mimi mara nyingine huwa naenda kununua panadol kwake, nikajichukulia siti na kukaa baada ya kuwasalimia ambapo wote walionekana kuwa bize sana na mazungumzo yao na sina hakika kama waliniitikia maana walishazama maongezini utadhani wao peke yao ndiyo waliokuwa kwenye basi!!

Back to the topic,.

Muda ulivyosonga huku mimi nikaendelea na mambo yangu Jf kidume akaagiza soda mbili za chupa (take away) , yaani ya kwake na ya kale kabinti!! Soda zikaletwa na jamaa kwa vile aliagiza mbili ile moja akamkabidhi bibie,. Bibie akaikataa ile soda akasema hakuwa na shida ya soda hivo haihitaji,. Jamaa akambembeleza sana yule binti maana ilishafunguliwa ile soda hivyo jamaa asingeweza kuirejesha kwa muuzaji labda anywe zote mbili mwenyewe,.. Kadri muda ulivyokwenda bibie alishikilia msimamo wake mpaka tunaondoka stendi ndipo jamaa ikambidi aichukue ile soda anywe zote mwenyewe!!

Sasa kidume akabadilisha mada na kuanza kumtongoza yule binti hadharani nikimaanisha tuliokuwa tumekaa siti ya nyuma tulikuwa tukisikia kila neno lililokuwa likitoka kwa yule mwanaume, mrejesho kutoka kwa binti ndiyo ulikuwa kero zaidi maana alikuwa anaropoka kabisa kiasi kwamba abiria wote walikuwa wakimgeukia yule binti,. Hadi nashuka kwenye lile basi hali ilikuwa tete sana maana abiria walikuwa wamekereka sana na kelele za yule binti!!

Ombi:

Mabinti mkitongozwa kuweni wapole basi, haina haja ya kukera wengine au kutoa sauti zenye kukera watu wengine ukizingatia watu wa pembeni hawatakiwi kujua nini kinachoendelea kati yenu wawili!!
 
sasa funguka vzr alikuwa hataki au anakubali? nini haswa kiliwakera nyinyi abiria wengine?
 
Itanibidi niwe natumia bus kila siku labda nitajifunza kuepukana na hili domo geze, yaani walitongozana hadharani! mleta mada naomba niwekee maneno zaidi walivyokuwa wakiongea.
 
Itanibidi niwe natumia bus kila siku labda nitajifunza kuepukana na hili domo geze, yaani walitongozana hadharani! mleta mada naomba niwekee maneno zaidi walivyokuwa wakiongea.

kwani wewe hujawahi kutongoza mkuu!!
 
Ngoza niendelee kuona Simba anavyofungwa mie!
Mmmh!
Mada za leo bhana!
 
M naona wote majanga manake mwanaume alikua anamtongoza binti na kila neno linasikika hvo na binti nae akajibu kwa sauti ilelile..........
 
Itanibidi niwe natumia bus kila siku labda nitajifunza kuepukana na hili domo geze, yaani walitongozana hadharani! mleta mada naomba niwekee maneno zaidi walivyokuwa wakiongea.

Napenda kuwa na mpenzi domo zege mana in reality me ni mpole balaa!!!!!!!
 
hadi mwisho yanga 3 simba 3 roho inaniuma kweli mi ni yanga damu uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!
 
Napenda kuwa na mpenzi domo zege mana in reality me ni mpole balaa!!!!!!!

Cc: mimi mwenyewe.

Hivi akiwa domo zege si mana yake utamtongoza wewe? Nakungojea mamii... ;-)
 
hadi mwisho yanga 3 simba 3 roho inaniuma kweli mi ni yanga damu uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!

mkuu unaweza kuanzisha thread yako na ukaelezea hisia zako huko!! Kuanika matapishi yako hapa si sawa, wengine tuna kichefuchefu na hayo mavitu!!
 
Bongo kwa ujumla hakuna faragha.

Tunahitaji kuongeza doctor/ patient confidentiality.

Tunahitaji kuongeza attorney/client confidentiality.

Tunahitaji kuongeza journalistic integrity to protect sources.

Tunahitaji kuongeza heshima kwa wengine tunapoongea in public.

Jamii zetu zina challenges nyingi sana za ku adapt tourbanization, kwenye mambo ya public transportation na mikutano ya watu wengi.
 
Itaje basi dialogue yao hata kwa mistari mi 4 hivi then narudi ku comment
 
Cc: mimi mwenyewe.

Hivi akiwa domo zege si mana yake utamtongoza wewe? Nakungojea mamii... ;-)

Mentor wewe ni mkali,naomba unifundishe basi kutongoza,huyu usipoondoka naye sijui
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…